Yanga hujipa majina yanayowakera wao

DullyJr

JF-Expert Member
Apr 10, 2011
13,979
11,816
Ni majina mangapi ya utani ya klabu ya Yanga umeshawahi kuyasikia maishani mwako?

Kama wanavyosema wahenga, ukiona nyani mzee ujue amekwepa mishale mingi. Basi kwa ukongwe wa Yanga ni lazima imekutana na majina mengi sana.

Hata jina la Yanga, limetokana na wao wenyewe na wengine kushindwa kutamka jina la Young Africans na hatimaye hadi leo kufahamika kwa jina hilo lenye umaarufu mkubwa. Lakini kitu ambacho unaweza kushindwa kuamini ni kwamba majina haya kwa asilimia kubwa wamejipa wenyewe.

Baada ya kukerwa na jambo fulani, mara nyingi huwa matokeo, mmoja wao huibuka na kuropoka neno ambalo huja kugeuka kuwa jina lao la utani ambalo wapinzani wao hulitumia kuwanyima raha.

Hivyo ndivyo majina kama Gongowazi, Kandambili, Yeboyebo, Utopolo hayo ni kwa uchache tu, yalivyoanza na sasa kuna jina jipya!

WALA MIHOGO
Bila shaka utakuwa umesikia siku mbili hizi mashabiki wa Yanga wakitaniwa wao ni wala mihogo. Kama hujasikia basi chukua hiyo, mashabiki wa Yanga kwa sasa wamepumzika kuitwa Utopolo, sasa ni Wala Mihogo.

Jina hilo limekuja kama mapokeo ya kauli ya Rais wa klabu hiyo, Mhandisi Hersi Said, alipokuwa akizungumza na viongozi wa matawi majuma mawili yaliyopita, alitumia kauli tata kuwalenga ‘mashabiki matokeo’ wa klabu hiyo ambao huwalaumu viongozi kila wakati timu yao isiposhinda.

“Achilia mbali mtu mwingine, Gharib (GSM) hawezi kwenda uwanjani, kwa presha aliyokuwa nayo. Anakaa pale, na ukimuona vile anavyokaa, natamani siku moja - Frank eh, naomba siku moja uichukue ile video, tuwaoneshe hawa wanachama wajue huyu mtu anaumia kiasi gani - hakai chini. Mara kashuka kwenye kochi, mara kakaa hivi...mara kakaa hivi.

Mke wake anamuuliza baba vipi, ‘achana na haya mambo ya mpira yatakuja kukuua.’ Huyo ni mtu anayewekeza fedha zake kwenye kusapoti timu. Anawekeza nguvu zake kwenye kuisapoti timu. Ana mapenzi na timu...hali hiyo ndiyo inamkuta.

Sasa kuna mtu yeye kala zake mihogo huko, ‘sisi timu inatuuma zaidi. Nyie viongozi nyie, sisi ndiyo tunaumia”

Mhandisi Hersi aliitoa kauli hii jijini Mwanza, Oktoba 28 mwaka huu katika Ukumbi wa Bwalo la Jeshi alipokuwa akiongea na viongozi wa matawi ya wanachama na mashabiki wa klabu hiyo kuelekea mchezo wao wa Ligi Kuu dhidi ya Geita Gold.

Kauli hii ilipokelewa vizuri sana tena kwa makofi bwaloni pale lakini baada ya sare ya 0-0 nyumbani dhidi ya Club Africain, ndipo mapokeo yakabadilika.

Wale mashabiki wala mihogo ambao Hersi aliwalenga, wakafanya remontada ya hatari na kurudisha mashambulizi kwa Rais wao. Mapovu yakawatoka na ndipo wapinzani wao wakaidaka na kuteleza nayo.

Kwa sasa habari ya mjini ni MIHOGO, sasa sijui ni mihogo ya Chanika au Jang’ombe?

