Yaliyomkuta Kitwanga kabla ya kung’olewa

Hadithi ya kitwanga karibu ifanane mna ya lowasa na jk.
Baada ya kuona rafiki amekuwa rais akajisahau kwamba sasa mda wa kula maisha umefika..kumbe rafiki yeye yuko serious na kazi
Mmh, najaribu tu kujiuliza; kati ya JK na Mamvi nani alikuaga serious na KAZI; nahisi mtazamo wako na wangu ni kama ipo tofauti.

To me the opposite is true; hivi ni lini serikali ya JK iliianza kutuhumiwa kwamba lipo OMBWE la uongozi kwenye serikali yake? Kama nakumbuka vizuri, shutuma hizo zilianza mara baada ya mamvi kujiuzuru u PM; mwenye kumbukumbu tofauti na zangu alete hapa.
 
Kwa hiyo hili gazeti linatuaminisha kwamba kutimuliwa kwa Kitwanga ni zengwe lililosukwa na 'maadui zake'? TISS nao inawezekana kweli wampelekee Rais taarifa za 'kupikwa'?

Na Rais JPM anaweza kuchukua maamuzi bila ya kujiridhisha? Muda utasema.
 
Atakuwa anajisafisha kiaina, lakini kachelewa sana.
 
Kwa hiyo JF ni jipu!!🙄
Sijaelewa point yako hapa sasa ni nini? Kama habari ilioandikwa na Mtanzania ni ya UONGO na wakati huo huo unasema wameitoa humu in other words ni kwamba habari za humu pia ni za UONGO! And then unashauri viongozi wa JF wawe na HATI miliki za habari za UONGO!!!!!? Sijakuelewa kabisa mkuu, hebu njoo kivingine please nielewe.
 
Asante kwa angalizo. Lakini jee ni kweli kuwa ndani ya ccm kuna hayo makundi hatari ya kutafutiana ubaya kiasi hicho? Maana hali hiyo ikiachiwa kuendelea inaweza kufikia kiwango cha kuondoana kabisa duniani kama mtu anaruka mitego yote anayowekewa.
Ndani ya CCM makundi yapo na nina wasiwasi kama yanaweza kuisha.

Kuna kundi jingine litaweka silaha chini lakini haina maana kuwa litakuwa limevunjika.

Tokea wakati wa Mwl. Nyerere kulikuwa na makundi yenye mtazamo tofauti lakini kwa sababu katiba ya chama na nchi ilikuwa hairuhusu kutoka nje na kuongea ili kupinga kinachofanywa na chama na serikali, ndiyo maana ilionekana kama hakuna makundi kwa sababu waliodiriki kupingana na fikra za Mwenyekiti na Rais, walijikuta wakiwa kwenye dhoruba kali kutoka kwenye dola.

Kipindi cha utawala wa Kikwete ndiyo tumeshuhudia ukweli wa makundi kutokana na haiba ya Kikwete ambaye ni democratic at the same time ni Laissez faire. Aliwapa nafasi ya kuongea na kufanya wapendavyo.

Kwenye utawala wa Kikwete Kundi moja lilikuwa ni progressive/reformer lakini lililojaa mafisadi na kundi lingine lilikuwa ni wahafidhina lakini lililojaa wazalendo.

Kwenye utawala wa Magufuli mpaka sasa unaonekana kutoa nafasi kwa kuwabeba wahafidhina, wazalendo na reformer/progressive, inabidi kundi la mafisadi lipambane a losing battle au liweke silaha chini na kuishi among them.

Kadri siku zinaenda tutazidi kufahamu uamuzi wa makundi na athari zake katika utawala la Rais Magufuli.

Makundi hayawezi kuisha na cha muhimu ni kiwango gani cha athari wa uwepo wake kwenye utawala.
 
Mkuu kuna habari nyingi humu JF waandishi wanaziiba then wanaziunga unga kesho yake unaona kwenye front pages za magazeti yao.
Haaya, na nyie mwazitoa wapi hizo hbr na story!!??? Nijuavyo, humu ndani weeengi wadaku tu, INA maana Mtanzania hutoaga hbr za udaku udaku!!??
 
