Yametimia: MSD yaweka nembo za Serikali kwenye dawa zake; wizi wa dawa kudhibitiwa

HAMY-D

JF-Expert Member
Sep 18, 2011
7,149
3,817
WanaJF,

Kama ambavyo ipo kwenye Ilani ya CCM ya mwaka 2015-2020 kuwa, Serikali itahakikisha dawa katika Mahospitali na Vituo vya afya zinapatikana wakati wote. Na kama ambavyo ahadi hiyo imekuwa ikinadiwa na Rais Dkt. Magufuli katika kampeni zake, sasa ni hatua ya utekelezaji wa ahadi hii kwa wananchi.

Katika kulitekeleza hilo, Mkurugenzi wa MSD aliagizwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, kwa niaba ya Rais, kuhakikisha kuwa dawa zote za Serikali zinakuwa na utambulisho maalum ili endapo zikikutwa zipo katika maduka ya dawa binafsi, basi hatua kali za kisheria zichukuliwe dhidi ya wamiliki wa maduka hayo.

Ikumbukwe, MSD inahudumia hospitali za Serikali tu na vituo vyake na kamwe dawa ambazo usambazwa na MSD hazipaswi kuuzwa kwa wamiliki wa maduka ya dawa binafsi. Hili katazo lipo kisheria. Hivyo ni kosa la jinai kwa dawa za Serikali kukutwa kwa wamiliki wa maduka ya dawa binafsi. Ameeleza Mkurugenzi wa MSD.

Aidha, Mkurugenzi huyo aliongezea kuwa, MSD itafungua maduka ya dawa makubwa karibu na mahospitali ya Serikali ili kurahisisha zaidi upatikanaji wa madawa kwa urahisi ikiwa ni sambamba na kusambaza madawa hayo kote nchini katika vituo vya afya kwa wakati, ili wananchi wote wenye uhitaji wa madawa waweze kupata bila tabu yoyote ile.

Kwa kuhitimisha, Mkurugenzi huyo ametoa namba maalum na itabandikwa kwenye vituo vya afya na mahospitali yote ya serikali kwa dhumuni moja la msingi ambalo ni endapo mwananchi yeyote atapata tabu katika kupatiwa dawa, basi atumie namba hiyo kutoa taarifa MSD na kupiga ni BURE kabisa. Hali kadhalika mkurugenzi huyo alikiri kuwa ni kweli wapo watumishi wasio waaminifi ambao wamekuwa wakiiba dawa hizo.
 
Madawa kwenye hospitali za serikali hakuna.. MSD wanaidai serikali mabilioni serikali imeshindwa kuwalipa pesa zote hazina zilitumika kumpigia kampeni Magufuli
 
Je wakitoa kwenye haya mabox yenye nembo. Wakatengeneza mabox mengine wakiziweka huko watajuaje? Madawa yanatakiwa kuunzwa hospital tu..Au wangeanza na kupiga marufuku baadhi ya dawa ambazo zinahitajika kwa kiasi kikubwa.. Na wananchi ndio wangeanzia hapo kufuatilia.. Pia maduka binafsi yanatakiwa kununua dawa msd... Hili kuzibiti bei ya dawa.... Na pia kuwe bei elekezi kama kampuni za simu zinavyo uza vocha..... Itasaidia kidogo kupunguza msongo wa matatizo ya upatikanaji wa dawa...
 
Mbona ni jambo rahisi sana, siku za nyuma mlikuwa wapi? Je, wanaweza kukanusha kwamba walikuwa wanahusika na huu wizi? Kwanini tusiwachukue kuwa ni walewale waliokuwa wanaiba? Kwa nini maduka haya yasifunguliwe ndani ya hospitali hiO?
 
Tatizo mtoa mada huwa anakurupukaa, hajui kuna mpaka mafamasia kwenye hili jukwaaa!!!

Nembo zilikuwepo sanaa, na watu wanapiga hizo dawaa!!

Mwizi ni mwizi tu, ukija na mbinu hii yeye anakuja na nyinginee, solution ni kuwaondoa hao wezi.
 
Je wakitoa kwenye haya mabox yenye nembo. Wakatengeneza mabox mengine wakiziweka huko watajuaje? Madawa yanatakiwa kuunzwa hospital tu..Au wangeanza na kupiga marufuku baadhi ya dawa ambazo zinahitajika kwa kiasi kikubwa.. Na wananchi ndio wangeanzia hapo kufuatilia.. Pia maduka binafsi yanatakiwa kununua dawa msd... Hili kuzibiti bei ya dawa.... Na pia kuwe bei elekezi kama kampuni za simu zinavyo uza vocha..... Itasaidia kidogo kupunguza msongo wa matatizo ya upatikanaji wa dawa...

Nembo zipo kwenye vidonge sio ma box
 
Hivi hakuna stock taking kujua dawa zinatika vipi?
Wizi umekubuhu kiasi kila kitu kipigwe muhuri.
Imani haipo watu hawana uaminifu hawamuigopi Mungu. Hii hatari ikiwa kila mtu ni panya road.
 
Na hata huko katika maduka ya hospitalini wachunge zisiingizwe za wahuni unashangaa mda wote zinauzwa za wahuni alafu za serikali hazitoki. Lakini pia tuwashauri baada ya kupeleka hizo dawa mahospitalini wahakikishe imetengenezwa reja ya bei za dawa na ibandikwe nje ya maduka hayo ili wananchi wasije kuuziwa dawa aina moja kwa bei aina tatu tofauti, na hilo lifanyike nchi nzima.
 
Back
Top Bottom