Jeshi la Polisi nchini limeundwa kwa mujibu wa sheria ya Jeshi la Polisi Tanzania PFO Cap.322 na majukumu yake yameainishwa wazi katika kifungu nambari 5 cha sheria hiyo. Jukumu kubwa ni kulinda amani na pia maisha na mali za wananchi/ raia. Ili kutekeleza jukumu hilo muhimu, Jeshi la Polisi nchini limetoa tamko la maono, lengo na mikakati ambayo kwa muhtasari linajumuisha mambo muhimu yafuatayo:-
Dira ya Jeshi la Polisi ni kuifanya nchi yetu kuwa yenye utulivu na amani ambapo utawala wa sheria unathaminiwa na kuenziwa ipasavyo.
Jeshi la Polisi linayathamini mambo yafuatayo:-
Kwa kuzingatia Dira ya Jeshi la Polisi na mambo muhimu linayoyathamini, Jeshi la Polisi lina lengo kuu la kusimamia sheria na amani kupitia utekelezaji wa sheria na kanuni zilizowekwa kwa ajili ya ulinzi na usalama wa wananchi wote wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ili kufikia lengo hilo kuu, Jeshi la Polisi limejipangia kutekeleza mambo yafuatayo:-
Dira ya Jeshi la Polisi ni kuifanya nchi yetu kuwa yenye utulivu na amani ambapo utawala wa sheria unathaminiwa na kuenziwa ipasavyo.
Jeshi la Polisi linayathamini mambo yafuatayo:-
- Umuhimu wa kuheshimu haki za binadamu.
- Umuhimu wa uwazi kwa jamii.
- Umuhimu wa uaminifu.
- Umuhimu wa uadilifu.
- Umuhimu wa kuwaheshimu raia, na
- Umuhimu wa kuwatumikia wananchi kwa uadilifu.
Kwa kuzingatia Dira ya Jeshi la Polisi na mambo muhimu linayoyathamini, Jeshi la Polisi lina lengo kuu la kusimamia sheria na amani kupitia utekelezaji wa sheria na kanuni zilizowekwa kwa ajili ya ulinzi na usalama wa wananchi wote wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ili kufikia lengo hilo kuu, Jeshi la Polisi limejipangia kutekeleza mambo yafuatayo:-
- Kudumisha sheria na amani nchini.
- Kutoa huduma thabiti na toshelevu za ulinzi na usalama.
- Kusimamia kwa uadilifu nyenzo za utendaji na kuwajibika kwa matumizi yake; na
- Kuimarisha taratibu za kupeana habari, mifumo ya mawasiliano na