Yamenishinda: Shemeji wa kiume ananitesa

Yamenishinda: Shemeji wa kiume ananitesa

jamani ndugu zangu wa jf, huyu jirani yangu ni kaka ana mkubwa tu na ana miaka 26 sasa na ni mhitimu wa diploma ya procurement mwaka juzi 2014 katika chuo cha uhasibu mbeya (TIA) na kwa sasa anakaa kwa dada yake mkubwa wa kwanza huku maeneo ya soweto mbeya. sasa shemeji yake (mume wa dada yake) huwa anapenda kumfanyia vituko vya mara kwa mara ila huyu jamaa anabaki kimya sana na kukosa la kufanya, ila yakimshinda huwa ananipigiaga simu na kuniomba ushauri lakini na mimi ninakosaga la kumwambia kusema kweli.

huyo mumwe wa dada yake kuna wakati huwa anamwambia jamaa amuwekee maji ya kuoga, kumuandalia chakula au hata kuwa anampigia nguo pasi kama dada yake hayupo, ilhali anajua kuna watoto wadogo na wanaweza kufanya shughuli kama hizo, na mshikaji anakuwa hana jinsi anaamua tu kumtumikia kafiri ili apate yake ridhiki.

kwa sasa ameomba aje akae na mimi kwa muda ili aondokane na hii karaha ya huyu bwana mkubwa, na mimi ndio nipo ninafikiria mombi yake kwa sasa.

anatia sana huruma............

Angekuwa Dar ningemtesa X2 coz akishika kisimu chake kaz kukandia wanaume wa Dar jf kumbe anaishi kwa dada.Akalime viazi umalila.
 
Mwambie ajisogeze...

Asibweteke asubiri kuajiriwa na kidiploma.

Aangalie mtaani kuna fursa gani....

Hata akifungua kigenge cha kisasa

Au akaangishe dagaa mchele feri aje kuuza

Kidogo kidogo asepe.

Au kwao mbeya kama wanalima ajihusishe na biashara ya mchele

Au afungue kibanda cha chips

Maana hapo anafukuzwa bila kuambiwa toka
kweli kabisa kabisa kaka. ila siwezi kumtosa best yangu huyu lazima nitakaa naye kidogo na kujaribu kumpa mwanga wa haya mema yaliyoshauriwa humu...........
 
Miaka 26 mtoto wa kiume anataka alelewe na shemeji, mtaani kuna watoto wa miaka 17 wanaendesha maisha bila hata hizo diploma. Msaidie mshkaji japo kwa kumfundisha kujitegemea kama ulivyo wewe.
 
Nadhani shemeji anajaribu kumpa msg hapo kua hamtaki kwake, na yeye kama anatafuta kazi au anategemea shemeji au dada yake amsaidie sio kwakwenda kumkalia kooni hivyo,binadamu wote sio sawa kila mtu na hulka zake,kwakiungwana
huwezi kum treat shemeji yako hivyo hata siku moja achilia mbali kua watoto wapo hata kama wasingekuwepo sio sawa kumfanyia hivyo mwenzie,lakini binadamu wanasahau kua anaetoa ni mungu leo yeye amepata hajui kesho itakuwaje..
 
Shit! Shit!
Huyo jamaa namjua kabisaaaa, si ndiye yule anayepiga kelele kila siku eti bunge lioneshwe live?
Shenzi zake kabisa, yani miaka 26 mtoto wa kiume unalilia ugali kwa shemeji?
Huyo shemeji akaze uzi tu maana hakuna namna....
Go Mr Shemeji go, ulipo tupo...!
 
ukiwa na shida bwana..utabadilishwa mwenendo tuu, mwenye nyumba atakunyoosha, msitiri mwenzako kwa muda, ila usimuachie akae kiholela tuu, atafute cha kufanya muanze ku-share costs na responsibilities
 
Mwambie arudi kwao ata kama ni kijijini, ataishije kwa dada ndo hao utasikia nilikua mjini kumbe alikua anafulia watu nguo
 
Mwanaume kukaa kwa shemeji yako.....Hii ni laaana kubwa sana kwa wanyakyusa
 
Kama kuna matusi ni wakati shemejiyo (Mume wa dadako) anapokuambia weye dume zima umpelekee maji ya kuoga chooni. Hilo lenyewe ni tusi. Aangalie, kuna siku mabaya yatamkuta.
Kwani lazima akae mjini ili atafute kazi? Sku hizi hata sm ya mchina inakamata mtandao. Kazi sku izi ni mtandaoni si kiguu na njia tena. Sasa, ka shemejiye anatoka asubuhi, kidume umelala, uamke saa 4 unywe chai alopika dadako. Saa 7 ule meza moja na shem chakula ambacho hujachangia, saa, siku, wiki, mwezi, mwaka jamaa anakuangalia tu. Tangu 2014. Unajitapa kuwa unatafuta kazi. Hata shem kachoka sasa. Huu ndo ukweli. Akukataaye hakwambii toka, matendo tu yatakuonesha.
Mshauri rafiki yako aende home kwao. Atafute kazi akiwa kwao. Ajishughulishe na mengine pia. Kutoka si lazima iwe ofisini, hata biashara/kilimo chamtoa mtu. Tena Morogoro!! Ardhi tele, mvua tele. Mnataka kazi za kuvaa shati nyeupe. Pole zenu
 
Aangalie ustaarabu kusubiri ajira na hicho kidiploma anasubiri meli airport..... Ajiandae kutumwa na shemeji ake, atatumwa zaidi ya hapo
 
Aangalie ustaarabu kusubiri ajira na hicho kidiploma anasubiri meli airport..... Ajiandae kutumwa na shemeji ake, atatumwa zaidi ya hapo

Evelyn;
Ukiwaambia hivyo wanasema; Mswalie Mtume yakhee. Kumbe huo ndo ukweli. Kama kishafika mahali pa kumwambia; dadako katoka, kaniwekee maji ya kuoga.....Wataka lugha gani?? Fumbo, mfumbie mjinga, ila mtoto wa mujini atalifumbua hilo.
 
Back
Top Bottom