Yanayojiri bungeni: Tarehe 20 Machi, 2014

Makangarawe

Senior Member
Joined
Nov 19, 2013
Posts
101
Reaction score
24
Bunge maalum la Katiba leo limepata mgeni kutoka Kenya mh. Amos Wako ambaye alikuwa mwanasheria wa Kenya na alishiriki katika mchakato wa kuandaa katiba.

Lengo la ujio wake ni kutoa fursa kwa wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba kujifunza jambo alilolifanya akiwa Mwanasheria wa Kenya aliyeshiriki Mchakato wa Kupata Rasimu ya Katiba ya Nchi hiyo hadi kupatikana kwa Katiba yake.

=== Updates ====

Kikwazo cha lugha aliyotumia Mh. Amos Wako


===

====
Rev. Mtikila naye anena,
 
^^
Anasema "You cannot need a new constitution, if you don't have a constitution crisis"
^^
 
Sitta kaona majanga wajumbe hawaelewi kiingereza vizuri, lolo, Sitta kamwambia jamaa atafsiri..
 
Wakati bwana Okao kutoka Kenya akiendelea kuelezea uzoefu wake kuhusu katiba ya Kenya na kutaka watanzania wajifunze kupitia Kenya, mtaalam huyu amekuwa akitoa maelezo hayo kwa njia ya kimombo na baadae kutafsiriwa, baadhi ya wajumbe wamemuomba M/Kiti ili mtaalamu huyo endelee tu kwa lugha ya kimombo kwa vile wengi wanafahamu. wakati Mwenyekiti akihoji kuwa endelee kwa lugha ya kimombo Mh Seif Ali Iddi amepeleka kichwa chake kushoto na kulia akiungana na baadhi ya wajumbe kutaka iendelee kutafsiriwa.,
 
Fafanua basi mkuu na uandike habari iliyojitosheleza.
 
hii kitu wamechemsha sana huyu Amos wenu anaongea kingereza tupu.eti amesema kiswahili kwao ni kigumu. sasa wamekuja na mkalimani hapa akiongea paragraph mbili anastop mkalimani anaelezea. baadae sita akaona ni kupoteza muda akamwambia aongee tu moja kwa moja kwani watanzania wengi wanajua kingereza. baada ya kuongea muda mrefu Sita anamkatisha tena anasema amepata msg kutoka kwa watu wengi eti lazima mkalimani atafsiri,lakini kwa sasa anatakiwa kutafsiri eneo kubwa yaani Wako aongee muda mrefuhalafu ndio atafsiri
 
katika kumchagua huyu msemaji kutoka Kenya kutokujua tu kiswahili ilikuwa inam-disqualify.
 
Sasa mbona hawakumwambia atumie kiswahili wakakurupuka na kiingereza lol, tz tunakurupuka jamani
 
Swala la shule za kina Kayumba/kata inabidi ubora wake usiisitizwe kwenye hii katiba. La sivyo hata wakalimani tutashindwa kuwazalisha.
 
Kwani lugha yetu ya taifa ni Kifaransa au Kiingereza?
Wajumbe wengi wa CCM ndio mbumbumbu, wanatuaibisha, Afadhali wamwachie Amos wako ashushe material moja kwa moja watatafasiri baadaye. Hawa wanatuaibisha sana maana Elimu imeshushwa na utawala wa CCM sasa wanamptotezea muda Mh. Wako na mpangilo wa mawazo yake. Utasikia magazeti ya Kenya watakavyotuchamba.
 
Yaani bunge letu lingekuwa linaendeshwa kwa Kiingereza kama Kenya ,mijadala ingekuwa inachukua muda mfupi sana,mambo ya ''Muongozo wa spika n.k ''yangepungua ama kuisha kabisa,wachangiajia wangekuwa wachache sana na utoro Bungeni ungeongezeka.
 
Sasa mbona hawakumwambia atumie kiswahili wakakurupuka na kiingereza lol, tz tunakurupuka jamani


Tumia akili ya kawaida tu! Kupitia almashauri ya kichwa chako, hakuna aliye kurupuka mgeni hakuweza kutumia lugha yetu kutoa mtililiko sahihi wa mawazo yake, hivyo utaratibu unaotumika ni sahihi
 
Kwani wakenya walijifunza kwa nani? Mi naona ilikuwa bora asiitwe huyo jamaa badala yake tungeangalia tu kwa uhalisia mahitaji na maoni ya watz yanataka nn na kuyafanyia kazi. Usije kushangaa huyo jamaa kulipa si chini ya tsh. 50,000,000 kwa hayo madudu tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…