Yaliyonikuta Tabora

Sehemu yoyote walopita waarabu sijajua ni kwa nini,nilienda kufacilitate semina Mtwara wahudumu wa hotel hawajali wateja similar kesi Lindi napo ni hivo hivo lakini nilienda Mwanza,Mbeya,Kilimanjaro huduma safi sijui waliwapa dawa gani hawa waarabu.

Na quality za polisi wa Tabora ziko chini sana. Kuna polisi mmoja alijitambulisha yeye ni lawyer....lakini vitu alivyokuwa anazungumza ni contrary kabisa na sheria ya suhahidi aliyokuwa akiizungumzia.
 
yaani ulivyoianza thread yako na ulichokiandika tofauti kabisa!! Kuna lodge kibao tbr zinawahudumu wanaojielewa tena ukiwaambia wakuamshe unasafiri jamaa wapo on time sn!!

Hayo ni matatizo ya mtu binafsi, hizo guest za karibu na stand mimi huwa silali yaani nipo radhi nikalale ipuli kuliko hizo guest!

Huyo dogo mmoja hawezi kukufanya udraw conclusion kuwa wahudumu wote wa lodge za tbr wapo hivyo, sample size yako ni ndogo mno unless ungekuwa umelala lodge nyingi kidogo na ukakutana na the same thng kidogo ningekuelewa!!

Ulivyoianza thread yako haiendani na ulichokiandika!
 
Hili jambo kaka ni muhimu utaje hiyo hotel yasije yakatukuta,pia tukatumia silaa tulizo nazo kihalali kumpekekanmtu kuzimu.Hilo jambo ni muhimu kabisa kutaja tujiepushe na hiyo hotel kama ukoma.

Yaitwa Goodley Hotel ipo karibu na uwanja wa mpira wa Ali Hassan mwinyi. ni ya ghorofa hivi......
 
Sijaona uhusisno wowote wa mkasa huu na Tabora kuwa nyuma kimaendeleo. Ninachoona hapa ni kuwa wewe ndo upo nyuma sana kimaendeleo
 
Na quality za polisi wa Tabora ziko chini sana. Kuna polisi mmoja alijitambulisha yeye ni lawyer....lakini vitu alivyokuwa anazungumza ni contrary kabisa na sheria ya suhahidi aliyokuwa akiizungumzia.

mkuu huyo alitaka kukuharibu kisaikolojia tu hanalolote!
 
Sijaona uhusisno wowote wa mkasa huu na Tabora kuwa nyuma kimaendeleo. Ninachoona hapa ni kuwa wewe ndo upo nyuma sana kimaendeleo

sema na wewe!! Eti ukienda dar ukakuta mama ntilie mzembe unadraw conclusion kuwa dar itarudi nyuma kimaendeleo! Only in tanzania.
 
Na quality za polisi wa Tabora ziko chini sana. Kuna polisi mmoja alijitambulisha yeye ni lawyer....lakini vitu alivyokuwa anazungumza ni contrary kabisa na sheria ya suhahidi aliyokuwa akiizungumzia.

Anaweza kua lawyer ila wenye elimu za kuungaunga ni wasumbufu sana wanasumbua sana huku jamiini
 

Sample size yangu ni kubwa mkuu huku ni kwetu napajua. Nimeshalala hoteli nyingi sana hapo Tabora lakini huduma ziko chini sana. Tatizo unataka kufananisha tukio hilo na hoteli zote. kwamba nikienda kulala hoteli nyingine muhudumu atanibamiza na mlango uvunjike kama ulivyovunjika wa Goodley Hotel. Sivyo! Ukilala hotel zingine utakumbana na kero ya aina nyingine.....siyo kwamba kero zinakuwa zan namna moja. naomba unielewe mkuu.
Kwa mfano unaingia hotelini unakuta toileti pepa hamna wakati ni hoteli kubwa kabisa napo utasemaje? Na kitu kama toileti pepa kuigundua haipo ni mpaka uende toileti na uwe na shida nayo. Ukiomba toileti pepa utaambia zimeisha na wewe unataka kujisaidi asubuhi uwahi. hiyo siyo kero?
 
