Yanayojiri Bungeni: Mbunge Catherine Ruge(CHADEMA) aapishwa, Wabunge watoa posho zao kama rambirambi

Troll JF

JF-Expert Member
Feb 6, 2015
7,804
12,233
Leo Mbunge wa Viti Maalum Mheshimiwa Catherine Ruge ameapishwa Katika Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Bunge limeazimia kutoa posho ya wabunge kwa siku ya leo kama rambirambi kwa msiba wa Wanafunzi waliofariki kwenye ajali Arusha.
 
Wabunge wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo wakiwa bungeni wamekubaliana kwa kauli moja kuwa posho za kila mbunge kwa siku ya leo zipelekwe kwa wazazi wa wanafunzi waliofariki kwa ajali ya basi la shule ya awali na msingi ya Lucky Vincent.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan anaongoza waombolezaji mbalimbali kuaga miili 35 ya marehemu katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

Mbali na Makamu wa Rais pia viongozi mbalimbali wa Serikali wamewasili katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid kuaga miili ya wanafunzi waliofariki kwa ajali Arusha.
 
Nimemuona!Na suit yake ya blue.Kuachia mambo yoooote,kwa jicho la kibinadamu tu...Mh.Mbunge ana "Neema sana za Allah"

Kajaaliwa sana kwa kweli...Mtanisamehe!!!
Huhitaji kuomba msamaha eti kwa nia ya kuzisifia neema za muumbaji. Uzuri wa asili kama mtu anao basi kumpa sifa zake ni wajibu. Hivyo hujafanya kosa lolote lile lenye kustahili kuomba msamaha.
 
Halafu kapewa kuuliza swali, Catherine Ruge akachemka. Spika akacheka, akasema "mwanzo mgumu".
 
Hivi ina maana kwa siku wanapiga laki 3! Aisee uchaguzi ujao mbunge wangu 'asiponyoosha mkono' hapati kitu! Ebo! sasa mipesa yote hii ale menyewe halafu kura tumpe hivi hivi? haiwezekani.
 
Yaani majonzi yote haya wameendelea na Vikao vya Bunge Leo!!!!! Au huu ni Msiba wa ARUSHA?
 
Back
Top Bottom