KANDAMBILI
Mwaka 1975 Yanga ilikumbwa na mgogoro ambao kimsingi ulifukuta kuanzia 1968. Mgogoro huo ambao chanzo chake ni mtafaruku uliotokana na ujenzi wa ofisi za makao makuu za Jangwani na Uwanja wa Kaunda, ulisababisha kukosekana amani klabuni hadi ulipokuja mpasuko wa 1976 uliozaa klabu mpya ya Pan Africa.

Mwenyekiti wa Yanga, Mangara Tabu Mangara na kundi lake akiwemo aliyekuwa mfadhili wao, Shiraz Shariff, walifanyiwa mapinduzi Julai 1975 lakini serikali ikayapinga.

Siku moja timu ikiwa mazoezini Uwanja wa Kaunda, wanachama wakaja na kelele zao kushinikiza Mangara awaachie timu yao.

Kelele hizo zikawafikia wachezaji na Uncle J, Juma Pondamali alipozisikia, akawajibu kwa dharau kwamba, ‘hata nyie wavaa kandambili zenu mnaweza kusema kitu mbele ya wenye fedha?

Hapo ndipo jina la kandambili lilipoanza.

Wakati huo watu wenye fedha walikuwa wakivaa viatu virefu yaani ‘rise on’ lakini waswahili waliita raizono.

Kwa hiyo moja kwa moja wale wenye fedha wakawa wavaa raizoni na wale masikini wakwa wavaa kandambiliWavaa kandambili wakapambana hadi uchaguzi ukafanyika Desemba 28, 1975 na wavaa raizoni wakashindwa.

Wakatoka na kwenda kuanzisha timu yao waliyooita Pan Afrika.

YEBOYEBO
Mwaka 2004 kampuni moja ya vinywaji hapa nchini ilikuja na aina fulani ya uji ulioitwa Yeboyebo. Mwaka huo kuna viatu fulani aina ya ‘sendoz’ iliibuka hapa mjini na kupendwa sana na ‘watoto wa mjini’.

Kwenye maonesho ya sabasaba, kampuni ile ya vinywaji ikaja na wazo la promosheni kwa ajili ya uji wao. Kwamba mtu ukinunua uji wa Yeboyebo, unapewa na zile aina ya sendoz...hapo ndipo sendoz zile zikaitwa yeboyebo na umaarufu wake ukazimika ghafla na kuwa viatu vya kishamba badala ya vya kijanja.

Asilimia kubwa ya viatu vile ilikuwa rangi ya njano na kijani, ambazo ni rangi rasmi za klabu ya Yanga.

Kwa kuwa Yanga ni kandambili na viatu vile vilikuwa jamii ya kandambili, basi jina la Yeboyebo likatoka kwenye vile viatu na kwenda Jangwani.

Kwa hiyo yeboyebo kimsingi ni mwendelezo wa Kandambili katika karne ya 21.

GONGOWAZI
Miaka ya zamani kabisa mpira ulichezwa bila jezi wala viatu hapa nchini.

Wachezaji walifunga bandeji miguuni ili kujikinga na ugumu wa ardhi na rafu za wapinzani uwanjani. Maisha yakaanza kubadilika na baadhi ya timu zikaanza kuvaa viatu na jezi, lakini Yanga ilichelewa kidogo. Safari moja shabiki mmoja wa klabu hiyo mwenye asili ya Asia alikwenda kutazama mechi, akashangazwa kuona wapinzani wao wamevaa jezi lakini wao wako migongo wazi.

Akaahidi kuwanunulia jezi akisema, ‘Hapana cheza tena gongo wazi’.

Hapo ndipo jina la Gongowazi lilipoanzia na kuendelea hadi leo.

UTOPOLO
Nenda kwenye kivinjari cha Google halafu andika Utopolo, litakuja jina la Yanga. Hili ni jina ambalo limejizolea sana umaarufu kwa miaka ya hivi karibuni.

Lilitokana na kauli ya shabiki wao mmoja aliyekerwa na matokeo na namna timu ilivyocheza kwenye moja ya mechi za Ligi Kuu.

