Yanayojiri Bungeni Dodoma: Jumatatu, Februari 02

Yanayojiri Bungeni Dodoma: Jumatatu, Februari 02

Magazetini

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2014
Posts
593
Reaction score
1,713

Taarifa ya mwaka kuhusu kamati ya UKIMWI imewasilishwa bungeni

Spika amemtangaza Sitta kukaimu uongozi shughuli bungeni kwani muhusika yuko safari.

Chibulunje: Ibara ya CCM inaitaka kutambua mkoa wa Dodoma kuwa makao makuu ya nchi, kitu gani kinashindikana.
Jibu: Kunahitajika maoni na maamuzu ya baraza la mawaziri ili muswada uje bungeni, Serikali imeshatoa agizo la kusimamisha ujenzi wa majengo mapya Dar es Salaam.

Chibulunje: Mchakato serikali ulioeleza si sababu za msingi kuchelewesha mchakato kwa miaka mitano, Je! Serikali haioni umuhimu wa kuharakisha mchakato kabla ya uchaguzi2015? Wizara bado zinajenga Dar es Salaam.
Jibu: Bunge kuwa Dodoma ni matokeo ya mchakato na azma ya serikali. Manispaa ya Dodoma tayari ina watu laki tano, tukihamisha zidisha mara kumi, sisi tunaenda kwa hatua kwa kuweka miondombinu ambayo itabeba watu watakaohamia. Kuhusu ujenzi DSM, naomba ushahidi na majengo hayo, isije ikawa mtu anajenga kareserch unit ukasema anajenga wizara.

Badueli:
Kwanini serikali isiandae ratiba maalumu ya kuhama kwa hatua iletwe bungeni
Jibu: Ni jambo zuri na ushauri tumeupokea

Akunay:
Kwa kuwa tayari imeshachukua miaka 43 na bado hatujafanikiwa, serikali haoni ni muda sasa wa kureview
Jibu: Siwezi kusema hapa kwa niaba ya serikali eti tumebadilisha, kama kuna haja tutakaa hapa. Kulikua kuna sababu ya kuhamisha makao makuu Dodoma, watu watatushangaa tukibadili msimamo wetu.

Faida Bakari: Je! Wafanyabiashara walemvu wangapi waliopata mabilioni ya Kikwete
Jibu: Mpango wa kuwawezesha wananchi kiuchumi ulikuwa na mpango wa kuongeza ajira bila kujali maumbile yao, Namshukuru Mh Mbunge kwa swali zuri na tumepokea kama changamoto.

Bakari:
Kwa kua waziri amikiri mkopo hauna vigezo maalumu, imesababisha watu wengi wenye ulemavu kukosa. Nashukuru kuletwa vigezo, Je! Vitaanza lini?
Jibu: Kwanza hakuna vigezo kabisa, vigezo vilikuwa kwa mabenki. Tutarejea tena vigezo vile ili viwe rahisi kwa walengwa.

Msabaha: Mikopo ya JK na kwa ZNZ Karume, kuna watu hawakurejesha, serikali ilichukua hatua gani!
Jibu: ZNZ walipata milioni 600 na wenyewe waliongeza milioni 600. Mkaguzi wa ndani ameshafanya kazi kubaini nani amerejesha na wasiorejesha ili hatua zichukuliwa

Kulikoyela: Pensheni ni haki, serikali ina mpango wa kuwapatia pensheni wahadhiri wa vyuo waliokuwa kwenye mpango wa SSS waliostaafu kabla ya march 2011, pia wazee wote waliofikia umri wa kustaafu!
Jibu: Wahadhiri bado linashughulikiwa, serikali bado iko katika utafiti na majadiliano ili kulipa pensheni kwa wazee wote.

Kulikoyela: Maswali hayajajibiwa, swala la wahadhiri lipo sasa zaidi ya miaka 20, timeline ikoje? Tuliahidiwa na waziri mkuu mchakato wa kulipa wazee wote utaisha karibuni
Jibu: Mpango wa wahadhiri, katika kikao cha maraza la mawaziri, iliamuliwa kuwa wale waliokuwa wanafundisha mpaka 2011, wahamishiwe PPF na wataendelea kulipwa. Wa kabla walikataa PPF hivyo baraza la mawaziri lilikataa. Kuhusu la pili kuhusu wazee wote bado tunaendelea na utafiti. Vyanzo vya fedha havitoshi. Bado tunaangalia vyanzo vingine.

Swali; Kuna wafanyakazi zaidi ya 300 walioachishwa kazi kwenye mgodi wa Buliyngule baada ya kupata matatizo kazini, wanazungushwa sana, serikali inatoa kauli gani?
Jibu: Linashughulikiwa na wenzetu wa OSHA, ni swala lefu na siwezi kulingumzia hapa.

Swali: Mahakama zinatumia kiingereza, Je! Serikali haioni ni muda sasa kutumia Kiswahili
Jibu: Serikali inafahamu umuhimu, lugha za mahakama za mwanzo zitakuwa Kiswahili. Lugha inayotumika mahakama kuu ni Kiingereza ama Kiswahili ila kumbukumbu zitaandikwa kwa lugha ya Kiingereza.

Swali: Kutokana na usumbufu unaopatikana, serikali haioni ni muda sasa kulileta bungeni libadishwe
Jibu: Ni kweli kuna haja ya hukumu pia kuandikwa kwa Kiswahili, changamoto kubwa ni sheria zetu zipo kwenye lugha ya kiingereza. Tumeshaongea na TUKI pia baraza la Kiswahili. Pia miswada yote tunayoleta ina lugha Kiswahili pia.

Swali: Karagwe kuna adha kubwa ya maji, na mheshimiwa rais alipokuja alituahidi, lini ahadi itatekelezwa
Jibu: Ni kweli kuhusu ahadi, stadi imeshafanyika, utekelezaji tu unasuburiwa pindi fedha zitakapopatikana.

Swali: Kwanini inatokea kampuni zinasema gharama zake za simu ziko chini sana wakati TCRA inasema ni sawa!
Jibu: TCRA haipangi gharama za simu bali inapanga gharama za maunganisho kati ya mtandao mmoja na mwingine ambazo kwa sasa ni Tshs 30.58 kwa DK, gharama za ndani za mtandao mmoja zinapanga na mtandao husika hivyo ni wazi zitatofautiana, ikiwa mtandao unatoza zaidi ya bei elekezi ya TCRA hatua stahiki zitachukuliwa.

Silinde: Kwa kuwa kuna kitengo cha hujuma, kuanzia 2010-2013 kumekua na vocha bandia, kampuni ya Vodacom imeisimamisha shivacom kutengeneza vocha kwa kasha ya kutengeneza vocha feki zenye thamani ya $ nilioni 350. M-Pesa pekee zimepita trilioni 10, kwanini serikali isilete taarifa bungeni kujua mwenendo mzima wa fedha hizi?
Jibu: Swala la vocha bandia hatulijasikia, Mgogoro wa Shivacom na vodacom ni mgogoro wa kibiashara na hatujapokea malalamiko ya vocha feki. Kwenye mtambo mpya, kwenye hatua ijao tumeweka kifaa kuweza kubaini miamala iliyopita kupitia mitandao ya simu, hivyo serikali itajua kodi inayopaswa kulipwa.

Kitandula: Wizara ilinijibu kufikia Dec 31 itakua imeweka mnara wa simu kata ya Mwakijembe, kwa sababu za kiusalama, serikali haioni eneo hili linatakiwa kuwa na mawasiliano ya simu?
Jibu: Ni kweli tulimpa barua kumueleza kampuni ya Vodacom ni lini itaweka mnara, tuliandika kulingana na barua tuliopewa na Vodacom. Kulingana na matatizo kwenye makampuni yaliyopewa kazi ya kujenga minara, ilishindikana na tumeshaziagiza kampuni za simu zitafute wajengaji wengine.

