Magazetini
JF-Expert Member
- Aug 16, 2014
- 593
- 1,712
Video nzima inayoonyesha kilichojiri viwanja vya Biafra siku ya uzinduzi wa kuboresha usalama wa raia
Habari wakuu,
Leo ni wiki ya uzinduzi wa kuboresha usalama raia, shughuli inayofanyika kwenye viwanja wa Biafra jijini Dar es Salaam. Miongoni mwa waliofika ni Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, John Magufuli, Rais mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Kikwete na wengineo wengi.
Tuwe sote pamoja kujuzana yanajiri viwanja vya biafra
========
Mzungumzaji aliyepita ni mkurugenzi wa CRDB, Dr. Charles Kimei na miongoni mwa mambo aliyogusia ni utumbuaji majipu. Kwa sasa anayeongea ni kamishna wa jeshi la polisi Tanzania, Ernest Mangu.
Mangu: Tutakaa na wataalam ili kubuni vyanzo fedha ili kutimiza tuliyoyapanga na ni mkakati ili kuboresha huduma tunazozitoa kwa wananchi na kero zote kwa jamii. Mangu anasema wakati Magufuli anafungua bunge alisema 'Serikali nitakayoiunda nataka ihudumie jamii kwa haraka' hivyo mpango wao unajibu hilo tatizo.
Mangu amemshukuru Rais Kikwete kwani mpango wa kuliboresha jeshi la polisi ulibuniwa wakati wake.
Amesema mkuu wa mkoa asaidie pia wananchi watakuwa wamejisaidia wenyewe kwa kuweka taa kwenye nyumba zao mbele na nyuma kwani jiji la Dar es Salaam liko kwenye giza. Mangu anasema Bilioni 27 zinahitajika ili jiji la Dar es Salaam liwe kwenye kiwango cha juu cha usalama pengine kuliko majiji yote Afrika.
Mwigulu Nchemba: Hamna demokrasia ambayo haina mipaka, mpango wa jeshi la polisi unatarajia kuanza utekelezaji wake Julai 1, 2016.
Mwigulu amewataka wananchi wawe wanatoa taarifa ili kuzuia uhalifu, amemuomba Rais Magufuli kupata fedha za kuweza kutekeleza mpango wa jeshi la polisi ili kuundoa uhalifu kwenye jiji la Dar es Salaam ambayo pia itavutia wawekezaji. Amesema hadhara sio ya kwake na alikuwa anachomeka, anamkaribisha Rais Magufuli.
Rais Magufuli: Kwa niaba ya watanzania, niwashukuru wananchi wa Dar kwa kuweza kuacha shughuli zenu na kuja kuhudhuria, wateni wenzangu wakwere wanasema shughuli ni watu. Nawashukuru CRDB, NMB pamoja na Super doll ambao wakurugenzi wao wako hapa, pia nashukuru nchi ya Malaysia ambao ndio wamesaidia uanzishwaji wa big results now(BRN) na mimi nakushukuru kwa kuona matokeo ya big results now.
Nashukuru watu wa biafra kwa kunipa kura nyingi ambapo nilifanya kampeni na kufanikiwa kuwa Rais mpaka natamani kuanza kampeni lakini uchaguzi umekwisha.
Amemuita mstahiki meya wa Kinondoni aje asalimie kwani ujambazi hauna chama(Hayupo). Badala yake amemuita diwani wa Kinondoni (CHADEMA) na amesalimia.
Anaesalimia kwa sasa ni mwenyekiti wa mkoa Dar es Salaam, Madabida.
Rais Magufuli amehoji kwanini jambazi aende kufanya ujambazi bila kupokonywa bunduki yake haraka wakati wao pia wana bunduki. Ametoa wito kwa polisi wote nchini, jambazi akienda sehemu na bunduki kufanya uhalifu, apokonywe bunduki yake haraka na polisi wanaowapokonya majambazi bunduki haraka wasipelekwe mahakamani, wapandishwe cheo kwani wananchi wamechoka.
Amesema jeshi la polisi wakiamua Tanzania kuwe na amani, kutakua na amani. Amesema vijana wanaweza kuwa na hamu ya kufanya kazi lakini maofisa wa polisi wanawabana bana. Rais amezungumzia mchezo wa kuvujisha taarifa za wanaotoa taarifa za uhalifu na kukemea.
Rais amesema pia waliotoa msaada, wakitokana na ujambazi pia wakamatwe. Amesema yeye hatumbui majipu lakini yanajitumbua yenyewe.
Magufuli ametoa wito kwa watanzania wote kuendelea kuliamini jeshi la polisi, kushirikiana nalo na kutoa taarifa kwa jeshi la polisi.
Rais ametoa rai ya kufunga CCTV kwenye mitaa, amesema Kinondoni ndio inasifika kuwa na uhalifu mwingi katika nchi hii. Amesema wilaya ya Kinondoni ilikuwa na vitendo vya uhalifu 8,094 na mwaka 2015 vikafika 8,804.
Rais ametoa agizo kwa TCRA ambao ndio wana wajibu wa ku-monitor simu zote washirikiane na jeshi la polisi. Asietaka kushirikiana na jeshi la polisi aondoke.
Rais Magufuli ametoa pongezi kwa Rais mstaafu, Jakaya Kikwete na IGP mstaafu kwa kubuni mpango huo na kuzaa matunda. Amesema amedhamiria kuijenga nchi kwa nguvu zake zote na atafanya kazi kwa nguvu zake zote na hatabagua mtu.
Rais ametaka Tupeleke maendeleo mbele na kuweka vyama pembeni.
Magufuli ametaka makampuni ya ukandarasi yaliosimamishwa na Makonda waanze kuchukuliwa hatua. Kasema vyombo vya dola vipo havitaki kuchukua hatua.
Rais ameshukuru bunge kwa kupitisha muswada wa mafisadi ili wanyooke. Amesema alikuwa anachomekea na atarudi siku rasmi kuzungumzia hilo swala.
Kwa sasa Rais Magufuli anazungushwa kwenye mabanda ya polisi.
============
Shughuli imeisha