Akihojia na moja ya vyombo vya habari hapa nchini, shabiki huyo akasema ‘Hii ni Yanga au Utopolo?’ Hapo ndipo jina la Utopolo lilipoibuka.

Lilipata zaidi umaarufu baada ya kuwa likitumiwa sana Haji Manara alipokuwa Msemaji wa Simba.

Wakati Yanga wakiwa kwenye harakati za kufanya mabadiliko ya kimfumo, walienda Hispania kutafuta ushauri wa kitaalamu.

Haji akawa anawatania kwa kusema wakirudi huko watabadili jina na kuwa Depotivo la Utopolo, akirejea majina ya timu za Hispania kama Depotivo la Coruna. Jina la Utopolo likawa maarufu zaidi na zaidi. Na sasa ni zamu ya wala mihogo.

Majina yote haya yametoka kwenye midomo yao wenyewe. Tusubiri mengine mengi yatakuja huko mbele

Ongezea lingine hapo chini

download.jpg
 
Ni majina mangapi ya utani ya klabu ya Yanga umeshawahi kuyasikia maishani mwako?”

Kama wanavyosema wahenga, ukiona nyani mzee ujue amekwepa mishale mingi. Basi kwa ukongwe wa Yanga ni lazima imekutana na majina mengi sana.

Hata jina la Yanga, limetokana na wao wenyewe na wengine kushindwa kutamka jina la Young Africans na hatimaye hadi leo kufahamika kwa jina hilo lenye umaarufu mkubwa.

Lakini kitu ambacho unaweza kushindwa kuamini ni kwamba majina haya kwa asilimia kubwa wamejipa wenyewe.

Baada ya kukerwa na jambo fulani, mara nyingi huwa matokeo, mmoja wao huibuka na kuropoka neno ambalo huja kugeuka kuwa jina lao la utani ambalo wapinzani wao hulitumia kuwanyima raha.

Hivyo ndivyo majina kama Gongowazi, Kandambili, Yeboyebo, Utopolo hayo ni kwa uchache tu, yalivyoanza na sasa kuna jina jipya!

WALA MIHOGO

Bila shaka utakuwa umesikia siku mbili hizi mashabiki wa Yanga wakitaniwa wao ni wala mihogo. Kama hujasikia basi chukua hiyo, mashabiki wa Yanga kwa sasa wamepumzika kuitwa Utopolo, sasa ni Wala Mihogo.

Jina hilo limekuja kama mapokeo ya kauli ya Rais wa klabu hiyo, Mhandisi Hersi Said, alipokuwa akizungumza na viongozi wa matawi majuma mawili yaliyopita, alitumia kauli tata kuwalenga ‘mashabiki matokeo’ wa klabu hiyo ambao huwalaumu viongozi kila wakati timu yao isiposhinda.

“Achilia mbali mtu mwingine, Gharib (GSM) hawezi kwenda uwanjani, kwa presha aliyokuwa nayo. Anakaa pale, na ukimuona vile anavyokaa, natamani siku moja - Frank eh, naomba siku moja uichukue ile video, tuwaoneshe hawa wanachama wajue huyu mtu anaumia kiasi gani - hakai chini. Mara kashuka kwenye kochi, mara kakaa hivi...mara kakaa hivi.

Mke wake anamuuliza baba vipi, ‘achana na haya mambo ya mpira yatakuja kukuua.’ Huyo ni mtu anayewekeza fedha zake kwenye kusapoti timu. Anawekeza nguvu zake kwenye kuisapoti timu. Ana mapenzi na timu...hali hiyo ndiyo inamkuta.

Sasa kuna mtu yeye kala zake mihogo huko, ‘sisi timu inatuuma zaidi. Nyie viongozi nyie, sisi ndiyo tunaumia”

Mhandisi Hersi aliitoa kauli hii jijini Mwanza, Oktoba 28 mwaka huu katika Ukumbi wa Bwalo la Jeshi alipokuwa akiongea na viongozi wa matawi ya wanachama na mashabiki wa klabu hiyo kuelekea mchezo wao wa Ligi Kuu dhidi ya Geita Gold.

