Amavubi
JF-Expert Member
- Dec 9, 2010
- 30,156
- 13,249
NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
ZIKIWA zimepita siku sita tangu Rais Dk. John Magufuli amng’oe aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga kwa ulevi, mengi yamezidi kuibuka hadharani. Pamoja na uamuzi huo wa Rais Magufuli, imeelezwa kuwa Kitwanga pamoja na timu yake walikuwa wakifuatiliwa nyendo zao na makachero. Chanzo cha kuaminika kiliiambia MTANZANIA kuwa moja ya taarifa ambazo ziliwasilishwa na makachero hao kwa Rais Magufuli ndizo zilisababisha kiongozi huyo kulazimika kuchukua hatua hiyo.
Chanzo cha kuaminika kiliiambia MTANZANIA kuwa moja ya taarifa ambazo ziliwasilishwa na makachero hao kwa Rais Magufuli ndizo zilisababisha kiongozi huyo kulazimika kuchukua hatua hiyo.
“Unajua Kitwanga alikuwa akishughulikiwa muda mrefu bila yeye mwenyewe kujua, na hata kuondolewa kwake hadi sasa haamini. Wapo waliodai kuwa baada ya kuwasilisha bajeti yake Mei 16, mwaka huu alikwenda kulala Morogoro badala ya nyumbani kwake mjini Dodoma katika eneo la Sengia (Site 11).
“Lakini pia inadaiwa kwamba kwa muda amekuwa halali nyumbani kwake na badala yake kwenda katika moja ya hoteli (jina linahifadhiwa) mjini Dodoma ambako hulewa hadi asubuhi jambo ambalo si la kweli, ni kama mkakati wa kumshughulikia… na si hivyo tu, hata baadaye zilitolewa taarifa kuwa yupo Morogoro, ambako pia watu walimfuatilia kwa karibu, lakini kwa bahati nzuri hakuwepo.
“Tena si hilo tu, hata pia eti wanadai alilewa sana kwa kunywa Vodka hali ya kuwa hatumii kinywaji hicho, na bila kujijua tangu usiku alipokuwa na madiwani wake (Mei 19), alikuwa akifuatiliwa na vyombo vya dola, tena walikuwa wakitumika wanawake ambao kama ndio walikuwa wakiandaa taarifa mbaya dhidi yake,” alisema mtoa habari huyo ambaye yupo karibu na mbunge huyo wa Misungwi.
Chanzo hicho cha habari kilisema kuwa pamoja na hali hiyo, wapo baadhi ya vigogo kutoka katika mashirika na taasisi nyeti za Serikali ambao walikuwa na vita ya kufa na kupona dhidi ya Kitwanga, hadi kufikia kufanya vikao vya siri vya kumshughulikia.
Mtoa habari huyo alisema kuwa mipango hiyo ilipangwa kwa ustadi mkubwa, ambapo tangu alipoteuliwa kushika wadhifa huo kuna baadhi ya watu walikuwa wakimfutilia kwa karibu wakiwemo ndani ya idara zilizokuwa chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani.
“Unajua huyu bwana alianza kushughulikiwa muda kidogo tangu siku ilipotolewa taarifa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, iliyoeleza kwamba naye hakujaza fomu ya maadili ya viongozi wa umma, yeye pamoja na mawaziri wenzake akiwemo Balozi Augustino Mahiga na January Makamba, ingawa nguvu kubwa ilikuwa kwake.
“Na tangu wakati huo haukupita muda kidogo likaibuka suala la Lugumi na kama unakumbuka hapo alikuwa na vita ndani ya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) pamoja na Uhamiaji ambako kote huko kuna watu waliwajibishwa,” alisema mtoa habari huyo.
Alisema pamoja na hali hiyo, katika kile ambacho kilikuwa kikiwatesa baadhi ya watu ndani ya Serikali ni hatua ya ukaribu kati yake na Rais Magufuli ambao kuna wakati zilisambazwa video katika mitandao ya kijamii zikimuonyesha akiwa na kiongozi huyo wa nchi wakati huo akiwa Waziri wa Ujenzi katika Serikali ya awamu ya nne chini ya Rais Jakaya Kikwete.
“Katika video hiyo anaonekana Kitwanga akiwa na Rais Magufuli uwanja wa ndege ambapo alikuwa akimuhamasisha achukue fomu ya kuwania urais, jambo ambalo alitekeleza baadaye na kufanikiwa kupita katika mchujo ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
“Katika kile kinachooneka vita ya kimkakati kati ya makundi mawili ndani ya CCM, hasa wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, kundi moja linaonekana kufanikiwa kupitia kuondolewa kwa Kitwanga katika nafasi ya uwaziri,” alisema.
...
Chanzo : Mtanzaniahttp://mtanzania.co.tz/?