Yanayosemwa huko Algeria kuhusu tuhuma za kufix mechi ya Tanzania vs Algeria

Lakini si tumepita? Au wanataka tukapigiane penati?
 
Kumiliki mpira sio kupata matokeo....Kama unabisha nenda kafuatilie takwimu za mchezo Kati ya Spain na Russia wa kombe la dunia ambapo Spaini alitolewa kwa penalties.......
 
Kwa wote mnaoongelea kuhusu takwimu za umiliki mpira, hilo nililiongeza mimi katika mjadala huu kuonyesha hata hilo halikuwaridhisha na kuonyesha jinsi wenzetu wanavyoangalia mpira tofauti na sisi. Sijaona wala kusikia wao wakitumia kigezo hicho kusema kulikuwa na upangaji matokeo.

Nilichofanya ni kuweka kila angle niliyopata na iliyozungumzwa kabla na baada ya mchezo.
 
Mechi ilikuwa sahihi kwa hayo matokeo mana Algeria hakuna walichokuwa wanatafuta katika mechi hii walishafuzu Ina mana na hao waganda tuseme walifix na Niger wakapewa zile goli mana Niger nayo ilikuwa ishajikatia tamaa
 
Aisee unaweza Kuta Kuna mtu anakuita BABA
 
Uganda wangetaka kufuzu wangeshinda mechi zao mapema kama Algeria,mambo ya kusubiri mechi ya mwisho ndio madhara yake hayo
 
Macho anajaribu kujificha kwenye kivuli cha Tanzania kwa matukio yake mwenyewe. Kwa kumbukumbu ilisemekana kocha wa Niger alitamka kuwa atahakikisha anafungwa na Uganda ili kuinyima Tanzania nafasi ya kufuzu Afcon akiwa na imani Algeria itaifunga taifa Stars.

Matokeo yamekuwa tofauti wanataka kuleta ujinga wa kuona hatukustahili kufuzu.
 
Ukweli usemwe Tz haikuwa na uwezo wakupata sare kwenye ardhi ya mwarabu..
. Kilichotokea ni kubebwa na mwarabu kutokuihitaji mechi.
 
Algeria lost at home 1-2 when hosted Cameroon towards Fifa 2022 world cup qualifier..wakati kule ugenini Cameroon walishinda 0-1.(first leg)

Kocha alikuwa huyuhuyu.
Kwny game ile host walitawala sehemu kubwa ya mechi.sasa kwann madai ya kupanga matokeo hayakuibuka tena kwny serious match kama like.

Tanzania haijaanza kutoa sare na Algeria ugenn Mara ya kwanza.

Mwaka 2011 Algeria na Tanzania walitoa sare 1-1 ktk mechi iliyochezwa kwny mji wa Blida hukohuko Algeria.

Mazingira ya sare ya 2011 hayatofautiani na ya juzi..possession kwa Algeria ilikuwa juu mno..

Nakumbuka ni shaaban kado alikuwa nyota wa mchezo kwa upande waTanzania.
 
Yaliopita si ndwele, tugange yaliopo na yajayo.
Ni fursa kwa taifa stars na Tanzania kuonekana
 
Ukweli kuwa mpira wa Tanzania umekua hautakiwi duniani, nchi nyingi bado zinaiona Taifa Stars ni ndondo club wakati sio kweli for now! Hivi Ibra Baka unampitaje Kwa mfano hata aje Ronaldo hafungi goli! Timu yetu kwasasa ina uwezo wa kupaki bus haswa na wamethibitisha Hilo dhidi ya Algeria!

Hata waseme nini Ukweli mpira wetu uko next level , wachezaji wanaweza na hawaogopi timu yoyote hata ugenini wanapiga boli na huko Afcon twende na wembe ni ule ule tukicheza na timu kali tunapaki bus na kushambulia kwa kushtukiza na tukicheza timu dhaifu tunafunguka na kushambulia kama nyuki mwanzo mwisho!

Waalgeria wote walikuja uwanjani na matokeo yao mfukoni na hasa kwa vile walitufunga nyumbani 2-0 wakajua kwao Algeria Stars tutaoga 8-0!

Sisi bongo ni bora kidogo kisoka kwa sasa na tulistahili kufuzu Afcon hasa baada ya Msuva kuifunga Uganda kwao ilitakiwa Ile mechi ya marudiano kwa Mkapa tumalize kazi ila ni ajabu wachezaji wetu wakaipuuza mechi muhimu tukakosa magoli mia kizembe sana Uganda wakatuadhibu nyumbani na kujisifu sana kulipa kisasi.

Tukutane Afcon , Taifa Stars mbele kwa mbele!
 
Porojo tu hizo, tuwape pongezi taifa stars kwa ujumla wamejitahidi sana kutoruhusu kufungwa, na kuwapa pressure timu pinzani kutoka mchezoni.

Swala la kumiliki mpira na usipate matokeo ni swala la kawaida tu mbona.
Labda hawaujui mchezo wa mpira mkuu, unaikumbuka inter ya Mourinho? Au the special one mwenyewe team zote alizofundisha na mifumo yake, anashinda sana game za hivi, possession zako ushindi wangu,

Micho aache kulia kulia. Ishaenda hiyo
 
Porojo tu hizo, tuwape pongezi taifa stars kwa ujumla wamejitahidi sana kutoruhusu kufungwa, na kuwapa pressure timu pinzani kutoka mchezoni.

Swala la kumiliki mpira na usipate matokeo ni swala la kawaida tu mbona.
Kuna mechi ya ulaya ilichezwa muda uleule ambao stars ilikuwa inakipiga na Algeria.

Nimesimuliwa kuwa timu iliyoshinda ilikuwa ni yenye low ball possession.

Kuwa na high ball possession si kigezo wala tiketi ya ulazima wa kushinda mechi.

Hata ngumi, mpiganaji anaweza akamiliki game muda mrefu halafu mpinzani akapiga moja tu ya knockout akawa mshindi.

Kunya anye kuku, akinya bata anaharisha. Imekula kwao.

Sent from my Infinix X688B using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…