Kauli hii ilipokelewa vizuri sana tena kwa makofi bwaloni pale lakini baada ya sare ya 0-0 nyumbani dhidi ya Club Africain, ndipo mapokeo yakabadilika.

Wale mashabiki wala mihogo ambao Hersi aliwalenga, wakafanya remontada ya hatari na kurudisha mashambulizi kwa Rais wao.

Mapovu yakawatoka na ndipo wapinzani wao wakaidaka na kuteleza nayo.

Kwa sasa habari ya mjini ni MIHOGO, sasa sijui ni mihogo ya Chanika au Jang’ombe?

KANDAMBILI

Mwaka 1975 Yanga ilikumbwa na mgogoro ambao kimsingi ulifukuta kuanzia 1968. Mgogoro huo ambao chanzo chake ni mtafaruku uliotokana na ujenzi wa ofisi za makao makuu za Jangwani na Uwanja wa Kaunda, ulisababisha kukosekana amani klabuni hadi ulipokuja mpasuko wa 1976 uliozaa klabu mpya ya Pan Africa.

Mwenyekiti wa Yanga, Mangara Tabu Mangara na kundi lake akiwemo aliyekuwa mfadhili wao, Shiraz Shariff, walifanyiwa mapinduzi Julai 1975 lakini serikali ikayapinga.

Siku moja timu ikiwa mazoezini Uwanja wa Kaunda, wanachama wakaja na kelele zao kushinikiza Mangara awaachie timu yao.

Kelele hizo zikawafikia wachezaji na Uncle J, Juma Pondamali alipozisikia, akawajibu kwa dharau kwamba, ‘hata nyie wavaa kandambili zenu mnaweza kusema kitu mbele ya wenye fedha?

Hapo ndipo jina la kandambili lilipoanza.

Wakati huo watu wenye fedha walikuwa wakivaa viatu virefu yaani ‘rise on’ lakini waswahili waliita raizono.

Kwa hiyo moja kwa moja wale wenye fedha wakawa wavaa raizoni na wale masikini wakwa wavaa kandambiliWavaa kandambili wakapambana hadi uchaguzi ukafanyika Desemba 28, 1975 na wavaa raizoni wakashindwa.

Wakatoka na kwenda kuanzisha timu yao waliyooita Pan Afrika.

YEBOYEBO

Mwaka 2004 kampuni moja ya vinywaji hapa nchini ilikuja na aina fulani ya uji ulioitwa Yeboyebo.

Mwaka huo kuna viatu fulani aina ya ‘sendoz’ iliibuka hapa mjini na kupendwa sana na ‘watoto wa mjini’.

Kwenye maonesho ya sabasaba, kampuni ile ya vinywaji ikaja na wazo la promosheni kwa ajili ya uji wao. Kwamba mtu ukinunua uji wa Yeboyebo, unapewa na zile aina ya sendoz...hapo ndipo sendoz zile zikaitwa yeboyebo na umaarufu wake ukazimika ghafla na kuwa viatu vya kishamba badala ya vya kijanja.

Asilimia kubwa ya viatu vile ilikuwa rangi ya njano na kijani, ambazo ni rangi rasmi za klabu ya Yanga.

Kwa kuwa Yanga ni kandambili na viatu vile vilikuwa jamii ya kandambili, basi jina la Yeboyebo likatoka kwenye vile viatu na kwenda Jangwani.

Kwa hiyo yeboyebo kimsingi ni mwendelezo wa Kandambili katika karne ya 21.

GONGOWAZI

Miaka ya zamani kabisa mpira ulichezwa bila jezi wala viatu hapa nchini.

