Habari zenu wana JF,
Miaka kadhaa iliyopita nilibaatika kukutana na msichana mmoja ambaye tulikuwa tukisoma nae miaka mingi ilyopita wakati wa shule ya msingi na kwakweli tulikuwa mabesti sana tena sana. lakini baada ya kumaliza shule ya msingi miaka hiyo kila mmoja alitawanyika kivyake mpaka miaka ya hivi karibuni tulipokutana nae, kweli upendo wangu kwake ukazidi mara dufu na ukafikia hatua ya kuwa wapenzi na hatimaye tukahamua kuoana nae. Baada ya miaka mitatu katika ndoa yetu, nikagundua mke wangu anatumia madawa fulani (phenobarbitone) na mara nilipokuwa nikimuuliza hizo dawa ni za nini alikuwa nasema huwa anatatizo la kuumwa tumbo na mara anapokunywa dawa hizo huwa anapata nafuu. lakini siku zilivyokuwa zikiendelea tatizo likazidi kujitokeza kwani akaanza kuwa anaanguka anguka na kupoteza fahamu mara kwa mara, na nilipokwenda kumuuliza dokta akasema huo ni ugonjwa wa kifafa, na akasema ni ugonjwa muda mrefu sana kutokana na vipimo alivyoviona. Dokta alishauri kuwa tusijaribu kupata mtoto kwani mara tu tutakapojaribu basi mke wangu anaweza kupoteza maisha. Sasa wanaJF, naomba ushauri wenu, kwa hali hii nifanye nini kwani raha ya maisha ni kuwa na watoto?