Yanga AKIFUNGWA na Simba tu KINANUKA......... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Yanga AKIFUNGWA na Simba tu KINANUKA.........

Discussion in 'Sports' started by Bwana Mapesa, Oct 1, 2012.

 1. Bwana Mapesa

  Bwana Mapesa JF-Expert Member

  #1
  Oct 1, 2012
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 1,925
  Likes Received: 660
  Trophy Points: 280
  Nawasalimu Wana JF!
  Kuna tetesi nimezipata kutoka kwa Wadau wakubwa wa Yanga ambao wanatofauti ya kimtazamo na Uongozi Mpya wa Yanga.Kumekuwa na Makundi ambayo chanzo chake ni Ma TYCOON walili wenye ugomvi wa mda mrefu ambao nao wameamua kuitumia Yanga kama sehemu ya Uwanja wa Mapambano yao.Filamu hii ilianza tokea kipindi cha Yanga Asili na Yanga Kampuni......
  "Reginald Mengi alikuwa ana heshima kubwa Yanga na akajitolea kusuluhisha mgogoro wa Yanga Asili na Yanga Kampuni.
  Awali, walimsikiliza na kwenda naye sawa, lakini alipotofautiana na wenye Yanga yao, yalimgeukia pale Star Light Cinema na hadi leo hajakanyaga tena kwenye shughuli ya Yanga."

  Reginald Mengi anayomilikivituo vya televisheni, redio na magazeti lukuki alishindwa kusuluhisha mgogorohuo wa Yanga licha ya kupania kwa dhati kuleta amani katika klabu hiyo.

  "Muafaka kati ya makundi hayo chini ya usuluhishi wa Manji ulifikiwa Agosti, mwaka 2006 na Mei 30, mwaka 2007, klabu hiyo ya Yanga ilifanya uchaguzi wake. Manji ametoa misaada mbalimbali kwa klabu hiyo kuanzia uongozi wa Imani Madega ambaye naye ni mwanasheria."

  kutokana na hali hiyo hapo utaona dhahiri wapi vita imeanzia....sasa tuendelee kipindi cha Uongozi wa Bwana Madega huyu na Manji walikuwa marafiki na hata akaingizwa madarakani na kuwa anafanya chochote ambacho bosi wake huyo anamuagiza.Lakini kipindi hiki bwana Manji alikuwa anamtumia mtu mmoja anaitwa Sabas ambaye ndiye alikuwa mwanasheria wake ni Sabas huyu ndiye aliyekuwa anapokea pesa kutoka kwa Manji kwenda Yanga via Madega.utata ulianza baada ya sabas kukimbia kwa Manji na kwenda kufanya kazi na Mengi.Hapo ndo kimbembe kimeanza,Manji akamtuhumu madega kuwa alikula pesa ya yanga wakati wa uongozi wake na Madega akajibu mapigo kwa kufungua kesi dhidi ya Manji na fidia ya bilioni 2....sasa utaona ili manji approve alichoongea mbele ya mahakama there are some people supposed to be incriminated njia rahisi ni Auditing kuanzia hapo atakuwa amemweza sabas na madega.Lakini pale kuna mchaga mmoja anaitwa Mosha huyu bwana uchaga umemponza na inaonekana dhahiri yupo kwenye kabi ya mzee RM.Hata siku ya uchaguzi wa Yanga yeye aliingia na Lambogrin na Manji aliingia na Range TDV8...ambapo Moshi alifanya hivyo ili nae kuonyesha jeuri ya pesa.

  MY TAKE:Sasa hapa kuna kundi la watu wanaompinga Manji ambao wanatafuta uchochoro wa kumchomolea nje ya Yanga na sababu pekee ni Yanga kupigwa simba then watu wakinukishe.si mnakumbuka kile kikundi kilichotokea kwenye vyombo vya habari wakati manji mfadhili na kusema hawamtaki analeta migogoro ndani ya timu yao?sasa vikundi kama vile vimeongezeka na wanajaribu kuangalia kila move ya uongozi mpya ili wapate upenyo wa kuendeleza vita yao ndani ya uwanja mpya(Yanga).KAMA WEWE YANGA INAKUHUSU ...TAFAKARI...CHUKUA HATUA
  KWA NILIOWAUDHI KWA UKWELI MNISAMEHE!
   
 2. WABHEJASANA

  WABHEJASANA JF-Expert Member

  #2
  Oct 1, 2012
  Joined: Jun 22, 2011
  Messages: 4,225
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  DUA la kuku hilo kaka halimpati mwewe!!!!!!!chukua hatua mapema
   
 3. N

  Nyakipambo JF-Expert Member

  #3
  Oct 1, 2012
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 435
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Lazima mtu apigwe bakora wiki hii pale mtaa wa twiga na jangwani
   
 4. M

  MIRIJA IKATWE Senior Member

  #4
  Oct 1, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 136
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ugomvi wa panzi furaha ya kunguru, si wagombane kabisa tuwapige walau saba itakuwa poa
   
 5. T

  Tanzania1960 JF-Expert Member

  #5
  Oct 1, 2012
  Joined: Sep 6, 2012
  Messages: 204
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  WEWE OMBA DUA SAANA MANAAKE NYIE SIMBA MMEISHA JUA NANI ANAKUJA NYUMA YENU MJE MPAKATWE..... VITUS ....YANGA WAJITAHADHARI NA NA HAWA WACHOCHEZI ,LAKINI HAMTAFANIKISHA.:whoo:
   
 6. M

  MzeePunch JF-Expert Member

  #6
  Oct 1, 2012
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 1,412
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Nijuavyo Manji amejipanga vizuri na ametumia pesa nyingi sana kuihujumu Simba ili Yanga iweze kushinda mchezo wa Jumatano. Kiufundi, Simba ni wazuri zaidi kuliko Yanga, na katika hali ya kawaida ndio washindi wa mechi ya Jumatano. Lakini kuna taarifa za wachezaji wa Simba kupokea/kuahidiwa hongo kutoka kwa Manji ili waifungishe timu yao. Hujuma nyingine baadhi yenu mnazijua (ref. Okwi, Maftah red cards). Lakini viongozi wa Simba wameshitukia dili na tayari wamewapiga mkwara wachezaji wao na hata kuwalisha yamini ili wadhurike iwapo watakuwa wamelamba pesa za Manji. Timu ya Simba katika mchezo wa Jumatano itakuwa na mabadiliko makubwa na itapangwa kwa uangalifu mkubwa sana, kuepusha uwezekano wa wachezaji wa kutumainiwa kuhujumu sababu ya pesa. Kama mjuavyo, Manji ana pesa nyingi anazozipata kwa njia za kifisadi (tena ufisadi wa kutisha!) hivyo anaweza kutoa kiasi chochote bila kuona uchungu ili mradi adhihirishe kuwa yeye ndiye anayefaa zaidi kuwa pale Yanga. Simba wanapaswa kuchukua tahadhari kubwa sana na baadhi ya wachezaji wao, na hata waamuzi wa mchezo wa Jumatano ambao kwa vyovyote watataka kuvuna mahela kutoka kwa Manji.
   
 7. Anselm

  Anselm JF-Expert Member

  #7
  Oct 2, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 1,705
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Ha ha ha ha ha I can see Wapenzi na Mashabiki wa Simba mmeanza kuandaa sababu lukuki mtakazozitoa baada ya mtanange wa kesho,tumewazoea ni kawaida yenu lkn mimi natakakumwambia mleta uzi...kihalisia Yanga hakuna Watindiga wa kuchotwa na fitina za kitoto kama hizo ukiona kuna mtu ana element za kitindiga Yanga basi ujue huyo ni mamluki yaani ni wa upande wa 2 anayetaka kuleta chokochoko upande wetu,pale Yanga watu wanatumia vichwa timamu kufikiri na kufanya maamuzi katu maamuzi ya kijinga hayawezi kuchukuliwa na watu makini wa Yanga,hilo ni Mosi....Pili.....kama ndo wameamua kutega sababu hiyo wame'fail ksbb kesho hatufungwi ninachowasihi nyie endeleeni kuandaa sababu kama hivyo mmeshaanza mara Okwi, mara Maftah mara hela za Manji mbona hamzisemehi hela chafu za Mhaini Hans Pop?
   
 8. Kennedy

  Kennedy JF-Expert Member

  #8
  Oct 2, 2012
  Joined: Dec 28, 2011
  Messages: 11,329
  Likes Received: 2,980
  Trophy Points: 280
  Mbona hilo linajulikana vzr hata ukimuuliza mtoto mdogo atakupa majibu kuwa kama YANGA akifungwa na mtani wake lazima KITANUKA.
   
 9. Donnie Charlie

  Donnie Charlie JF-Expert Member

  #9
  Oct 2, 2012
  Joined: Sep 16, 2009
  Messages: 6,577
  Likes Received: 846
  Trophy Points: 280
  Tunakuarifu Shughuli Ya Binti Mrembo Yanga Anayetarajia Kufunga Ndoa Na Kijana Mtanashati Simba Sports Club (wekundu Wa Msimbazi) Ambayo Itafanyika Tar.3.10. 2012. Mshenga ni Mtibwa Ametumwa Kupeleka gunia 3 Za mpunga kama zawad ya Kufungia Uchumba. Ukiwa Ndugu Wa Karibu Na Bwana Harusi (SIMBA) Unaombwa Kufika Uwanja wa Taifa. Atakapolishwa Keki Bibi Harusi mtarajiwa(YANGA). Kufika Kwako Ndio Ukamilisho Wa Shughuli Hii muhimu.
   
 10. T

  Tanzania1960 JF-Expert Member

  #10
  Oct 2, 2012
  Joined: Sep 6, 2012
  Messages: 204
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  wewe sijui ni nani ?lakini unachoongea unakifahamu ?bora uwe mpenzi wa mpira acha kujiingiza kwenye siasa ,wewe una uhakika gani hela za manji ni chafu? May be we huna mbele wala nyuma eti fedha chafu,kwa hiyo serekali ya tanzania ni vipofu wasimjue mtu ?nenda zako huko mbele ongea maana sio ujinga ujinga hunaaa loloteee labda unataka kudandia tuuu.
   
