Yaliyojiri Mkutano wa Chadema Igunga

Yaliyojiri Mkutano wa Chadema Igunga

kibogo

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2012
Posts
9,739
Reaction score
4,746
Jana kumefanyika mkutano Mkubwa wa Chadema Ulioongozwa na Makamanda wa CDM Igunga wakiongozwa na Mwl. Kashindye pia walikuwepo Diwani Vicent Kamanga, Ndg Anuary, Katibu pamoja na Mwenyekiti wa CDM Wilaya ndg, Hamis Majimoto. Ikumbukwe fitina na hila nyingi zilitumika kukwamisha Mkutano huo ikiwepo na ile ya kukataza kutumika kwa eneo la sokoine ambalo ni maalaum kwa mikutano iwe ya kisiasa au Kidini.
Lengo la mkutano huu lilikuwa ni
1. Kuwatoa wasiwasi wananchi na wapenzi wa CDM juu ya tuhuma ambazo zilikuwa zimeenea kwamba Mwl. Kashindye, viongozi wa CDM wilaya na mkoa na mawakili waliohusika na kesi kwamba wamekula Rushwa hadi kusababisha ile hukumu iliyomrudishia Kafumu Ubunge wake.

2.Kuwaelezea wananchi utendaji wa DC ambao umejionyesha dhahili juu ya kukitumika chama zaidi kuliko lengo la cheo hicho ambalo ni kushirikiana na wananchi katika kuleta maendeleo ya Igunga bila ubaguzi wa Kiitikadi ambacho kwake imekuwa ni tofauti.

3. Kupima uwezo wa Chama katika ngazi ya Wilaya kwani mkutano huu uliitishwa na wanaCDM wa igunga na hakukuwa na mgeni yeyote kutoka nje kama ilivyozoeleka

4. Kumpokea Mwanachama kutoka CUF Ndg Anthon ambaye alikuwa ni Kampeni Manager wa Mgombea wa Ubunge kupitia CUF Ndg Mahona ambaye jana alivaa gwanda Rasmi na kujiunga na makamanda.


1.JPG 2.JPG 3.JPG 4.JPG

5.JPG
Mwl. Kashindye akihutubia wananchi.






 
Jambo la maana sana na huo mwitikio umeonyesha kwamba kwa kweli wapo pamoja
 
kibongo hongera kwa kutoa taarifa bila kuongezea bidhaa maarufu kutoka katika kile kiwanda chenu
 
Last edited by a moderator:
ni hatua nzuri sio ukishinda tu unafanya mkutano, hata ukishindwa kesi pia
 
Thanx kamanda kwa habari za ukombozi kutoka hapo Igunga; By ze way hizo siyo habari njema hata kidogo kwa vijana wa Lumumba.

Tafsiri ya picha inadhihirisha wazi Mwl. Kashindye ndiye Mbunge wa Igunga, whilst Peter Dalali Kafumu ni Mbunge wa CCM.

Ushauri wangu kwa Mwl. Kashindye asikate tamaa, tutamkabidhi jimbo lake ifikapo 2015 asubuhi na mapema.
 
yaani hii ni bila makamanda wa juu bila hata kubeba watu kwa maroli na hii ni baada ya kushindishwa kwa hila...tutashinda au hapata tawalika
 
WAALIMU KASHINDYE NA DOKTA MKUMBO TUNATAMBUA JUHUDI ZENU MAJIMBONI KWENU NA KUJIJENGEA MASHINA IMARA YA WAPIGA KURA

Mwalimu Kashindye tumetambua kazi yako pevu hapo Igunga; kasi iongezeke maradufu kwa kuunda timu mahiri kwa kila kata hapo jimboni.

Kila mtu amtazame Dr Kitila Mkumbo na staili yake ya kisayansi zaidi kule jimboni kwake Iramba na jinsi gani alivyojiweka karibu zaidi na wapiga kura kama utitiri kote mashinani.











 
yaani hii ni bila makamanda wa juu bila hata kubeba watu kwa maroli na hii ni baada ya kushindishwa kwa hila...tutashinda au hapata tawalika
Kitaeleweka 2015, Kafumu anajua harudi.
 
Vizuri mmeondoa uvumi huo. 2015 is not far...chamsingi kupiga na kulinda kura.
 
Nimependa sana malengo ya kuitisha mkutano huo wa hadhara huko Igunga,nadhani malengo yametimia,na kinachotakiwa sasa ni kufanya juhudi hizo,mwitikio huo wa wananchi wa Igunga uwe sustainable mpaka 2015 nakuendelea
 
kweli makamanda wa cdm mnapiga kazi natumaini mwaka 2015 itakuwa kazi rahisi sana
 
Back
Top Bottom