Yaliyojiri mahakamani Mnyika vs Hawa Nghumbi case

Lua

JF-Expert Member
May 19, 2011
704
305
Ilianza hivi

1..DAI LA KWANZA KURA 14854 HAZIJULIKANI ZILIKOTOKEA WAKATI WA MAJUMUISHO
Wakili upande wa mlalamikaji; siku ya kutangaza matokeo ulikuwepo?
Hawa: Sikuwepo
Wakili: kwanini hukuwepo kwenye kituo cha majumuisho?
Hawa: wakala wangu alikuwepo
Wakili: je ulisaini form ya matokeo
Hawa: Sikusain
Wakil: inatakiwa kama hujasaini ujaze form je ulisain?
Hawa: Wakala wangu hakupewa
Wakili: Aliomba?
Hawa: Hakuomba
Wakili: Je unafaham tofauti ya kura zako ulizopata na za mh Mnyika ni ngapi baada ya matokeo kutangazwa?
Hawa: ndio nafaham
Wakili: ni ngapi?
Hawa: 16198
(kwa maana mnyika alipata kura 66742 na Hawa kura 50544)

Wakili: madai yako kuwa kuna kura 14854 ambazo kwenye majumuisho hazieleweki zilikotokea....je unadhan kama ukipewa kura zote na kuassume ni zakwako je zitabadili matokeo?
Hawa: Hazitabadilisha matokeo
Wakili; kama hazibadili sasa madai yako makubwa hasa ni nini?
Hawa: Madai yangu ni ukiukwaji wa utaratibu wa majumuisho
Wakili: Mh.Mnyika anahusika vipi na huo utaratibu?
Hawa; sijui
Wakili: je,,matokeo yaliyoko kwenye form namba 21 ambayo ni ya matokeo ya jumla ya kwenye vituo yanayoonyesha ulipata kura 50544 unamashaka nayo?
Hawa:Sina mashaka nayo
Wakili:Kama huna mashaka nayo basi hakuna tatizo kwenye ushindi wa Mh.Mnyika
Hawa:sikulalamikia ushindi bali utaratibu
Wakili:Kama ndivyo basi inaonyesha huna imani na tume ya uchaguzi?
Hawa:ninaiman nayo
Wakili:Je Unakumbuka siku ya kuhesabu kura mkurugenzi wa uchaguzi kutoka tume Kiravu alikuwepo?
Hawa:ndio alikuwepo
Wakili:we huoni kama mlikuwa mna bahati ya pekee kuwa na mkurugenzi kwenye kituo chenu cha kuhesabia kura?
Hawa:ndio ni bahati kubwa
Wakili:sasa iweje wewe huna imani na utaratibu uliotumika?
Hawa:kwa kweli hata mm hapo sielewi
2..DAI LA PILI:MALALAMIKO YA VITUO KUWA UAINISHAJI WA KURA KWENYE FOM HAUELEWEKI
Wakili:
je ni vituo vingapi unavyovilalamikia?
Hawa:sijui wakala ndiye aliyeniambia mm sikuwepo
Wakili;Kwenye madai ya awali (Amended Petition) ulisema na ukasaini kuwa ulishuhudia wewe mwennyewe na unajua,,sasa iweje hapa mahakaman unakataa?
Hawa;Sina uhakika kama nilisema hivyo
Wakili;Je..Kingereza unakijua?
Hawa;Najua lakini cha kuokoteza
Wakili:Angalia hii (anampatia Amended petition ya madai yake)
Hawa;(Anaangalia )
Wakili:Je haya madai yaliyoandikwa humu na wakili wako na kusainiwa na wewe unayatambua?
Hawa:Ndio nayatambua
Wakili;sasa mbona unapinga hapa mahakaman kuwa anayejua kila kitu ni wakala ilihali wewe umesaini huu waraka?
Hawa:ni kutojua sheria tu.
3..DAI LA TATU :KUKASHIFIWA KWENYE MKUTANO WA TAREHE 11/09/2010 KUWA AMEUZA NYUMBA YA UWT
Wakili:je wakati huo Mh.Mnyika anakukashfu ulikuwepo?
Hawa:hapana sikuwepo ila niliambiwa na shahidi wa pili ambaye ni Robert Bondera
Wakili:baada ya kuambiwa ulichukua hatua gani?
Hawa:sikuchukua hatua yeyote na ndio maana nikaileta huku mahakamani
Wakili;je unazijua form za maadili?
Hawa:ndio nazijua
Wakili:je,ulijaza form na kusaini?
Hawa:ndio
Wakili:form zinaelekeza kama mgombea akikashifiwa wakati wa kampeni anatakiwa aandike malalamiko kwa mwenyekiti wa uchaguzi wa jimbo ambaye ni mkurugenzi .Je ulifanya hivyo?
Hawa:sikufanya
Wakili:je tarehe 30/07/2010 ulihojiwa na TAKUKURU kuhusu tuhuma za rushwa na jalada halijafungwa.ni kweli?
Hawa:ahaaa nilihojiwa ,,ni kweli lakini sikuwa na ufaham wa kukumbuka kama limefungwa au bado.
Wakili:wakati wa kipindi cha mijadala ya mchakato majimboni kuna mwananchi alikuuliza juu ya wewe kuhusika na uuzaji wa nyumba ya UWT..Ni kweli?
Hawa:Ndio ni kweli
Wakili;Ulisema utamshtaki,,je ulifanya hivyo?
Hawa;sikufanya hivyo
Wakili:kwa nn hukumshtaki ilihali ulishatangaza hadharani?
Hawa:nilipuuzia kwasababu haikuwa kweli
Wakili:kutokumshtaki kwako huoni kama kuna ukweli ndani yake?
Hawa:si kweli ..mm ndiye ninayesema
Wakili:wakati wa kampen mlikuwa mnaongozwa na nn?
Hawa:Na ratiba ya kampeni za nje
Wakili:je wakati mnapobadili ratiba ya mkutano mnetumia njia gani ya maandishi au simu?
Hawa;Maandishi
Wakili;Unaijua ratiba ya tume kama ukionyeshwa.
Hawa:ndio
Wakili(anampa na kumwambia asome tarehe hiyo 11/09/2010 ambayo anadai kukashifiwa kwenye mkutano Riverside)
Je,,kwenye hii ratiba inaonyesha chadema walikuwa na mkutano sehemu gani?
Hawa:haionyeshi kama walikuwa na mkutano
Wakili:sasa haya madai ya kukashifiwa tarehe hiyo uliyapata wapi wakati umekiri kuwa hawakuwa na mkutano kwa mujibu wa ratiba ya tume ya uchaguzi
Hawa:niliambiwa na shahidi wangu
Wakili:basi shahidi atatuhakikishia ukweli atakapokuja
HAKIMU
Wakili:
umesema wakati mnyika anatangaza nia ya kugombea alimkashfu Hawa,,je haya maneno ni sahihi?
shahidi:ndio ni kweli