Indeed they are trying at the their level best to exonerate him(hon Kitwanga) however, the truth has been revealed and action has been taken by the honorable President.
 
NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM

ZIKIWA zimepita siku sita tangu Rais Dk. John Magufuli amng’oe aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga kwa ulevi, mengi yamezidi kuibuka hadharani. Pamoja na uamuzi huo wa Rais Magufuli, imeelezwa kuwa Kitwanga pamoja na timu yake walikuwa wakifuatiliwa nyendo zao na makachero. Chanzo cha kuaminika kiliiambia MTANZANIA kuwa moja ya taarifa ambazo ziliwasilishwa na makachero hao kwa Rais Magufuli ndizo zilisababisha kiongozi huyo kulazimika kuchukua hatua hiyo.

Chanzo cha kuaminika kiliiambia MTANZANIA kuwa moja ya taarifa ambazo ziliwasilishwa na makachero hao kwa Rais Magufuli ndizo zilisababisha kiongozi huyo kulazimika kuchukua hatua hiyo.

“Unajua Kitwanga alikuwa akishughulikiwa muda mrefu bila yeye mwenyewe kujua, na hata kuondolewa kwake hadi sasa haamini. Wapo waliodai kuwa baada ya kuwasilisha bajeti yake Mei 16, mwaka huu alikwenda kulala Morogoro badala ya nyumbani kwake mjini Dodoma katika eneo la Sengia (Site 11).

“Lakini pia inadaiwa kwamba kwa muda amekuwa halali nyumbani kwake na badala yake kwenda katika moja ya hoteli (jina linahifadhiwa) mjini Dodoma ambako hulewa hadi asubuhi jambo ambalo si la kweli, ni kama mkakati wa kumshughulikia… na si hivyo tu, hata baadaye zilitolewa taarifa kuwa yupo Morogoro, ambako pia watu walimfuatilia kwa karibu, lakini kwa bahati nzuri hakuwepo.

“Tena si hilo tu, hata pia eti wanadai alilewa sana kwa kunywa Vodka hali ya kuwa hatumii kinywaji hicho, na bila kujijua tangu usiku alipokuwa na madiwani wake (Mei 19), alikuwa akifuatiliwa na vyombo vya dola, tena walikuwa wakitumika wanawake ambao kama ndio walikuwa wakiandaa taarifa mbaya dhidi yake,” alisema mtoa habari huyo ambaye yupo karibu na mbunge huyo wa Misungwi.

Chanzo hicho cha habari kilisema kuwa pamoja na hali hiyo, wapo baadhi ya vigogo kutoka katika mashirika na taasisi nyeti za Serikali ambao walikuwa na vita ya kufa na kupona dhidi ya Kitwanga, hadi kufikia kufanya vikao vya siri vya kumshughulikia.

Mtoa habari huyo alisema kuwa mipango hiyo ilipangwa kwa ustadi mkubwa, ambapo tangu alipoteuliwa kushika wadhifa huo kuna baadhi ya watu walikuwa wakimfutilia kwa karibu wakiwemo ndani ya idara zilizokuwa chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani.

“Unajua huyu bwana alianza kushughulikiwa muda kidogo tangu siku ilipotolewa taarifa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, iliyoeleza kwamba naye hakujaza fomu ya maadili ya viongozi wa umma, yeye pamoja na mawaziri wenzake akiwemo Balozi Augustino Mahiga na January Makamba, ingawa nguvu kubwa ilikuwa kwake.

“Na tangu wakati huo haukupita muda kidogo likaibuka suala la Lugumi na kama unakumbuka hapo alikuwa na vita ndani ya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) pamoja na Uhamiaji ambako kote huko kuna watu waliwajibishwa,” alisema mtoa habari huyo.

Alisema pamoja na hali hiyo, katika kile ambacho kilikuwa kikiwatesa baadhi ya watu ndani ya Serikali ni hatua ya ukaribu kati yake na Rais Magufuli ambao kuna wakati zilisambazwa video katika mitandao ya kijamii zikimuonyesha akiwa na kiongozi huyo wa nchi wakati huo akiwa Waziri wa Ujenzi katika Serikali ya awamu ya nne chini ya Rais Jakaya Kikwete.