Ayoub: TZ imekuwa na ushirikiano na uingereza kwa muda mrefu, kwanini ubalozi wa Uingereza umefungwa muda mrefu na kuleta adha!
Jibu: Ubalozi haujafungwa na wala hatutarajii, ni kweli huduma za viza zimeamishiwa kwa wakala, kutokana na maelezo ya ubalozi, pamoja na kuwa viza zinashughulikiwa, muda wa wastani ni siku 18 kabla ya safari. Tatizo litakuja endapo kuna safari ya Ghafla. Serikali inaendelea kufanya jitihada kupunguza adha ya kupata viza.

Nyongeza: Kwakua amekiri kuna uhusiano mzuri na Uingereza, huduma kufanywa na mawakala badala ya ofisi yenyewe huoni inajenga sura mbaya kwa watanzania. Swala la visa Nairobi, ni lini watakaa kikwelikweli kulitatua!
Jibu: Ni kweli huduma za visa zinatolewa na balozi husika, serikali ya Uingereza inajaribu kubana matumizi pia inaweka pamoja ili kudhibiti wageni wanaoingia uingereza ikiwemo Ugaidi na sasa wanashughulikia kwa pamoja Pretoria

UTAMBULISHO WA WAGENI NA MATANGAZO
 
Mwanri porojo sana, eti wanajipanga miaka 43 kuhamia Dodoma!
 
radio gani inarusha matangazo ya bunge live nisaidieni wadau
 
Wabunge wazingatie haya kuhusu mahakama ya kadhi. Kila ukikaribia uchaguzi CCM huja na mbinu chafu za kuwagawa wananchi ili wapate kura hata kama mbinu hizo zinamatokeao mabaya kwa amani ya nchi yetu. Hivi sasa CCM wameshatupa fupa ili wananchi wakimbilie na kuacha kujadili uovu wa CCM kama vile katiba mbovu pendekezwa ya kulazimisha na ufisadi mwingi ambao viongozi wa chama tawala inaufanya. Tunalazimika kufuata fupa hili lililorushwa na CCM ili kuzuia madhara ambayo nchi hii itayapata ikiwa tutawaachia CCM kufanya mambo machafu wapendevyo ili kubaki madarakani.

Mahakama ya kadhi ya serikali ya CCM haikubaliki kwa sababu nyingi, japo watetezi wake ambao CCM inawatumia wanakuja na sababu zao ambazo hazina msingi na zinapingana. Baadhi ya sababu zinazotolewa na wanaojiita wanazuoni wa kiislam, ambao wamewahi kutamka waziwazi kuwa Tanzania inaongozwa na mfumo kristoni ni kama zifuatazo:
1.Waislam wanafungwa na utaratibu maalum wa maisha ambao chanzo chake ni kurani na maelekezo ya mtume
2. Wanahitaji kufuata amri za mwenyezi Mungu na suna ya mtume na sheria hizo haziwezi kujadiliwa bungeni.
3. Wanahitaji mahakama ya kadhi inayokidhi mahitaji ya kijamii ya waislamu kwa sasa. Mambo yanayotajwa kwa sasa kuwa yatashughulikiwa na mahakama ya kadhi ni ndoa, mirathi, wakfu. malezi ya watoto. Wanasisitiza kuwa mambo hayo ni mahitaji ya kijamii na siyo fahari ya kidini, hivyo wenye imani nyingine isiyo ya kiislamu wasiwe na wasiwasi.

Shida moja wapo kubwa ya mahakama ya kadhi ni kuwa serikali ya CCM inataka kulazimisha watu kushiriki imani ya kiislamu, ilimradi tu wao wapate kura. Ni njia ya kuislimisha nchi, na hii ni kuwafurahisha wale wanaodai kuwa nchi hii inafuata mfumo kristo. Hebu angalia, anayeteua kadhi na wasaidizi wake ni rais wa nchi. Maana yake ni kwamba unajenga dhana kuwa rais anatakiwa awe muislamu kila wakati ili kukidhi matakwa ya uislamu. Ndiyo maana itakuwa vigumu kwa mkiristo kuwa rais wa Zanzibar ambako kuna mahakama ya kadhi. Kufuatia malalamiko ya watu wa imani nyingine na hasa ukristo kusema wazi kuwa kazi ya serikali si kuchagulia watu imani gani wafuate, watetezi wa mahakama ya kadhi kwa sasa wamekuja na version mpya ya utetezi. Hawataji kwa wazi kuwa mahakama ya kadhi itaamua kuhusu masuala ya Ramadhani.

Kwa ufupi, kuna hila na kujipinga kwa kauli zinazotetea mahakama ya kadhi ya serikali ya CCM. Wanasema ni mahitaji ya kijamii siyo fahari ya kidini. Wakati huo huo wanasema wanataka kufuata maelekezo ya kurani na mtume. Haya ni masuala ya imani yanayowahusu waislamu, kwa nini serikali iwe na dini? Katiba yetu inasema serikali haina dini bali watu wanadini zao. Hivyo mahakama ya kadhi inatakiwa kuanzishwa na kuendeshwa na waislamu wenyewe siyo wananchi wote. Kuna hoja kwamba viongozi wa serikali hutumia gharama za wananchi wote kuhudhuria sherehe za kuapishwa maaskofu au mashehe. Vitu viwili hivi ni tofauti kabisa. Kuhudhuria hizo sherehe ni adhoc, siyo lazima, hakuna matakwa yoyote ya kimfumo wa serikali. Kuweka sheria ya mahakama ya kadhi kuendeshwa na serikali ni kulazimisha kila mtu kishiriki uislamu. Unalazimishwa kulipa kodi ya kuhudumia mahakama hizo kuanzia ngazi ya kijiji, kata, tarafa, wilaya, mkoa, kanda na taifa. Na wahudumu katika mahakama ya kadhi ni waislamu tu, ‘makafri' kuwaruhusiwi. huu ni ubaguzi wa wazi. Kuna mtetezi mmoja anasema kuwa watu wa dini nyingine pia wanaweza kutumia mahakama ya kadhi. Hii ni kujichanganya, mara unasema ni kwa waislamu pekee kulingana na imani yao, mara unasema vingine. Mtu wa imani nyingine anahusika vipi na ibada za kiislamu. Maana mambo yanayosimamiwa na mahakama ya kadhi ni ibada. Hivyo mahakama hizi ziendeshwe na waislamu wenyewe pekee.

Kuna kitu kingine kimejificha katika madai ya mahakama ya kadhi. Kuwa mahakama ya kadhi itashuguhulika na mahitaji ya kijamii ya sasa ya waislamu. Hii inamaana kuwa mahitaji ya kijamii kwa waislamu yakibadilika, kama vile hitaji la kuhukumu wezi, waislamu watadai hitaji hilo la kijamii liongezwe katika mambo yanayoshughulikiwa na mahakama ya kadhi. CCM inatupeleka pabaya. Kuna watu hawana dini, kuna wanaofuata dini za asili, kuna wakristo, wahindu, serikali itagharimia uendeshaji wa mahakama za dini zote hizo na wale wasio na dini? CCM kweli ni janga la taifa.
 
Wabunge wazingatie haya kuhusu mahakama ya kadhi. Kila ukikaribia uchaguzi CCM huja na mbinu chafu za kuwagawa wananchi ili wapate kura hata kama mbinu hizo zinamatokeao mabaya kwa amani ya nchi yetu. Hivi sasa CCM wameshatupa fupa ili wananchi wakimbilie na kuacha kujadili uovu wa CCM kama vile katiba mbovu pendekezwa ya kulazimisha na ufisadi mwingi ambao viongozi wa chama tawala inaufanya. Tunalazimika kufuata fupa hili lililorushwa na CCM ili kuzuia madhara ambayo nchi hii itayapata ikiwa tutawaachia CCM kufanya mambo machafu wapendevyo ili kubaki madarakani.

Sasa tusicheze na mbwa atatufuata mskitini. Tukichekacheka na CCM ya sasa itatuingiza matatani.
Ni wakati wa kuwapumzisha hawa jamaa zetu japo kwa miaka 5 wataondokewa na ulevi wa madaraka walio nao kwa sasa.
Nchi nyingi zimefanimiwa baada ya kuwaondoa walewa madaraka, k.m Zambia,Malawi,Kenya n.k
2. CCM imegeuka chama cha kifamilia msije shangaa Salma Kikwete akipendekezwa kugombea urais na baadaye amwachie mwanae Ridhiwani.
 