Wachezaji walifunga bandeji miguuni ili kujikinga na ugumu wa ardhi na rafu za wapinzani uwanjani. Maisha yakaanza kubadilika na baadhi ya timu zikaanza kuvaa viatu na jezi, lakini Yanga ilichelewa kidogo. Safari moja shabiki mmoja wa klabu hiyo mwenye asili ya Asia alikwenda kutazama mechi, akashangazwa kuona wapinzani wao wamevaa jezi lakini wao wako migongo wazi.

Akaahidi kuwanunulia jezi akisema, ‘Hapana cheza tena gongo wazi’.

Hapo ndipo jina la Gongowazi lilipoanzia na kuendelea hadi leo.

UTOPOLO

Nenda kwenye kivinjari cha Google halafu andika Utopolo, litakuja jina la Yanga. Hili ni jina ambalo limejizolea sana umaarufu kwa miaka ya hivi karibuni.

Lilitokana na kauli ya shabiki wao mmoja aliyekerwa na matokeo na namna timu ilivyocheza kwenye moja ya mechi za Ligi Kuu.

Akihojia na moja ya vyombo vya habari hapa nchini, shabiki huyo akasema ‘Hii ni Yanga au Utopolo?’ Hapo ndipo jina la Utopolo lilipoibuka.

Lilipata zaidi umaarufu baada ya kuwa likitumiwa sana Haji Manara alipokuwa Msemaji wa Simba.

Wakati Yanga wakiwa kwenye harakati za kufanya mabadiliko ya kimfumo, walienda Hispania kutafuta ushauri wa kitaalamu.

Haji akawa anawatania kwa kusema wakirudi huko watabadili jina na kuwa Depotivo la Utopolo, akirejea majina ya timu za Hispania kama Depotivo la Coruna. Jina la Utopolo likawa maarufu zaidi na zaidi. Na sasa ni zamu ya wala mihogo.

Majina yote haya yametoka kwenye midomo yao wenyewe. Tusubiri mengine mengi yatakuja huko mbele

Ongezea lingine hapo chiniView attachment 2599272
Hee hawakuwa tishet enzi hizo?
 
Ni majina mangapi ya utani ya klabu ya Yanga umeshawahi kuyasikia maishani mwako?

Kama wanavyosema wahenga, ukiona nyani mzee ujue amekwepa mishale mingi. Basi kwa ukongwe wa Yanga ni lazima imekutana na majina mengi sana.

Hata jina la Yanga, limetokana na wao wenyewe na wengine kushindwa kutamka jina la Young Africans na hatimaye hadi leo kufahamika kwa jina hilo lenye umaarufu mkubwa. Lakini kitu ambacho unaweza kushindwa kuamini ni kwamba majina haya kwa asilimia kubwa wamejipa wenyewe.

Baada ya kukerwa na jambo fulani, mara nyingi huwa matokeo, mmoja wao huibuka na kuropoka neno ambalo huja kugeuka kuwa jina lao la utani ambalo wapinzani wao hulitumia kuwanyima raha.

Hivyo ndivyo majina kama Gongowazi, Kandambili, Yeboyebo, Utopolo hayo ni kwa uchache tu, yalivyoanza na sasa kuna jina jipya!

WALA MIHOGO
Bila shaka utakuwa umesikia siku mbili hizi mashabiki wa Yanga wakitaniwa wao ni wala mihogo. Kama hujasikia basi chukua hiyo, mashabiki wa Yanga kwa sasa wamepumzika kuitwa Utopolo, sasa ni Wala Mihogo.

Jina hilo limekuja kama mapokeo ya kauli ya Rais wa klabu hiyo, Mhandisi Hersi Said, alipokuwa akizungumza na viongozi wa matawi majuma mawili yaliyopita, alitumia kauli tata kuwalenga ‘mashabiki matokeo’ wa klabu hiyo ambao huwalaumu viongozi kila wakati timu yao isiposhinda.

“Achilia mbali mtu mwingine, Gharib (GSM) hawezi kwenda uwanjani, kwa presha aliyokuwa nayo. Anakaa pale, na ukimuona vile anavyokaa, natamani siku moja - Frank eh, naomba siku moja uichukue ile video, tuwaoneshe hawa wanachama wajue huyu mtu anaumia kiasi gani - hakai chini. Mara kashuka kwenye kochi, mara kakaa hivi...mara kakaa hivi.

Mke wake anamuuliza baba vipi, ‘achana na haya mambo ya mpira yatakuja kukuua.’ Huyo ni mtu anayewekeza fedha zake kwenye kusapoti timu. Anawekeza nguvu zake kwenye kuisapoti timu. Ana mapenzi na timu...hali hiyo ndiyo inamkuta.

Sasa kuna mtu yeye kala zake mihogo huko, ‘sisi timu inatuuma zaidi. Nyie viongozi nyie, sisi ndiyo tunaumia”

Mhandisi Hersi aliitoa kauli hii jijini Mwanza, Oktoba 28 mwaka huu katika Ukumbi wa Bwalo la Jeshi alipokuwa akiongea na viongozi wa matawi ya wanachama na mashabiki wa klabu hiyo kuelekea mchezo wao wa Ligi Kuu dhidi ya Geita Gold.

Kauli hii ilipokelewa vizuri sana tena kwa makofi bwaloni pale lakini baada ya sare ya 0-0 nyumbani dhidi ya Club Africain, ndipo mapokeo yakabadilika.

Wale mashabiki wala mihogo ambao Hersi aliwalenga, wakafanya remontada ya hatari na kurudisha mashambulizi kwa Rais wao. Mapovu yakawatoka na ndipo wapinzani wao wakaidaka na kuteleza nayo.

Kwa sasa habari ya mjini ni MIHOGO, sasa sijui ni mihogo ya Chanika au Jang’ombe?

KANDAMBILI
Mwaka 1975 Yanga ilikumbwa na mgogoro ambao kimsingi ulifukuta kuanzia 1968. Mgogoro huo ambao chanzo chake ni mtafaruku uliotokana na ujenzi wa ofisi za makao makuu za Jangwani na Uwanja wa Kaunda, ulisababisha kukosekana amani klabuni hadi ulipokuja mpasuko wa 1976 uliozaa klabu mpya ya Pan Africa.

Mwenyekiti wa Yanga, Mangara Tabu Mangara na kundi lake akiwemo aliyekuwa mfadhili wao, Shiraz Shariff, walifanyiwa mapinduzi Julai 1975 lakini serikali ikayapinga.

Siku moja timu ikiwa mazoezini Uwanja wa Kaunda, wanachama wakaja na kelele zao kushinikiza Mangara awaachie timu yao.

Kelele hizo zikawafikia wachezaji na Uncle J, Juma Pondamali alipozisikia, akawajibu kwa dharau kwamba, ‘hata nyie wavaa kandambili zenu mnaweza kusema kitu mbele ya wenye fedha?

Hapo ndipo jina la kandambili lilipoanza.

Wakati huo watu wenye fedha walikuwa wakivaa viatu virefu yaani ‘rise on’ lakini waswahili waliita raizono.

Kwa hiyo moja kwa moja wale wenye fedha wakawa wavaa raizoni na wale masikini wakwa wavaa kandambiliWavaa kandambili wakapambana hadi uchaguzi ukafanyika Desemba 28, 1975 na wavaa raizoni wakashindwa.

Wakatoka na kwenda kuanzisha timu yao waliyooita Pan Afrika.

YEBOYEBO
Mwaka 2004 kampuni moja ya vinywaji hapa nchini ilikuja na aina fulani ya uji ulioitwa Yeboyebo. Mwaka huo kuna viatu fulani aina ya ‘sendoz’ iliibuka hapa mjini na kupendwa sana na ‘watoto wa mjini’.

