Yaliyojiri ndani ya #Malezi|#SimuliziZa116

Yaliyojiri ndani ya #Malezi|#SimuliziZa116

Sema Tanzania

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2016
Posts
251
Reaction score
466
Ilikuwa ni siku ya tarehe 2 Januari 2018 ambapo mshauri wetu wa Huduma ya Simu kwa mtoto alipokea simu ya mama kutoka wilaya ya Ubungo. Mama huyo alikuwa na malalamiko ya kukosa matunzo ya mtoto kutoka kwa baba yake.

Mama alisema ‘Mzazi mwenzangu hatoi matunzo kwa mtoto wetu tangu alipozaliwa mpaka sasa amefikisha umri wa mwaka mmoja’. Mshauri wetu aliuliza kama kuna hatua yoyote aliyowahi kuchukua kabla ya kupiga #116 na mama akaeleza kuwa hakuwa amechukua hatua yoyote.

Mshauri wetu aliwasiliana na Afisa Ustawi wa Jamii wa wilaya ya Ubungo na kumueleza juu ya tatizo la mama la kutelekezwa pamoja na mwanae. Afisa Ustawi alishauri kuwa mama afike ofisi ya Ustawi wa Jamii wilaya ya Ubungo siku ya tarehe 5 Januari.

Ilipofika tarehe 5 Januari mshauri wetu aliwasiliana na mama aliyekua na furaha kwa kuwa alifanikiwa kupata msaada kutoka kwa Afisa Ustawi wa Jamii. Alieleza kuwa Afisa Ustawi alizungumza na wazazi wote wawili na kumuelewesha baba mtoto juu ya majukumu yake ya malezi kwa mwanae na kuwa kinyume na kutofanya hivyo anaweza kushtakiwa kisheria.

Baba mtoto alikiri kutowajibika kwa malezi kwa kipindi chote cha mwaka mmoja na kuahidi kuwa sasa yupo tayari kuwajibika kama baba na mlezi wa mtoto na yupo tayari kutoa matunzo kwa mtoto wake kila mwezi.

Huduma ya Simu kwa Mtoto kupitia namba inaendelea kusikiliza na kufikia watoto wengi zaidi hata sasa. Akina mama wengi waliotelekezewa watoto wanapata msaada kupitia huduma hii. Tafadhali piga namba #116 sasa uzijue huduma za mtoto hapa Tanzania ama uweze kushiriki kumuokoa mtoto anaefanyiwa ukatili. Mwambie rafiki tuifanye jamii kuwa bora zaidi kwa malezi ya watoto wetu. Inawezekana.
 
Tunashukuru. Keep up the good work lakini mimi Ustawi wa Jamii walinisumbua sana kwa zaidi ya miezi mitano ukiwatafuta wanakwambia wako busy ( kwa hao niliokutana nao ) . Ilibidi nitoe bakhshish
 
Hii kauli ""inawezekana ""hii huwa inanishekesha semeni"" yatapungua ""

Mabazazi hawawezi kuisha katu huo ndo ukweli labda watu waanze kujikomboa kifkra wenyewe wajue hili baya au zuri unless otherwise mabazazi wataendelea kuwepo
 
Tunashukuru. Keep up the good work lakini mimi Ustawi wa Jamii walinisumbua sana kwa zaidi ya miezi mitano ukiwatafuta wanakwambia wako busy ( kwa hao niliokutana nao ) . Ilibidi nitoe bakhshish
Pole sana kwa madhila hayo yaliyokukuta. Tafadhali, tuzidi kuhimizana katika kufanya kila namna ya kuhakikisha tunawalinda watoto
 
Hii kauli ""inawezekana ""hii huwa inanishekesha semeni"" yatapungua ""

Mabazazi hawawezi kuisha katu huo ndo ukweli labda watu waanze kujikomboa kifkra wenyewe wajue hili baya au zuri unless otherwise mabazazi wataendelea kuwepo
Habari mkuu. Sisi na wewe tukiwa wamoja kauli ya inawezekana hugeuka kuwa kitendo.
 
Wanaume pia mnawarudishia watoto wao waliotimiza umri wa kukaa na wazazi wao wa kiume? (Katika ndoa za waliotengana)
 
Back
Top Bottom