Yaliyotokea Vikao vya CCM Dodoma: Tafsiri Yangu

Bwana/Ndg Mjengwa kama kawaida yako umeandika article nzuri lakini yenye prophecies nyingi kuliko majibu.

Kitu nataka nikuambie damu ya kumsafisha Lowassa bado haijaumbwa au kutengenezwa. Wenye kuchafua jina wanazo silahanyingi wanazoweza kutumia pindi zitakapohitajika. To start with wanaweza wakatafuta faili la kambarage.

Kinachotokea sasa ni kwamba anakosekana mtu msafi wa kumtunga kidole Lowassa. Wote ni walewale. Subili ile siku atakayokutana ana kwa ana na wana CDM. Ndiyo siku yake ya kulia na kusaga meno. Sisi yetu macho na kupiga kura.
Umenena vyema...sasa kama wote ni walewale kwa nini wengine wachafu hawasemwi..ili silaha na vita iwe kali na hatimaye CCM itoke madarakani kirahisi...

Maggid hana makosa, kama tunataka ukweli tuwachonganishe..usije ukakuta kuna siku mtu anahama nchi!

Yaani kwa Maggid kuandika makala hii...si ni kiberiti au msukumo tosha wa wengine kutoa hizo silaha? kwanini?
 
Lowassa atajisafisha sana,lkn hatakati mbele ya watu wenye weledi wao. Hapa mtaani kwetu wanamsifia kwmb ni mtendaji na haundi TUME. Lkn hajatueleza ukweli kuhusu kuachia kwake ngazi.

Mwisho watz tunampelekaje ikulu mtu mwenye kashfa nyekundu kama zile???
 
Kundi la kina Sitta lina ajenda tatu kuu
1. Kumzuia Lowasa Kwenda Ikulu
2. Kumzuia Lowasa kwenda Ikulu
3. Kumzuia Lowasa kwenda Ikulu
Hawana ajenda nyingine, hawana mikakati, Sitta alikuwa spika, yeye kazi yake tulitegemea ingekuwa neutral, hatukutegemea yeye ndo aishikie bango kamati ya mwakyembe. Sasa tumegundua janja yao. nakubaliana na wewe Mjengwa. Lowasa ni mnyeyekevu sana, pamoja na kushambuliwa na vyombo vya habari hakuwahi kugombana navyo, hajawahi kumshambulia Sitta personally. Sita kaguswa kidogo na Mwanahilisi na Tanzania daima kaanza kutukana hovyo. Mwanasiasa hapaswi kuwa hivyo.

Hili nalo neno
 
Nilikuwa nimejiandaa kuchangia hii thread, ila nilipoona tu jina la mwandishi ni Maggid mjengwa basi nimechoka hapo hapo, yaani mtu huyu anaeweza kununuliwa na wajingawajinga kama kina Kusaga ili asitoe picha za tamasha la Anti virus kwenye blog yake ndio Lowasa atashindwa kumnunua fukara kama huyu?
Maggid ni mtu wa kupuuzwa kama wapuuzi wengine.
 
Aibu yetu, aibu yenu. Hii ni aibu sana, Mungu atunusuru. Mungu atupe faraja, Mungu ainusuru Tanzania yetu. Sina zaidi ya haya maana kuna mambo ambayo hayastahili hata kusemwa ila iko siku ukweli utadhihiri. Ikifika mahali mtu anaita kaniki 'nyeupe' na taa ina rangi "nyeusi" ujue huu ndio "mwanzo wa mwisho."
 
Napenda kujua ni wewe mjengwa au??

Lowassa kwanini mumtetee sana kunani yeye si kidume kwanini asiweke mambo hadharani si yeye huyo anasema siasa za tanzania ni za Hovyo hovyo iweje analia wanamchafua je kwanini yeye asiyaseme mwenyewe kwenye umma au mihadhara kuwa yeye hausiki kabisa na RICHMOND wala DOWANS au scandle yoyote ile?

UMMA unapenda kusikia KAULI yake kuwa kwanini yeye alijuuzulu Uwaziri Mkuu je ni kwa shinikizo au kwa hiali yake na atoe sababu za any of the reason kwanini alijiuzulu kama kwa shinikizo aeleze kwanini ama ni kwa hiali yake aeleze kwanini period msiwaweke watanzania pabaya maana Lowassa asitafute mchawi toka enzi za mwalimu Lowassa mwalimu alikukataaa kabisa wazi wazi iweje leo unajitakasa kwa kusema TZ kuna siasa za hovyo wakati nawe uko kwenye hizi siasa?
 
Nilikuwa nimejiandaa kuchangia hii thread, ila nilipoona tu jina la mwandishi ni Maggid mjengwa basi nimechoka hapo hapo, yaani mtu huyu anaeweza kununuliwa na wajingawajinga kama kina Kusaga ili asitoe picha za tamasha la Anti virus kwenye blog yake ndio Lowasa atashindwa kumnunua fukara kama huyu?
Maggid ni mtu wa kupuuzwa kama wapuuzi wengine.

Ndugu yangu Matola,
Asante sana. Nawe unahukumu bila ushahidi wala kutoa nafasi ya mimi kujitetea. Kule kwangu Mjengwablog kuna picha kibao za tamasha la anti virus la Mr Sugu.

Na mimi nimeanza kuandika tangu nikiwa Form Three pale Tambaza Secondary, ni mwaka 1986. Tena nilianzisha kijarida changu ' Tambaza News' nikiandika habari na makala kwa mkono kwenye A-4. Tuliokuwa nao Tambaza wanaujua ukweli huo. Na kamwe, katika miaka yangu zaidi ya 20 ya uandishi sijapata kupokea bahasha ili niandike makala. Siku zote nimeandika kutokana na kusukumwa na hoja ninazoziamini na ninazoweza kuzisimamia na kuwajibika nazo.
Tatizo letu WaTanzania ni kuamini kuwa kila mtu ana bei. Hivi hao wanaotuhumiwa ufisadi wana fedha kiasi gani kiasi kuweza kumuhonga kila mwandishi wa makala wa nchi hii? Kama una ushahidi wa mimi kununuliwa na kuwa kwenye payroll njoo nao hapa. Na ikithibitika, basi, nami sio tu nitaacha mara moja kazi hii ya kuandika, bali nitawaomba radhi pia wasomaji wangu wote.

Maggid,
Iringa,
 
Back
Top Bottom