Yaliyomkuta Davido kutoka Sony, sasa ni zamu ya Ali Kiba

ubuntuX

JF-Expert Member
Aug 18, 2014
1,977
2,200
Label ya sony imekuwa ikilalamikiwa jinsi inavyotreat wasanii mbalimbali wanaotokea Africa, pia imekuwa ikihusishwa na uuaji wa vipaji vingi barani hapa

Baada ya mwaka jana, Msanii Davido kusoteshwa na kuzuiliwa kutoa nyimbo mpya na label yake hii ya sony baana ya kusain nao mkataba mpaka hali hii ikazua maswali na mtafaruku mkubwa juu ukimya wake wa muda mrefu isivyo kawaida, sasa hali hiyo imemkuta msanii wetu kipenzi cha watu ALIKIBA

Ni zaidi ya mwaka sasa tangu alikiba alipoachia smash hit yake iliyotamba sana "Aje"
baada ya hapo ukimya umetawala pasi na washabiki wake wasijue nini cha kufanya

inasemekana sasa Sony ndio wanamuhenyesha nguli huyu na kusubilisha kutoa ngoma mpya mpaka hapo watakapoamua!

Hili jambo litakuwa na impact mbaya kwa Kiba, hasa ukiangalia jinsi ushindani ulivyo kwa sasa katika game yetu hapa nchini na afrika kwa ujumla

Sony, tuachieni msanii wetu atupe Raha "tumechoka" sasa
 
Hahahahahahah warundi nchini watakuwepo wengi tu Mkuu haupo pekee yako. Jamaa ana kipaji lakini bado hajajua namna ya kukitumia au ndiyo kishafika ukomo wake.
Jamaa ni mzuri, ila watu walim overate ili alete upinzani kwa Diamond kama kubalance game.

Kosa alilolifanya ni kudhani ile overate ilikuwa ya uhalisia na akaanza kulazimisha kuishi at an overated level.
 
Hahahahahahah warundi nchini watakuwepo wengi tu Mkuu haupo pekee yako. Jamaa ana kipaji lakini bado hajajua namna ya kukitumia au ndiyo kishafika ukomo wake.
Kheee.....kumbe hata mimi mrundi

Jamaa namfananishaga na mpishi wa pilau ambae baada ya kusifiwa, basi akaanza kuongezea manjonjo kwa kuweka asali, mapapai, nanasi, maziwa kwenye hiyo pilau akifikiri atawachizisha wateja wake kwa furaha kumbe ndio anaalibu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom