Yaliyojiri: Mkutano wa Mgombea wa CCM, Dr. Magufuli jimboni Kahama - Septemba 25, 2015

Dah, magufuli ametokea over the top karuka kioo cha mbele ka biringita.. Dah , noma.
 
Msukuma anazungumza kwa sasa anasema Mzee Lowassa ni mgonjwa.,yeye ni shahidi amezunguka nae ndege moja kwa zaidi ya Mwezi mmoja na alithibitisha kuwa Mzee Lowassa ni Mgonjwa.

Pia Msukuma amedai kuwa Mgeja alikuwa ni Mwenyekiti anayeongoza kwa Kulala katika vikao..na kwamba ameshukuru kuwa Mzigo huo umeondoka CCM..

Lakini amedai kuwa Sumaye ndie aliyeuza Mgodi wa Kahama mwaka 1998 akiwa Waziri Mkuu inakuwaje leo aseme amekuja kuwakomboa..watu ambao amewadhulumu...
 
Tatizo kubwa la msingi kwa Ukawa lilianzia wakati wa kumsimamisha mgombea urais. Ukawa badala ya kumsimamisha mtu wao, mfano anayefahamu vizuri cdm, sera zake na malengo yake ; au anayefahamu NCCR, CUF au NLD, wakamchukua mtu aliyetoka CCM. Hili limewaletea shaka kubwa wale wanaotamani mabadiliko.

Lakini ndani ya vyama hivi kuna watu wamevitumikia kwa uaminifu mkubwa. Wengine wamepigwa na kuumizwa wakitetea sera za vyama hivi. Baadhi wamefungwa na kuishi maisha magumu wakitetea vyama hivi. Walikubali kuumia hivyo wakilenga mabadiliko.Hawakutegemea mabadiliko hayo yangeletwa na watu kutoka nje ya vyama vyao hasa CCM.

Hakuna mwenye chuki binafsi na mgombea wa CDM aliyetoka CCM. Kama tulivyosema mwanzoni hatufanyi kampeni za CCM wala Magufuli, bali ni kampeni za taifa letu, hivyo tunasema wazi kwamba si kutangaza chuki binafsi na mgombea huyo, hapana.

Mgombea huyo, Lowasa ni ndugu yetu, mjomba wetu, rafiki yetu na Mtanzania mwenzetu.Tunachoamini ni kwamba Lowasa ni aina ya watu wanaosema hapana wakimaanisha ndiyo na kusema ndiyo wakimaanisha hapana. Ni aina ya watu wanaolia wakati wa kucheka na kucheka wakati wa kulia.

Kama Lowasa angeamua mapema yaani hata kabla ya mchakato wa CCM wa kumtafuta mgombea wake wa urais, akaamua kujiunga na vyama vya upinzani, wengi wetu tungeelewa na wala tusingekuwa na kelele hizi. Tatizo hapa na ambalo ni tatizo hadi siku ya uchaguzi ni EL aliingia upinzani pale jina lake lilipokatwa.

Maana yake hakuingia upinzani kutafuta mabadiliko, aliingia upinzani kupata urais. Kama jina lake lingebaki CCM bila kukatwa mtu huyu angekuwa kidedea upande wa CCM, huku ni kulia wakati wa kucheka.

Hata huko nyuma, aligombea ikashindikana. Na nia hii ambayo sio mbaya amekua nayo maisha yote. Si vibaya, maana kila mtu kuna anachokitamani. Yeye anautamani urais. Lakini kwa vile na sisi tumekuwa tukitamani mabadiliko, na tukiamini mabadiliko haya yataletwa na wapinzani sasa tumekata tamaa na kuona usaliti huu wa kutuletea mtu ambaye hawezi kusimamia mabadiliko tuliyotamani.


Ndio maana tunashawishika na Dr Magufuli ambaye yupo kwenye chama chake na huko nyuma hakuonesha uchu wa madaraka. Tunakumbuka uchaguzi wa 2005 alipoulizwa kuhusu kugombea urais, alisema yeye kazi yake kujenga barabara na madaraja. Mwaka huu hatufahamu vizuri ni nani aliyemshawishi kugombea maana tuliona hakuwa na nguvu kubwa. Hakutumia fedha nyingi wala hakuwa na mikakati mikubwa kama wagombea wengine.

Magufuli akisema hapana ni hapana na ndiyo ni ndiyo....ni msimamizi mzuri wa sheria . Akicheka
amecheka akilia amelia.

Tunataka mabadiliko si ya kufoji.....
AliUNuk6hqSNWTZH7EEO_P_00a0fVFcr5nh9LKrTI1TI.jpg
 
Sasa ni zamu ya Mzee Sitta, ambae ni mlezi wa Mkoa wa Shinyanga/.

>>> Anaelezea kuhusu Lembeli kuwa ni mtu anayesujudia wezi na matapeli kama Lowassa..

>>> CCM inawasimamia Watanzania wa kawaida, wanyonge wa nchi hii na sio walanguzi na wanaotumia madaraka kujitajirisha.

>>> Amesema kuwa Dr Magufuli anazungumzia kuhusu Ilani zinazotekelezeka na zinazoeleweka..

>>> Amesema anamjua Lowassa tangu akiwa kijana, ni mtafutaji na mjanja mjanja mwenye historia ya kudokoa tangu utotoni..
 
Ndugu zangu kwa mara ya kwanza nimeangalia mkutano wa Magufuri Kahama kupitia luninga nikiwa nasubiri usafiri. Wakuu mikutano ya Magufuri msidanganyike hata kidogo ni Fiesta tupu ya bure. Hata aibu hawana kabisa hawa watu!!!!
 
Bulembo amesema kuwa Lembeli amekimbia Ushetu baada ya kushindwa kutimiza ahadi zake kwa wananchi..amekimbilia Kahama mjini akidhani kuwa wananchi wa Kahama hawamjui..
 
Magufuli ameshatembelea Vijiji 2512 mpaka sasa..,na wanafanya mikutano ya ndani na nje zaidi ya 30 kwa siku, anashangaa UKAWA wanaweza kushindaje..?
 
Sasa ni zamu ya Mzee Sitta, ambae ni mlezi wa Mkoa wa Shinyanga/.

>>> Anaelezea kuhusu Lembeli kuwa ni mtu anayesujudia wezi na matapeli kama Lowassa..

>>> CCM inawasimamia Watanzania wa kawaida, wanyonge wa nchi hii na sio walanguzi na wanaotumia madaraka kujitajirisha.

>>> Amesema kuwa Dr Magufuli anazungumzia kuhusu Ilani zinazotekelezeka na zinazoeleweka..

>>> Amesema anamjua Lowassa tangu akiwa kijana, ni mtafutaji na mjanja mjanja mwenye historia ya kudokoa tangu utotoni..
AlxLY6gGWzNvL7zMGTGVy2zn6y4vG385i1_nhiCzZ983.jpg
 
UPDATES
Bulembo: Tunapita kila kijiji tukiomba kura, tunaamini tutashinda kia mwananchi anapata nafasi ya kusikia sera zetu
 
Duh. Hii hatari!

Magufuriko yako Kahama!

Nilimpinga Lowassa wakati akiwa ndani ya CCM na ninaendelea kumpinga hata akiwa nje ya CCM.

Lowassa hafai kuwa Rais wa Tanzania
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom