Yanga 28, simba 14 duru la kwanza | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Yanga 28, simba 14 duru la kwanza

Discussion in 'Sports' started by MaxShimba, Nov 1, 2008.

 1. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #1
  Nov 1, 2008
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160


  Hesabu duru la kwanza zafungwa:Yanga 28, Simba 14

  *Wanijeria Simba 'wageuka' mabondia, wajaribu kwa kocha

  Na Sophia Ashery

  MIAMBA ya soka nchini Simba na Yanga jana ilimaliza ngwe ya kwanza ya Ligi Kuu Tanzania Bara kwa suluhu, ambapo Yanga iliumana na Polisi Moro Uwanja wa Jamhuri Morogoro, huku Simba ikiumana na Moro United Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

  Kutokana na matokeo hayo Yanga imemaliza nduru la kwanza la ligi hiyo ikiwa na pointi 28 baada ya kushinda michezo tisa, suluhu mmoja na kufungwa mmoja, huku Simba ikimaliza kwa pointi 14 baada ya kushinda mechi nne, kufungwa tano na sare mbili.

  Katika mechi ya Simba jana, timu hiyo ilishindwa angalau kuwapa faraja mashabiki wake, baada ya Jumapili kufungwa bao 1-0 na Yanga, ambapo jana ilipata nafasi kadhaa za kufunga, ila umaliziaji haukuwa mzuri.

  Kama washambuliaji Mussa Hassan 'Mgosi', Emmanuel Gabriel, Ulimboka Mwakingwe wangetulia, huenda Simba ingeibuka na ushindi.

  Lakini Moro United nayo ilipoteza nafasi kupitia kwa Amri Kiemba, Thomas Maurice na Patrick Mangunguru.

  Katika hali isiyo ya kawaida, baada ya kumalizika mchezo huo, mchezaji Mnijeria Orji Obina , alimpiga kiatu Kocha Mkuu wa Simba, Mbulgaria Krasmir Bezinsk, huku akimtuhumu kwa kitendo cha kutowapanga katika mechi yeye na Mnijeria mwenzake Emeeh Izechukwu, ambaye pia alikuwa akimtolea maneno makali kocha huyo.

  Hali hiyo ilizua tafrani kwa mashabiki kutaka kuwapiga wachezaji hao, hali iliyofanya askari waliokuwa wakilinda usalama kuwatawanya mashabiki waliokuwa na hasira na kisha kuwaingiza wachezaji hao kwenye vyumba vya kubadilishia nguo.

  Kutoka Morogoro, Nickson Mkilanya anaripoti kuwa mashabiki waliohudhuria mchezo huo walishuhudia washambuliaji wa timu zote mbili wakishindwa kutumbukiza mipira wavuni.

  Yanga ilipata nafasi nyingi, lakini Athumani Idd, Mrisho Ngassa na Maurice Sunguti, lakini walishikwa na kigugumizi cha miguu.

  Nao washambuliaji wa Polisi Moro, Fredy Hagai, Ally Moshi, Imani Mapunda na Nsa Job walipoteza nafasi nyingi za kufunga.

  Kutoka Mbeya, Rashid Mkwinda anaripoti kuwa Prisons jana iliifunga Toto African mabao 2-0 Uwanja wa Sokoine mjini humo, huku mabao ya Prisons yakifungwa na Henry Mwalugala dakika 15 na Oswald Morris dakika ya 29.

  Tuma kwa Rafiki Nakala inayochapika   
 2. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #2
  Jan 21, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Masatu, Invisible na wengine wapenda soka la bongo, vipi matokeo Yanga (Taifa Stars) na Prison kwenye League ya TFF nadhani wamecheza leo huko jamhuri ya watu wa Mbeya...tuhabarisheni tafadhali...
   
 3. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #3
  Jan 21, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Guess what
   
 4. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #4
  Jan 21, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Wafunga buti wamepigwa ama mzee unataka semaje?
   
 5. A

  Amwanga JF-Expert Member

  #5
  Jan 21, 2009
  Joined: Jan 11, 2009
  Messages: 294
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Vipi matokeo jamani Yeboyebo wametupa kandambili au wamemchapa nazo afende Mbeya? Usiku mwema wanachama.
   
 6. A

  Amwanga JF-Expert Member

  #6
  Jan 21, 2009
  Joined: Jan 11, 2009
  Messages: 294
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Yeboyebo ya wafunga Wavaa buti 1-0
   
 7. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #7
  Jan 21, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Thanks mkuu....mwendo mdundo
   
 8. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #8
  Jan 22, 2009
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Mwaka wenu Kagoda FC. Hivi Manji bado yuko ICU?
   
Loading...