Yaliyojiri: Uzinduzi wa kampeni za CHADEMA jimbo la Kalenga

mkuu,mawazo anatafuta umaarufu kwa nguvu, eti na yeye anamuiga mwehu lema ili akubalike kwa wahafidhina wa kaskazini, amepewa ofa ya kugombea ubunge kanda ya ziwa na wenye chama mbowe na lema

kwa taarifa yako hakuna gamba hata mmoja mwenye uwezo wa kupambana na kamanda mawazo,iulizeni mizigo yenu kama Ngeleja,Limbu,Ndasa na Mawe3 watawapeni majibu!!!!
 
Hiki ndio chama chetu chama chama watanzania wote tume ya uchaguzi irekebishe daftari la wapiga kura waone chama kitavyoshinda kwa asilimia mia kila mahali
 
on 14:31


Wanachi wa Kata ya Kalenga walio hudhuria kwenye mkutano wa ufunguzi,wa kampeni za Ubunge katika Jimbo la Kalenga -Iringa Mjini

Chief wa Wahehe akisalimia wananchi katika mkutano wa adhara

Ndugu Benson Kigaila akisema neno la Ufunguzi wa Kampeni za ubunge

Katibu Mkuu wa Chadema Dir Wilbroad Slaa akifungua rasmi Kampeni za Ubunge Kalenga

Silaa za Ushindi

Katibu Mkuu wa Chadema Dir Wilbroad Slaa akifungua rasmi Kampeni za Ubunge Kaleng


Mbunge mtarajiwa Bi Grace Mvanda Tendega akinadi sera zake kwa wananchi




Katibu Mkuu wa Chadema Dir Wilbroad Slaa akimnadi Bi Grace Mvanda Tendega kwa wananchi wa Kalenga

Nguvu ya Umma

Katibu Mkuu wa Chadema Dir Wilbroad Slaa akiwa ameongozana na Mgombea Ubunge Kupitia CHADEMA Bi Grace Mvanda Tendega,baada ya kumalizika kwa mkutano

Huu Ndio Msafara wa kumsindikiza Bi Grace Mvanda Tendega kutoka Kata ya Kalenga Kurudi Iringa Mjini

Bi Grace Mvanda Tendega kwenye gari katika msafara kutoka Kata ya Kalenga Kurudi Iringa Mjini

 
Wananchi wako Upande Mmoja - DAFTARI LA UCHAGUZI Liko Upande Mwingine...

Nchi yetu Mwenye haki hana VOICE...
 
Bila kuboresha daftari la wapiga kura na kuwa na tume huru ya uchaguzi ni ndoto kwa upinzani kupata ushindi wa kishindo! Believe me or not!
 
Ni bahati mbaya sana hao vijana hawajajiandikisha kupiga kura. CCM itashinda kwa kura za vikongwe waliojiandikisha mwaka 2010 (ambao wanadhani kuwa Nyerere ndiye bado rais wa nchi hii).
 
Upeo wetu wa kuchambua mambo ni mdogo wengi wetu....wezee huwa hawatoki kwenye mikutano, pili vijana ni chachu ya ushawishi na ndo wanalea wazazi wao..mf nikiamua baba yangu asipigie chama fulani hapigi...tatu wazee sasa hawapigi kura kwani wameona hakuna jipya, nne vijana wengi walijiandikisha kipiga kura na tafiti zimeonyesha uchaguzi ulopita asilimia kubwa ilitoka kwa vijana na ndo mana kura za mshindi wa kwanza zilishuka, kumbukeni roma haikujengwa siku moja. Wosia...ccm msibweteke eti wapiga kura ni wazee....na cdm msilale kwa kuwa wasomi na vijana wAnawasupport. Piga kazi. Nashangaa ccm.kuweweseka wakati mpo madarakani kwa takriban 53 years, leteni impact ili iwauze na wapunzani hatafyata bila hivyo watawasumbua.....mjifunze marekani, australia, uingereza, misri....watu wameamuka....unyerere haupo tena. Slowly but surely
 
Picha nyingi ninazoziona za mikutano ya CDM ni za mtaji wa 2015-2020 kama daftari litaboreshwa.
 
chedema mpaka sasa wapiga kura wakewalio wengi ni wanachama wa ccm
chadema wameisha tafuta mtaji wa watu wengi sana na wameisha upata ila bado wajasajiliwa tu.
kwa mfano mimi nilikua mteja mzuri sana wa ccm ila sasa baada ya kupata elimu kupitia chadema siwataki tena ccm ata kuwaona na kama ningekuwa na uwezo.................."
 
Kwa mtaji huu ni vizuri CHADEMA wakaanza kujiandaa kisaikologia kwa janga litakalowafika la kukataliwa na wanaKalenga wengi kwenye sanduku la kura.

Kama huwezi kusoma basi hata picha zinatoa ujumbe mwanana kisiasa.

Sanduku la kura halina spinning za kisiasa.

Sanduku la kura huwa halijali umetumia aina gani ya usafiri, watu na mgombea.

Sanduku la kura halijali siasa za matukio kama kuongelea mambo ya posho za bunge la Katiba kwenye kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge.

Sanduku la kura linajali na kuheshimu sera na ilani ya uchaguzi
 
Nawaonea huruma sana chadema wameshindwa tayari kabla hawajaanza. Very sad to them.
 
Chadema waendelee kutoa elimu ya uraia kalenga. Wana kalenga wamenyonywa na maccm kwa muda mrefu sana! Ccm inatumia udhaifu wa wananchi wa vijijini ili kuendelea kutawala! Ccm imediriki hata kurithisha ubunge kwa mtoto wa marehemu mgimwa ikiamini wanakalenga si chochote! Jambo hili lingefanyika sehemu nyingine ccm wangepata kipigo cha mbwa mwizi kwenye uchaguzi huu! Wana kalenga amkeni! Kumekucha.
 
Wana Kalenga chagueni chaguo sahihi. Itoseni CCM miaka yote hamsini inawatumia kama vikaragosi.
 
Chadema waendelee kutoa elimu ya uraia kalenga. Wana kalenga wamenyonywa na maccm kwa muda mrefu sana! Ccm inatumia udhaifu wa wananchi wa vijijini ili kuendelea kutawala! Ccm imediriki hata kurithisha ubunge kwa mtoto wa marehemu mgimwa ikiamini wanakalenga si chochote! Jambo hili lingefanyika sehemu nyingine ccm wangepata kipigo cha mbwa mwizi kwenye uchaguzi huu! Wana kalenga amkeni! Kumekucha.
Acha uongo wewe chadema ndiyo wanyonyaji wakubwa.
 
Back
Top Bottom