W

 
Kesi nyingine ni waste of resources and time. Mahakama inalalamika haina fedha za kundesha kesi za uchaguzi, kumbe kesi zenyewe ndio hizi? Ndio majibu ambayo wapiga kura wangejibiwa kama wangemchagua kuwa mbunge wao. I wonder how many of these sort of people we have in Parliament.
 
kesi imehairishwa hadi tarehe 26/03/2012 saa tatu asubuhi, mahakama ya kazi iliyopo maeneo ya akiba, (nssf zamani).
 
Sasa huyu anatafuta nini kwa watanzania!! hivi angekapata uwakilishi ingelikuwajje? au ndiyo haya majitu yakupandikizwa!!naona hana kazi ya kufanya, mwambieni akashtaki kwa wassira!!!
 
Kweli hawa jamaa wameamua kuzorotesha uchumi wetu!Hizo hela angepeleka vikoba jamani!Labda 2015 angepata jimbo(sio ubungo lakini,huku ameshaharibu kabisaaaaaaaaa)!
 
Huyu mama aliteuliwa DC na uteuzi wa kesho atatesa tena na wilaya mpya!Tanzaniaaa tanzaniaaaa nakupendaaa kwa moyooo woooteeeeee,,,,,,angekuwa mbunge angepata wizara ya sheria na katiba,,,,
 
Kesi nyingi za uchaguzi za CCM vs Upinzani zilifunguliwa kwa maagizo ya Makamba. Sasa wagombea ambao hawana weledi wa kutosha waliingia kichwa kichwa wao wenyewe wakashitaki na wale wenye weledi kama akina Dr. Burian waliwatumia wapiga kura wao ili kuepuka aibu.

Mwenendo wa hii kesi unamuweka kwenye spotlight huyo mama, come 2015 wapiga kura wengi watakuwa wanamfahamu kwamba hana weledi na hivyo hata kwenye kura za maoni hawezi kupita.

Dr. Burian amesita kwenda kutoa ushahidi kwa kuogopa kuwekwa kwenye kundi la akina Hawa Ng'humbi maana kwa kuwa kesi hazina kichwa wala miguu ni rahisi sana kuchanganywa hata kama Wakili wake amekesha anam-coach namna ya kujibu maswali, huwezi kujua Wakili wa Utetezi amejiandaa na maswali ya namna gani na ana info kiasi gani kuhusiana na mshitakiwa na mashihidi wake.

Matatizo ya Chama Tawala kukubali kuongozwa na watu wenye weledi mdogo, wanaishia kutumia nguvu zaidi kuliko busara wakitarajia kwamba serikali itawalinda au mahakama itawapendelea hata kama wakienda kuchemsha kwenye kesi.
 
Ni heri wanaubungo mlimnyima ubunge,angeshinda ingekuwa matatizo matupu, maana ingekuwa kuzomea na kupiga meza kwa vitu asivyovijua.
Mungu tusaidie wengine walio kama huyu huko mjengoni ni janga la kitaifa.
 
Siamini kama kweli uyu Mama ndiye angekua mbunge wangu. Sindiyo yangekuwa yaleyale ya akina ndiyo mzee!!! kweli chama tawala kazi ipo kama ndiyo design za wabunge wateule wa CCM kama izi, kwa kizazi chetu waandike 0.
 
mama yangu wewe hivi hawa watu huwa hawapewi ushauri kabla ya kufungua kesi?


Mnyika mbunge mpaka 2015 OVA

kweli kabisa wasilazimishe kututawala kwa nguvu.tulishaamua kwenye kura kazi kwao wanatafuta ushindi mezani?mbona gape ni kubwa sana wakubali tu
 
Mimi huyu mama nilikuwa namkubali sana hususani mara baada ya kuisoma CV yake kwa kweli niliamini kwamba alikuwa candidate mzuri ukimcompare na mnyika, hasa chuo alichosomea cha huko uholazi. sasa anavyosema anajua kiingereza cha kuokoteza yaani kama cha kanumba nashindwa kumwelewa vizuri, pia alikuwa afisa mwajiri wa ile kampuni yetu ya mafuta so sijui alikuwa anaajiri vipii.
 
29 Reactions
Reply
Back
Top Bottom