Wabunge wazingatie haya kuhusu mahakama ya kadhi. Kila ukikaribia uchaguzi CCM huja na mbinu chafu za kuwagawa wananchi ili wapate kura hata kama mbinu hizo zinamatokeao mabaya kwa amani ya nchi yetu. Hivi sasa CCM wameshatupa fupa ili wananchi wakimbilie na kuacha kujadili uovu wa CCM kama vile katiba mbovu pendekezwa ya kulazimisha na ufisadi mwingi ambao viongozi wa chama tawala inaufanya. Tunalazimika kufuata fupa hili lililorushwa na CCM ili kuzuia madhara ambayo nchi hii itayapata ikiwa tutawaachia CCM kufanya mambo machafu wapendevyo ili kubaki madarakani.

Ndugu yangu kama umeusoma huo mswada , nadhani hukuuelewa. Unachofanya ni upotoshaji
 
Yote haya ni shida ya kikwete kuwa raisi. Ana hila sana na mambo mengi ya kichini chini huyu mtu. Ukujumlisha na tabia zake za kutokujali mambo ya taifa na shida za nchi, msishangae kwamba haoni hatari ya kusilimisha serikali kwa sababu he is insensitive.

Kujadili masuala ya kuingiza serikali kwenye dini ni kujadili kuvunja katiba. Wabunge angalieni. Unafiki wa ccm, unaamsha makundi yenye nia ovu kwa taifa ili kutufitinisha wakidhani nchi ikichafuka wao hawana shida maana watakuwa na ulinzi muda wote kwa vie ni watawala. Wanatumia kila mbinu hata kama ni chafu kama kuteka watu, kuua, kupiga kwa green guards, kuiba na kugushi matokeo na sasa mahakama ya kadhi ili mradi tu wabaki madarakani.

Ccm wasiokuwa na ndoto za kutawala na kupata ulinzi wa polisi na majeshi, ogopeni na kataeni huu umpumbavu. Nchi ikichafuka, kikwete, kinana, sheini, pinda watakuwa na ulinzi wa jeshi muda wote na haya madhara hayatawakuta wao wala familia zao. Wewe je? Watakukulindaje?

Ni ujinga kuipeleka nchi kwenye misingi ya kundi lililojaa vitisho ubabe, vurugu, na mitafaruku usiyokoma ukidhani utawaridhisha. Ni mwanzo wa vurugu kubwa zaidi. Ukitaka kulianglaia hiili, tazama mabango na comments zao wanazotoa hata humu jf. "Kadhi ni lazima hata kama ni kwa jihadi", "Mara tusipopewa kadhi tanzania haitakalika",' "Tukikosa kufanyiwa hiki, tutawanonyehs makafir"., halafu na wewe kiongozi unakuwa blackmailed ukadhani ukifanya vile utakuwa unajenga amani. Wehu.

Kama kadhi ni ibada yao, hawajakatazwa kuabudu. Wafanye kila wanaloliona linahitajika kwao lakini si kulazimisha serikali iwasimamie. Huu ni wehu na ni hila za kishetani kabisa. Na sabbu yao kubwa ei wawe kama Wakristo, Wakristo wako vile kweli? Mbona dunia ingeshateketea zamani?
 
Akichangia bungeni jioni hii amesema Kikwete amabadili karibu mawaziri 200. "Ninyi wabunge wa Ccm ambao hamjateuliwa labda hamjui kusoma na kuandika" Akaendelea kuuliza kwa miezi hii sita unambadilishia mtu wizara akafanye nini? Wakati akiendelea kutema cheche na kusema anadhalilisha taasisi ya urais na maneno yake hayana ukweli.
 
80% ya wabunge wa UKAWA ni waropokaji! CCM itatawala milele
 
Ameongea ukweli tuona mpaka Anna Kilango amepewa unaibu waziri.
 
Back
Top Bottom