Taja jina la hotel Ili iwe fundisho...........inawezekana mmiliki pia yupo humu.........

siku nyingine nenda Zanzibar kale upepo na wife.......kule watu wamezoea utalii.........
Preta, umeniletea mteja mzuri..... Jamani TZ taamu sana kwa vituko!!
 
Sijaona uhusisno wowote wa mkasa huu na Tabora kuwa nyuma kimaendeleo. Ninachoona hapa ni kuwa wewe ndo upo nyuma sana kimaendeleo
Mkuu kumbuka mimi ni mzaliwa wa huko Tabora na sijawahi kuukana unyamwezi wangu. Ninayoongea ni kweli tupu.
Hebu nikupe mkasa mwingine wa nyuma. Nilikodi tzxi kunipeleka kijijini...njiani polisi wa tigo wakatusimamisha na kuanza kumhoji dereva ya kwamba tunaenda wapi. Akawajibu nampeleka huyu mteja. Wakakagua nyaraka zingine zote za gari wakakuta ziko safi. Wakamuuliza dereva gari hiyo imetengenezwa kubeba watu watano pamoja na dereva iweje imebeba watu wawili tu?
Sasa nikuulize mkuu hili nalo siyo kero? Au wewe unalionaje maana unaona kana kwamba Tabora naipondea wakati mimi ni mzaramo........
 
siku nyingine lala kwenu au kwa nduguzako. tabora hakuna hotels isipokuwa lodge na lodgekubwa kubwa
 
sema na wewe!! Eti ukienda dar ukakuta mama ntilie mzembe unadraw conclusion kuwa dar itarudi nyuma kimaendeleo! Only in tanzania.

Hiyo ni nyanja moja tu tena rahisi. Kumbuka mteja siyo huyu anayeondoka bali ni mteja ajaye. Mimi nakuwa ni marketing manager wa hoteli bila wao kujua kwa kuwa tu huduma niliyopewa ni nzuri. Mtu akikupigia simu leo yupo mahali fulani mkoani akitaka umwelekeze hoteli nzuri sidhani kama utamwelekeza hoteli uliyotukanwa ama kudharauliwa na mteja. Hiyo ni nyanja ya hoteli...bado hujaigusa sekta ya usafirishaji, elimu, afya na uchumi. Kwa watu wenye vichwa vibovu namna hiyo unategemea nyanja zingine zinazohitaji hekima ya juu zaidi unadhani wataiweza? Maendeleo yao itakuwa ni ndoto....!
 
Malyenge..pole kwa mkasa hata mm nakuunga mkono asilimia kubwa ya nyumba za kulala wagen hapo tabora wako hivyo hususan maeneo ya stend ya mabas..kwasababu wana uhakika wa kupata wateja ambao wanasafir..siku nyingne chukua chumba gest za mbali kidogo hao huwa na afadhar..kingine tabora inasifika kwa kuwa na huduma ya short time kwa wale wachepukaji..ndo mana wahudumu weng hawajali watu wanaolala mpaka asubuh
 
Kwanini usingelala pale Orion ?hata hivyo sababu ulizotaja hazina uhusiano wa moja kwa moja na maendeleo ya mkoa wa Tabora.
 
Kwanini usingelala pale Orion ?hata hivyo sababu ulizotaja hazina uhusiano wa moja kwa moja na maendeleo ya mkoa wa Tabora.

Mkuu kwani wewe huwa ukienda kampala huwa unalala Hilton Hotel? Kwani ukubwa wa hoteli ndio ubora wa huduma?
 
Polisi wa Tanzania akili zao kama misukuke vile...

Hii ni kwa sababu imejaa vilaza waliokosa nafasi za kuendelea kimasomo...
 

Na mimi pia ni mzaliwa wa huko, nimesoma huko (Msingi na Sekondari hapo Milambo), Nimeanzia kazi hapo kwa miaka 5. So I know Tabora, kuanzia Ipuli, Isevya, Kanyeye, Mwanza road, Ng'ambo n.k. Hizo case study zote hazina uhusiano na unyamwezi.
Je, haiwezekani kuwa mmilki na mhudumu wa hiyo Gest wasiwe wanyamwezi?
Je, haiwezekani hao polisi wa tigo wasiwe wanyamwezi?
Wanyamwezi si wajinga kiasi hicho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…