Mnyamwezi wa Urambo
JF-Expert Member
- Dec 7, 2011
- 928
- 275
Sample size yangu ni kubwa mkuu huku ni kwetu napajua. Nimeshalala hoteli nyingi sana hapo Tabora lakini huduma ziko chini sana. Tatizo unataka kufananisha tukio hilo na hoteli zote. kwamba nikienda kulala hoteli nyingine muhudumu atanibamiza na mlango uvunjike kama ulivyovunjika wa Goodley Hotel. Sivyo! Ukilala hotel zingine utakumbana na kero ya aina nyingine.....siyo kwamba kero zinakuwa zan namna moja. naomba unielewe mkuu.
Kwa mfano unaingia hotelini unakuta toileti pepa hamna wakati ni hoteli kubwa kabisa napo utasemaje? Na kitu kama toileti pepa kuigundua haipo ni mpaka uende toileti na uwe na shida nayo. Ukiomba toileti pepa utaambia zimeisha na wewe unataka kujisaidi asubuhi uwahi. hiyo siyo kero?
Sehemu yoyote walopita waarabu sijajua ni kwa nini,nilienda kufacilitate semina Mtwara wahudumu wa hotel hawajali wateja similar kesi Lindi napo ni hivo hivo lakini nilienda Mwanza,Mbeya,Kilimanjaro huduma safi sijui waliwapa dawa gani hawa waarabu.
Wewe ni muongo, mimi pia ni mzaliwa na nimekulia Tabora mjini. Usitegemee ulale guest za buku halafu upate matatizo uje ututukane humu. Karibu na stand kuna hoteli nyingi sana tu za maana kama GOLDEN EAGLE na FRANKMAN sijawahi kupata huduma mbaya toka kwao.
Huwezi kusema vibaya mkoa mzima kwasababu ya huyo mlevi na polisi njaa ambao wapo nchi nzima.
Pole Polisi wa TZ ni watafuta hela. Atafanya kitu chochote mpaka ipate hela yako. Kama huna kosa atasingizia umemtukanaPolisi wa Tanzania akili zao kama misukuke vile...
Hii ni kwa sababu imejaa vilaza waliokosa nafasi za kuendelea kimasomo...
usifikiri kwa kutumia hasira hautaeleweka, mbona hata mimi nilicheleweshwa ubungo mhudumu analiwa chumbani?Hapana mkuu......ni katika hali ya kuwa karibu na eneo la stendi.......Kwa taarifa tu kwa tabora hata hoteli iwe kubwa kiasi gani uelewa wa watu wa Tabora unafanana.
Mkuu unatuporomoshea matusi yote hayo wanyamwezi kwasababu ya muhuni mmoja tu?
Hututendei haki kabisa mkuu
Miafrika banah sijui ikoje!..huo ni umaskini au we ni le mbebez mwalimu.
Tatizo mnalala gest za maskini. Nenda lodge ya maana afu lala presidential suite uone kama utapata hayo majangazi!!
Mkuu kwani wewe huwa ukienda kampala huwa unalala Hilton Hotel? Kwani ukubwa wa hoteli ndio ubora wa huduma?
Wakuu natumaini hamjambo,
Leo napenda niwaeleze jinsi baadhi ya mikoa yetu ilivyo nyuma kimaendelo na tulikuwa hatujui sababu ya mikoa hiyo kuwa nyuma kimaendeleo. Lakini kwa safari yangu ya Tabora mjini nimegundua ni kutokana na upeo mdogo wa wananchi wa mikoa hiyo iliyo nyuma kimaendelo.
Ni kwamba nilikuwa likizo ya mwaka haki ambayo kila mtumishi anapaswa kupewa. Nilipomaliza likizo yangu usiku wa kuamkia tarehe 15 Mwezi huu nililala kwenye hoteli moja mjini Tabora karibu na stendi kwa ajili ya kujidamkia mabasi yanayokuja Dar Es Salaam ambayo saa ya kuripoti ni saa kumi na moja na nusu alfajiri. Nilifuata taratibu zote za kihoteli na ilipofika saa kumi na moja na robo alfajiri nilikuwa tayari (mimi na mke wangu) kwa safari.
Kufika mapokezi hatukukuta muhudumu yeyote. Nilijaribu kuita kwa sauti kumwita mhudumu atufungulie mlango tuondoke lakini hakuna dalili ya kuitikiwa. Bahati nzuri kuna mteja mwingine naye alikuwa akisafiri alfajiri hiyo naye akaja tukaungana kumtafuta muhudumu bila mafanikio.
Ndipo kwa kutumia maarifa mengine nikajaribu kumwita mlinzi wa nje huko getini aje atusaidie kutufungulia ama kumtafuta muhudumu atufungulie. Lakini tulishindwa kwa sababu getini ni mbali sauti zetu hazikumfikia mlinzi. Ndipo nikapata wazo la kumpigia simu jamaa yangu mmoja aliyepo Tabora mjini aje amgongee mlinzi kisha amfahamishe kuna watu ndani wanahitaji kutoka hotelini lakini hawamwoni muhudumu.
Wazo langu lilifanikiwa maana jamaa akaja akamgongea mlinzi wa hoteli na kumfahamisha ya kuwa muhudumu haonekani na kuna watu wanahitaji kutoka hotelini. Ndipo mlinzi alipomtafuta muhudumu akampata (sijui alimpata wapi hilo sijui). Muhudumu akaja kutufungulia lakini akiwa katika hali ya ulevi.
Baada ya kutufungulia (yule mteja mwingine amekasirika kupita maelezo) ndipo nikamwambia muhudumu nikiwa nimesimama mlangoni kuwa wasilalamike kutopata wateja maana moja ya sababu yawezekana ikawa ni hii aliyotufanyia leo.
Muhudumu akanijibu ".......hata usipokuja tena kwani mteja ni wewe peke yako? Nipishe nifunge mlango......." Huku akinisukumiza na mlango nitoke mlango ukabamiza mabegi niliyokuwa nimeshika mkononi na matairi ya mabegi yakavunja vioo vya mlango huo.
Kilichofuatia akaamuru mlinzi afunge geti tusitoke mpaka hapo polisi watakapokuja. Nikafungiwa ndani ya geti la hoteli kuanzia saa 11 dk 29 alfajiri mpaka polisi walipokuja saa 1 dk 40 asubuhi. Wakaja wakanikamata kwa tuhuma ya kuingia hotelini kwa nia ya kuharibu mali!
Kwa hiyo basi likaniacha na safari ikawa imekufa!
Nikawekwa mahabusu mpaka saa 5 na nusu asubuhi yule jamaa yangu alipotafuta watu wa kuja kunitolea dhamana. Kesi ikaamuliwa nilipe mlango wa hoteli shilingi LAKI SABA ili nisipelekwea mahakamani. Nikawaomba badala ya kulipa pesa mimi nitafute fundi aje atathmini gharama kisha atengeneze nimlipe.
Suala ni kutengeneza mlango....Nilipata upinzani mkali sana polisi kwamba nawafundisha kazi. Nikawaambia sheria za nchi yetu siyo nzuri,mlalamikaji anaaminiwa sana kuliko mshitakiwa.
Wao walikuwa na uthibitisho gani kuwa mimi niliingia hotelini kwa nia ya kuharibu mali? Aliyevunja ni muhudumu siyo mimi!!
Hatimaye ikakubalika nitafute fundi. Nikampata fundi gharama ya kioo ikawa ni shilingi elfu ishirini na ufundi ni shilingi elfu kumi tu. Mlango ukawa umekamilika kutengenezwa saa 7 dk 36 mchana.
Hayo ndiyo yaliyonikuta Tabora. Mlango wenyewe ni huu nilio u atach na muhudumu mwenyewe ni huyo dogo mwenye shati jekundu. Ameniboa sana........!!!!!
View attachment 246879
Yule jamaa mteja mwingine alitangulia kutoka sasa mimi nilipobaki kumweleza aliyotufanyia ndipo yakatokea hayo. Tukabaki wawtatu mimi, mke wangu na jamaa aliyekuja kumgongea mlinzi. Tulishindwa kutok maana geti lilifungwa na jamaa yangu aliyekuja aliingiza gari ndani Tusingeweza kutoka........
Na Tabora unavyopajua saa 11 alfajiri uanzishe varangati si utaambiwa jambazi!!! Polisi walivyokuja kwa suala la kioo tu walitoa pingu wanifunge sembuse ufanye fujo? Mkuu Tabora mimi ni kwetu napajua sana. Uelewa ni ziro! Hata ukiwa mwalimu ukapangiwa Tabora ukiacha tabora boys, Milambo na Tabora girls Tabora ni matatizo....!!!!!!!
watu wa tabora wanafanana uelewa??unaonekana ww n mjuaji saana,na ulilala hotel ya bei rahis,teheee tabora hakuna maendeleo ww ulienda wap na wap?Hapana mkuu......ni katika hali ya kuwa karibu na eneo la stendi.......Kwa taarifa tu kwa tabora hata hoteli iwe kubwa kiasi gani uelewa wa watu wa Tabora unafanana.
watu wa tabora wanafanana uelewa??unaonekana ww n mjuaji saana,na ulilala hotel ya bei rahis,teheee tabora hakuna maendeleo ww ulienda wap na wap?
maendeleo gani Tbr,punguzeni uchawi na uswahili watu tuje kuwekezaMkuu achana naye huyo anastress za kulipishwa gharama za mlango.
Kwa sisi tunaoijua Tabora ya miaka hiyo ghorofa ni ofisi ya mkuu wa mkoa tu mpaka sasa hivi, mabadiliko ya kimaendeleo tunayaona.
msamehe huyo malyenge(makengeza) amevurugwa
Mkuu achana naye huyo anastress za kulipishwa gharama za mlango.
Kwa sisi tunaoijua Tabora ya miaka hiyo ghorofa ni ofisi ya mkuu wa mkoa tu mpaka sasa hivi, mabadiliko ya kimaendeleo tunayaona.
msamehe huyo malyenge(makengeza) amevurugwa
Sasa wewe ndo umeanza dharau....................................Mbona kuna maghorofa kibao tu yamejengwa Tabora? Hivi wewe ni mnyamwezi wa Urambo ama ni mkimbizi wa Urambo? Maana kama Tabora ni kwenu usingeshindwa kuyaona maghorofa yaliyojengwa.....matokeo yake unakumbukumbu ya tabora ya miaka kibao..... Maghorofa yapo mengi siku hizi si kama zamani. Acha kudharau wanyamwezi. Tunazungumzia huduma mbovu Tabora na si kubeza maghorofa. Usitoke nje ya mada........