BM-40 OPERATOR
Senior Member
- Oct 13, 2012
- 153
- 55
Jamani ndugu zangu wa JF,
Huyu jirani yangu ni kaka ana mkubwa tu na ana miaka 26 sasa na ni mhitimu wa diploma ya procurement mwaka juzi 2014 katika chuo cha Uhasibu Mbeya (TIA) na kwa sasa anakaa kwa dada yake mkubwa wa kwanza huku maeneo ya Soweto Mbeya.
Sasa shemeji yake (mume wa dada yake) huwa anapenda kumfanyia vituko vya mara kwa mara ila huyu jamaa anabaki kimya sana na kukosa la kufanya, ila yakimshinda huwa ananipigiaga simu na kuniomba ushauri lakini na mimi ninakosaga la kumwambia kusema kweli.
Huyo mumewe wa dada yake kuna wakati huwa anamwambia jamaa amuwekee maji ya kuoga, kumuandalia chakula au hata kuwa anampigia nguo pasi kama dada yake hayupo, ilhali anajua kuna watoto wadogo na wanaweza kufanya shughuli kama hizo, na mshikaji anakuwa hana jinsi anaamua tu kumtumikia kafiri ili apate yake ridhiki.
Kwa sasa ameomba aje akae na mimi kwa muda ili aondokane na hii karaha ya huyu bwana mkubwa, na mimi ndio nipo ninafikiria maombi yake kwa sasa.
Anatia sana huruma...