“Katika video hiyo anaonekana Kitwanga akiwa na Rais Magufuli uwanja wa ndege ambapo alikuwa akimuhamasisha achukue fomu ya kuwania urais, jambo ambalo alitekeleza baadaye na kufanikiwa kupita katika mchujo ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

“Katika kile kinachooneka vita ya kimkakati kati ya makundi mawili ndani ya CCM, hasa wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, kundi moja linaonekana kufanikiwa kupitia kuondolewa kwa Kitwanga katika nafasi ya uwaziri,” alisema.
...

Chanzo : Mtanzania
TOO LTE TO DISCUSS KITWANGA SAGA LOH

POLEN SANA
 
Hata mjinga ataamini Kitwanga siku ile alikuwa ameamka nazo kwa jinsi alivyolijibu swali lile. Habari alikuwa anafuatiliwa au vipi hapa taarifa hiyo hainanafasi hata kidogo.
HIII M CCM BANA BASI KUSOMA AMA KUSIKIA AMJUII

BASI KUONA.NAKO.HAMJUII.AMA ILE VID AMKUONAA
 
A
Sijaelewa point yako hapa sasa ni nini? Kama habari ilioandikwa na Mtanzania ni ya UONGO na wakati huo huo unasema wameitoa humu in other words ni kwamba habari za humu pia ni za UONGO! And then unashauri viongozi wa JF wawe na HATI miliki za habari za UONGO!!!!!? Sijakuelewa kabisa mkuu, hebu njoo kivingine please nielewe.
Asante!
 
kiwango gani cha pombe kinatosha au kinatakiwa kwa mbunge kuwa nacho, niambieni najua kuna kiwango fuolani cha pombe huruhusiwi kuwa nacho wakati unaendesha gari
 
naona kiwango chako hapo kwa avatar ni sawa.............ila nadowload mantiki ya hoja yako
 
Indeed they are trying at the their level best to exonerate him(hon Kitwanga) however, the truth has been revealed and action has been taken by the honorable President.
period.
 
Sitamshambulia kwakuwa....NI RAFIKI YANGU.
 
NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM

ZIKIWA zimepita siku sita tangu Rais Dk. John Magufuli amng’oe aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga kwa ulevi, mengi yamezidi kuibuka hadharani. Pamoja na uamuzi huo wa Rais Magufuli, imeelezwa kuwa Kitwanga pamoja na timu yake walikuwa wakifuatiliwa nyendo zao na makachero. Chanzo cha kuaminika kiliiambia MTANZANIA kuwa moja ya taarifa ambazo ziliwasilishwa na makachero hao kwa Rais Magufuli ndizo zilisababisha kiongozi huyo kulazimika kuchukua hatua hiyo.

Chanzo cha kuaminika kiliiambia MTANZANIA kuwa moja ya taarifa ambazo ziliwasilishwa na makachero hao kwa Rais Magufuli ndizo zilisababisha kiongozi huyo kulazimika kuchukua hatua hiyo.

“Unajua Kitwanga alikuwa akishughulikiwa muda mrefu bila yeye mwenyewe kujua, na hata kuondolewa kwake hadi sasa haamini. Wapo waliodai kuwa baada ya kuwasilisha bajeti yake Mei 16, mwaka huu alikwenda kulala Morogoro badala ya nyumbani kwake mjini Dodoma katika eneo la Sengia (Site 11).

“Lakini pia inadaiwa kwamba kwa muda amekuwa halali nyumbani kwake na badala yake kwenda katika moja ya hoteli (jina linahifadhiwa) mjini Dodoma ambako hulewa hadi asubuhi jambo ambalo si la kweli, ni kama mkakati wa kumshughulikia… na si hivyo tu, hata baadaye zilitolewa taarifa kuwa yupo Morogoro, ambako pia watu walimfuatilia kwa karibu, lakini kwa bahati nzuri hakuwepo.

“Tena si hilo tu, hata pia eti wanadai alilewa sana kwa kunywa Vodka hali ya kuwa hatumii kinywaji hicho, na bila kujijua tangu usiku alipokuwa na madiwani wake (Mei 19), alikuwa akifuatiliwa na vyombo vya dola, tena walikuwa wakitumika wanawake ambao kama ndio walikuwa wakiandaa taarifa mbaya dhidi yake,” alisema mtoa habari huyo ambaye yupo karibu na mbunge huyo wa Misungwi.

Chanzo hicho cha habari kilisema kuwa pamoja na hali hiyo, wapo baadhi ya vigogo kutoka katika mashirika na taasisi nyeti za Serikali ambao walikuwa na vita ya kufa na kupona dhidi ya Kitwanga, hadi kufikia kufanya vikao vya siri vya kumshughulikia.

Mtoa habari huyo alisema kuwa mipango hiyo ilipangwa kwa ustadi mkubwa, ambapo tangu alipoteuliwa kushika wadhifa huo kuna baadhi ya watu walikuwa wakimfutilia kwa karibu wakiwemo ndani ya idara zilizokuwa chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani.

“Unajua huyu bwana alianza kushughulikiwa muda kidogo tangu siku ilipotolewa taarifa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, iliyoeleza kwamba naye hakujaza fomu ya maadili ya viongozi wa umma, yeye pamoja na mawaziri wenzake akiwemo Balozi Augustino Mahiga na January Makamba, ingawa nguvu kubwa ilikuwa kwake.

“Na tangu wakati huo haukupita muda kidogo likaibuka suala la Lugumi na kama unakumbuka hapo alikuwa na vita ndani ya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) pamoja na Uhamiaji ambako kote huko kuna watu waliwajibishwa,” alisema mtoa habari huyo.

Alisema pamoja na hali hiyo, katika kile ambacho kilikuwa kikiwatesa baadhi ya watu ndani ya Serikali ni hatua ya ukaribu kati yake na Rais Magufuli ambao kuna wakati zilisambazwa video katika mitandao ya kijamii zikimuonyesha akiwa na kiongozi huyo wa nchi wakati huo akiwa Waziri wa Ujenzi katika Serikali ya awamu ya nne chini ya Rais Jakaya Kikwete.

“Katika video hiyo anaonekana Kitwanga akiwa na Rais Magufuli uwanja wa ndege ambapo alikuwa akimuhamasisha achukue fomu ya kuwania urais, jambo ambalo alitekeleza baadaye na kufanikiwa kupita katika mchujo ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

“Katika kile kinachooneka vita ya kimkakati kati ya makundi mawili ndani ya CCM, hasa wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, kundi moja linaonekana kufanikiwa kupitia kuondolewa kwa Kitwanga katika nafasi ya uwaziri,” alisema.
...

Chanzo : Mtanzania
Huko kufuatiliwa kutokufuatiliwa wala si swala. Kwa hali ilivyotokea hata kama angelifanya mtu ambaye siku moja kabla alikuwa akihudumu kama Imamu au askofu katika nyumba za ibada angetendewa kama alivyotendewa Mh Kitwanga.
 
hata mimi unanipa wasiwasi kama unaelewa vizuri masuala ya uandishi na vyanzo vya taarifa
Very good question. Haya mleta mada jibu swali hilo, alipokuwa bungeni siku hiyo, alikuwa amelewa au hakuwa amelewa?
Maana umeeleza blabla nyingi bila kueleza iwapo kweli siku hiyo alikuwa amelewa au hapana.

Nina wasiwasi na uandishi wa aliyeandika habari hii kwenye gazeti la Mtanzania pamoja na mleta mada hapa jukwaani[/QUOTE
 
Very good question. Haya mleta mada jibu swali hilo, alipokuwa bungeni siku hiyo, alikuwa amelewa au hakuwa amelewa?
Maana umeeleza blabla nyingi bila kueleza iwapo kweli siku hiyo alikuwa amelewa au hapana.

Nina wasiwasi na uandishi wa aliyeandika habari hii kwenye gazeti la Mtanzania pamoja na mleta mada hapa jukwaani
kama kweli wewe ni Dr basi utakua wa miti shamba kama yule Prof pale mjengoni ikiwa unashindwa kuelewa logic ndogo namna hii na kupost utumbo
 
Back
Top Bottom