Yaliyojiri Uwanja wa Taifa: Taifa Stars 2 - 1 Equatorial Guinea

mugah di matheo

JF-Expert Member
Jul 28, 2018
6,276
12,336
Taifa Stars ya Tanzania inachuana na Equitorial Guinea leo usiku na mshambuaji wa taifa stars Mbwana Samatta amesema ana matarajio makubwa kuwa watakuwa na matokeo mazuri katika mechi hiyo.

taifa stars.png

Vijana hao wa Taifa Stars watatumia uwanja wao wa nyumbani kujaribu kupata alama zote kwenye mechi hiyo itakayoanza saa moja za usiku majira ya Afrika Mashariki jijini Dar es saalam.

Taifa stars ambao hawakushinda mechi yoyote katika fainali ya kombe la mataifa bingwa Africa AFCON zilizoandaliwa nchini Misri, wanamatarajio makubwa hasa baada ya mahasimu wao wa jadi Harambee Stars ya Kenya kutoka sare ya 1-1 na Misri huko Alexandria.

AFCFF933-3DA1-41B4-8EFE-5468D00FC625.jpeg

UPDATE
E881CBD5-C389-49AF-8952-69679B7F7623.jpeg

======


BAO la la dakika za usiku lililofungwa na Abubakar Salum 'Sure Boy' limeiwezesha Taifa Stars kuvuna alama tatu katika mchezo wa kusaka tiketi ya kushiriki fainali za Afcon 2021 baada ya kuifunga Guinea ya Ikweta mabao 2-1.

Mchezo huo uliopigwa Uwanja wa Taifa ulishuhudiwa Stars wakiutawala kwa asilimia kubwa lakini iliweza kujikuta ikienda mapumziko ikiwa nyuma bao 1-0.

Mchezo huo ulianza kwa kasi kwa wenyeji kuutawala kutokana na mashambulizi yaliyokuwa yakifanywa na nahodha wa Stars, Mbwana Samatta aliyekuwa akisaidiana na Simon Msuva kuliandama lango la wapinzani.

Samatta alikosa kuiandikia bao Stars dakika ya pili baada ya mpira wake kuokolewa na Mlinda mlango wa Felipe Ovono ambaye alionesha umahiri wake wa kuokoa michomo.

Wakati vijana hao wa Kocha, Etienne Ndayiragije wakiendelea kulisakata soka mbele ya watazamaji waliojitokeza kwa wingi kutoa sapoti, walijikuta wakiruhusu bao dakika ya 15 lililofungwa na Petro Obiang ambalo lilidumu hadi mapumziko.

Hata hivyo Samatta alikosa nafasi nyingne ya kuisawazishia Stars dakika ya 40 lakini, Ovono aliweza kuzuia hatari hiyo langoni mwake na kuonekana kuwa kwenye ubora katika mchezo huo.

Kipindi cha pili kilianza kwa Stars, kumtoa Hassan Kessy na nafasi yake kuchukuliwa na Ditram Nchimbi mabadiliko ambayo yalimfanya, Samatta kuwa huru katika uchezaji wake na yalifanikiwa kusawazisha bao.

Bao la Stars lilifungwa na Simon Msuva dakika 68 baada ya kumzidi ujanja kipa wa Guinea ambaye muda mwingi alionekana kuwa kinara wa kuizuia Stars kufunga na hadi dakika za nyongeza, Sure Boy alipoachia shuti kali lililozama nyavuni na kuipa ushindi Stars mabao 2-1.

Kikosi kilichanza cha Stars kilikuwa na Juma Kaseja, Erasto Nyoni, Kelvin Yonda, Hassan Kessy, Bakari Mwamnyeto, Salum Abubakar, Mbwana Samatta, Simon Msuva, Mohamed Hussein, Farid Mussa na Mzamiru Yassin.
 
Hii Game Kocha Mgunda alishaharibu hali ya hewa, ila namshukuru sana Mzungu Bongozozo amejitahidi sana kuturejeshea uzalendo wetu. Naandaa Tochi ya kwenda kummulika kipa wa Equatorial Guinea.
Bongozozo anakomaa kuturudisha mchezoni.
Hahahaha, mzungu kachungulia fursa ,yule liquid kaishia wapi
 
Back
Top Bottom