Kwenye maonesho ya sabasaba, kampuni ile ya vinywaji ikaja na wazo la promosheni kwa ajili ya uji wao. Kwamba mtu ukinunua uji wa Yeboyebo, unapewa na zile aina ya sendoz...hapo ndipo sendoz zile zikaitwa yeboyebo na umaarufu wake ukazimika ghafla na kuwa viatu vya kishamba badala ya vya kijanja.

Asilimia kubwa ya viatu vile ilikuwa rangi ya njano na kijani, ambazo ni rangi rasmi za klabu ya Yanga.

Kwa kuwa Yanga ni kandambili na viatu vile vilikuwa jamii ya kandambili, basi jina la Yeboyebo likatoka kwenye vile viatu na kwenda Jangwani.

Kwa hiyo yeboyebo kimsingi ni mwendelezo wa Kandambili katika karne ya 21.

GONGOWAZI
Miaka ya zamani kabisa mpira ulichezwa bila jezi wala viatu hapa nchini.

Wachezaji walifunga bandeji miguuni ili kujikinga na ugumu wa ardhi na rafu za wapinzani uwanjani. Maisha yakaanza kubadilika na baadhi ya timu zikaanza kuvaa viatu na jezi, lakini Yanga ilichelewa kidogo. Safari moja shabiki mmoja wa klabu hiyo mwenye asili ya Asia alikwenda kutazama mechi, akashangazwa kuona wapinzani wao wamevaa jezi lakini wao wako migongo wazi.

Akaahidi kuwanunulia jezi akisema, ‘Hapana cheza tena gongo wazi’.

Hapo ndipo jina la Gongowazi lilipoanzia na kuendelea hadi leo.

UTOPOLO
Nenda kwenye kivinjari cha Google halafu andika Utopolo, litakuja jina la Yanga. Hili ni jina ambalo limejizolea sana umaarufu kwa miaka ya hivi karibuni.

Lilitokana na kauli ya shabiki wao mmoja aliyekerwa na matokeo na namna timu ilivyocheza kwenye moja ya mechi za Ligi Kuu.

Akihojia na moja ya vyombo vya habari hapa nchini, shabiki huyo akasema ‘Hii ni Yanga au Utopolo?’ Hapo ndipo jina la Utopolo lilipoibuka.

Lilipata zaidi umaarufu baada ya kuwa likitumiwa sana Haji Manara alipokuwa Msemaji wa Simba.

Wakati Yanga wakiwa kwenye harakati za kufanya mabadiliko ya kimfumo, walienda Hispania kutafuta ushauri wa kitaalamu.

Haji akawa anawatania kwa kusema wakirudi huko watabadili jina na kuwa Depotivo la Utopolo, akirejea majina ya timu za Hispania kama Depotivo la Coruna. Jina la Utopolo likawa maarufu zaidi na zaidi. Na sasa ni zamu ya wala mihogo.

Majina yote haya yametoka kwenye midomo yao wenyewe. Tusubiri mengine mengi yatakuja huko mbele

Ongezea lingine hapo chini

"rise on" = raizono
"young" = yanga.
Gongowazi tabu kweli kweli. Vipi kuhusu nomino Chura aka Vyura
 
Hii ya vyura ni kutokana na eneo walilopo pale jangwani kuna asili ya mafuriko ukienda muda kama huu masika nadhani hukuti watu pale kutokana na maji kuzingira eneo lote lile,na ukipita mida ya jioni utasikia ni kelele za vyura tu krooooooo krooooooooowakaamua kuwaita vyura...
Ule ni mkondo wa maji kiujumla yanayoenda kumwaga baharini kule salender bridge
 
Mtasema mengi Sana kuhusu Yanga Ila mnaumia ndani kwa ndani Yanga nusu fainal hiyo.
Mkijicheki hamna uhakika lazima mlete Thread Kama hizi
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣

Ukireply comment hii wew ni sh..............
 
Lucky Eymel alisema mashabiki yanga yapo kama mambwa yanabweka wow wow na yanajazwa yanajazika na mataahira kama manara kama manyumbu
 
Back
Top Bottom