Yaliyojiri: Sherehe za miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar

Yaliyojiri: Sherehe za miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar

Hamuyu

Senior Member
Joined
Mar 29, 2010
Posts
118
Reaction score
21
Tupo ndani ya uwanja wa amani, uwanja umejaa na umependeza tutawaletea matukio yote. viongozi mbali mbali wameshakuwepo
 
Tupo ndani ya uwanja wa amani, uwanja umejaa na umependeza tutawaletea matukio yote. viongozi mbali mbali wameshakuwepo

Mbona kimya mkuu, maana huku TANESCO wameishaloga.
 
Kwa mliokwenye uwanja wa Amani na mnaofuatilia kilele cha sherehe za miaka 50 ya mapinduzi ya Zanzibar, tushirikishane mambo ya kuvutia na kupongezwa na yale ambayo unahisi wangeweza kufanya vizuri zaidi ya walivyofanya. Bila kusahau mikanganyiko ya itifaki kwa marais wawili. Karibuni..!
 
Kila anayeingia uwanjani anagawiwa kofia na mwavulia kujikinga na jua/mvua
 
The three musketeers wametokelezea? All for one, one for all. United we stand divided we fall. Hurray COW.
 
Wimbo wa taifa la Zanzibar anaujua shein tu. Huku bara hatuvijui vitu hivyo. Nadhani leo jk yuko zanzibar kama rais wa Tanganyika.
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Nipo naangalia sherehe za miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar lakini nimeshangazwa kuona sherehe zimetawaliwa na bendera za CCM utafikiri ni sherehe za CCM. Je hizi sherehe haziwahusu waumini na wanachama wa vyama vingine? Ni aibu kwa serikali kushindwa kutofautisha sherehe za kitaifa na zile za Kichama.
 
CCM wameteka sherehe, CUF hawaonekani. Ni chipukizi wa ccm, uvccm wanafanya gwaride wale wa cuf hata kutajwa tu hakuna.
 
Mbona yametawaliwa kiCCM zaidi? Je Rais Kagame na Uhuru wapo?
 
Hakika hizi sherehe ni za CCM,inakuwaje sherehe za kitaifa kama hizi yanatajwa makundi ya chama tena kimoja?
 
Nipo naangalia sherehe za miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar lakini nimeshangazwa kuona sherehe zimetawaliwa na bendera za CCM utafikiri ni sherehe za CCM. Je hizi sherehe haziwahusu waumini na wanachama wa vyama vingine? Ni aibu kwa serikali kushindwa kutofautisha sherehe za kitaifa na zile za Kichama.
Ule Umoja wa Kitaifa upo wapi au ni wa kwenye ulaji tu serikalini?
 
Haya maonesho yamefana sana especially haya ya waandamanaji na mbwa
 
Nipo naangalia sherehe za miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar lakini nimeshangazwa kuona sherehe zimetawaliwa na bendera za CCM utafikiri ni sherehe za CCM. Je hizi sherehe haziwahusu waumini na wanachama wa vyama vingine? Ni aibu kwa serikali kushindwa kutofautisha sherehe za kitaifa na zile za Kichama.

Wengine hawahusiki, hizi ni sherehe za kichama kitaifa, ndio chama cha MAPINDUZI, wao ndio wamiliki wa mapinduzi...
 
Back
Top Bottom