Francis12
JF-Expert Member
- Sep 30, 2016
- 7,533
- 22,278
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye, leo Jumanne, Machi 21, 2017, atakuwa na Mkutano na Waandishi wa Habari, Saa 7 mchana katika Ukumbi wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA). Atatoa msimamo wa Wizara ya Habari kuhusu kadhia ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, baada ya kuvamia ofisi za Clouds Media.
Jana asubuhi Waziri Nape aliunda Kamati ya watu watano ikiongozwa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo ambaye pia ndiye Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas, ili kuchunguza tukio alilolifanya Makonda kabla ya kutoa tamko rasmi la Wizara anayoiongoza.
==========
UPDATES:
Tunasubiri wahusika kufika ukumbini baada ya kufika tutawataarifu muendelee kuwa na subira.
Mpaka muda huu 13.28 wahusika hajawafika ukumbini.
Taarifa kutoka kwa Waziri wa Habari na Michezo Nape Nnauye.
"Kuna simu nyingi juu ya ripoti. Nawaomba tutulie Kamati wanamalizia kazi yao, ikikamilika tutataarifiwa muda na mahali nitakapokabidhiwa!" - Nape Nnauye