Mathias Byabato
JF-Expert Member
- Nov 24, 2010
- 1,033
- 723
Wanabodi salaam.
Nipo katika kikosi cha operation hii hivyo nitawajuza yanayojiri kwa maelezo,picha na video kadri operation inavyokwenda...
Serikali ya Mkoa wa Kagera kupitia vyombo mbalimbali vya ulinzi na usalama imeanza operation kabambe ya kuondoa mifugo yote na shughuli nyingine zinazofanywa na baadhi ya wananchi katika misitu na mapori ya Hifadhi ya Taifa yaliyoko katika wilaya kadhaa za mkoa huo.
Wafugaji wanaondolewa baada ya kupewa notisi ya kuondoa mifugo yao kwa hiari ambapo baadhi wametekeleza agizo hilo na wengine kukaidi.
Kwa siku ya kwanza leo ng'ombe zaidi ya 1200 zimekamatwa ...
Updates.
UPDATES APRIL 2,2017

Updates april 3,2017:
Bodi ya mamlaka ya wanayamapori Tanzania (TAWA) imetoa ndege 2 zisotumia rubani (drone) ili zitumike katika kusaka ng'ombe porini hasa maeneo yasiyofikaka kwa urahisi.Pia TAWA imetoa simu za upepo 20 kwa ajili hiyo.Wataalam 3 wa kuedesha ndee hizo tayari wametua biharamulo. vifaa hivyo vina thamani ya dolla elfu 40.
Picha zitawekwa hapa baadaye
Updates april 3,2017
Wafugaji na wachungaji wa Ng'ombe wapatao 19 wamefikishwa katika mahakama ya wilaya ya biharamulo hivi punde kwa tuhuma za kulishia mifugo katika misitu na ifadhi za taifa.
Mengine yatakayojiri kuhusu kesi hii na picha baadaye