 11. B

  Baba Kiki JF-Expert Member

  #11
  Oct 2, 2012
  Joined: May 31, 2012
  Messages: 1,366
  Likes Received: 488
  Trophy Points: 180
  Kwa utafiti wangu nimegundua mashabiki wa Simba hawaiogopi Yanga ndani ya uwanja, ila nje ya uwanja, na wale wengi wa Yanga wanasema washamaliza kazi nje ya uwanja na kushinda ni lazima. Sijui hii maana yake nini.
   
 12. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #12
  Oct 2, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Longo longo nyingi kesho vijana wa jangwani watawaonyesha vijana wa msimbazi kilichomtoa nyoka pangoni washachonga sana waarabu wale
   
 13. T

  Tanzania1960 JF-Expert Member

  #13
  Oct 3, 2012
  Joined: Sep 6, 2012
  Messages: 204
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  KESHO ILE RAMBI RAMBI YA YULE MCHEZAJI WENU NANI YULE ? YULE MLIOKULA PESA ZAKE HALAFU ILE TIMU YENU ILEE NDOGO ILEE AMBAYO MLIWAAHIDI KAMILIONI MOJA KILA MCHEZAJI KITAWALIZA ,NA MKITAKA KUSHINDA BASI HII LEO USIKU MALIZENI MADENI YAO.:juggle:
   
 14. M

  MzeePunch JF-Expert Member

  #14
  Oct 3, 2012
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 1,412
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135

  Unauliza mimi ni nani? Angalia vizuri, naitwa MZEE PUNCH. Labda wewe ni mgeni hapa mjini (Bongo)), hujui lolote kuhusu suala zima la UFISADI. Kama sio mgeni, basi ni miongoni mwa Watanzania wengi waliozibwa usoni na blanketi jeusi hata wasijue jinsi raslimali zao zinavyoporwa na wajanja wachache, akiwemo Manji. Yeye huwaita Watanzania NYANI WEUSI, na hutamba kwamba atawaibia mpaka wakome! Hulijui hilo kwa sababu wewe bila shaka ni shabiki tu wa Yebo Yebo kutoka maeneo ya Tandika unayefurahia kulipiwa kiingilio na huyu fisadi kwenda uwanjani. KALAGA BHAO.
   
 15. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #15
  Oct 3, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,435
  Likes Received: 19,789
  Trophy Points: 280
  wakinukishe tu toka sasa hivi manake kuchezea kichapo haipukiki Yanga watakuwa wateja wetu kwa muda mrefu sana
   
 16. lutayega

  lutayega JF-Expert Member

  #16
  Oct 3, 2012
  Joined: Feb 29, 2012
  Messages: 1,215
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Km watamalizana simba haituhusu, na km mnataka muonewe huruma ili msifungwe pia haituhusu. Mi nachojua leo tukiwahurumi basi itakuwa ni simba3 yanga 1, au mjiandae kwa 6 bila ili mkamalizane vizuri
   
 17. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #17
  Oct 3, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,005
  Likes Received: 739
  Trophy Points: 280
  Tutakamata mnyama tu.
   
 18. Makoye Matale

  Makoye Matale JF-Expert Member

  #18
  Oct 3, 2012
  Joined: May 2, 2011
  Messages: 6,480
  Likes Received: 450
  Trophy Points: 180
  We mbeya tu acha mambo ya Yanga wayashughulikie wenyewe.

  Hata kikinuka shida iko wapi, wewe utapata hasara au faida gani? Manji kachaguliwa kwa mujibu wa katiba na kama amekosa sifa za kuwa kiongozi katiba hiyo hiyo itatumika kumwondoa. Si unakumbuka Benjamin Netanyahu alikuwa waziri mkuu wa Israel miaka ya nyuma kikanuka kwa sababu fulani fulani, akaenda nje akajipanga na kurejea tena kwenye nafasi yake. Sasa wewe unaona kuna lipi la ajabu hata kama kikinuka?

  Bahati mbaya Simba wengi wanaamini kuwa uwepo wa Manji pale Yanga ni tishio kubwa kwao, hivyo wekundu hawa sasa nao wameamua kuungana na wasaliti ndani ya Yanga ili Manji aondoke.

  Kwa jina la Allah (Mwenyezi Mungu aishie milele), washindwe kabisa, Yanga isonge mbele!
   
 19. T

  Tanzania1960 JF-Expert Member

  #19
  Oct 3, 2012
  Joined: Sep 6, 2012
  Messages: 204
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  aisee wengine sisi tukipata buku tu tunakimbilia kwenye inteneti kafe kuandika vitu vya uchochezi kwa sababu yetu ya ushabiki ,lakini mwisho wa siku natafuta lifti ya kwenda home .. kule kwa mtoni..:embarassed2:
   
Loading...