Yaliyojiri Ikulu: Rais Magufuli awaapisha wakuu wa mikoa, Kamishna mkuu TRA na Mkurugenzi mkuu PCCB

Mugo wa kibilo

Senior Member
Oct 13, 2012
175
72
111fvhvmhvmhbmh.JPG

Picha ya pamoja ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Wakuu wa Mikoa baada ya kuwaapisha wakuu wa Mikoa, Kamishena Mkuu wa Mamlaka ya Mapata Tanzania na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa Ikulu jijini Dar es salaam Marchi 15,2016
12VCVCC.JPG

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan pamoja na viongozi wengine katika picha ya pamoja na Kamishena Mkuu wa Mamlaka ya Mapata Tanzania Ndg. Alphayo Japani Kidata na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa Kamishna wa Polisi Valentino Longino Mlowala (waliosimama) Ikulu jijini Dar es salaam baada ya kuwaapisha Marchi 15,2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.John .P. Magufuli anawaapisha wakuu wa mikoa wateuliwa kabla ya kuanza rasmi shughuli zao za kiutendaji.

Rais Magufuli ameongelea suala la wafanyakazi hewa kwenye Halmashauri zote nchini, amewapa siku 15 wakuu wapya wa mikoa kuhakikisha hakuna wafanyakazi hewa katika Halmashauri zote nchini.

Rais Magufuli wafanyakazi hewa, vijana wafanye kazi watakao kataa wapelekwe kwenye makambi wakafanye kazi, awaagiza wakuu wa mikoa ndani ya siku 15 kuhakikisha hamna wafanyakazi hewa katika mikoa yao

Rais Magufuli amewataka wa kuu wa mikoa hao kuhakikisha hakuna vijana ambao watakuwa wanakwenda kucheza pool table asubuhi na badala yake vijana hao wanatakiwa kufanya kazi kweli kweli hata kwa kulazimishwa.

"Nimeamua kuwateua wakuu wa Mikoa nikiamini kwamba mtaniwakilisha vizuri katika mikoa yenu, Napenda niwape pole kwa sababu mtakwenda kufanya kazi kweli kweli kutatua kero za wananchi wetu.

Lakini pia niwaombe wakuu wa mikoa mkasimamie watu wafanye kazi hasa vijana haiwezekani vijana leo hii unamkuta saa mbili asubuhi anacheza Pool table wakati wa kina mama wanalima shambani, kama hawataki kufanya kazi kwa kupenda walazimishwe kufanya kazi."

Rais Magufuli: Nimeamua kuwateua nyinyi kama wakuu wa mikoa nikiamini mtaniwakilisha vizuri popote.

Rais Magufuli: Wananchi Kusindikizwa na polisi maana yake hakuna usalama.

Rais Magufuli: Na hasa kutambua nyinyi ndio wenyekiti wa kamati za ulinzi na usalama mkaniwakilishe.

Rais Magufuli: Haiwezekani kwa nchi ambayo inajitawala miaka 50 raia wake wakisafiri wasindikizwe na polisi.

Rais Magufuli: Nataka Tanzania katika awamu yangu isitokee mahali mkuu wa mkoa anaomba chakula.

Rais Magufuli: Niwape grace time ndani ya siku 15 wakurugenzi wawe wamejumlisha wamewatoa wafanyakazi hewa katika payroll

Rais Magufuli: Mshahara wa mwezi tukigundua mkurugenzi amelipa mshahara hewa ajue hana kazi na tunampeleka mahakamani

Rais Magufuli: Singida na Dodoma ina wafanyakazi hewa 202

Rais Magufuli: Leo pia tumeapisha Kamishna mkuu wa TRA na kamanda wa TAKUKURU.

Rais Magufuli: Nyinyi mna mamlaka ya kuwaweka watu ndani hata masaa 48, kawawekeni wengi ili kusudi wajue kwamba wananchi wanatakiwa kuheshimiwa.

Rais Magufuli: Tusiogope kuchukua maamuzi, nafuu uchukue maamuzi hata kama ni mabaya yatarekebika huko mbele.

Rais Magufuli: Haiwezekani kila siku majambazi, kwa nini Rwanda hakuna majambazi, kwa nini Tanzania tu, mkafanye kazi.

Magufuli: Morogoro watu wanauana sana ndio maana sikuona sababu ya mkuu wa mkoa kubaki pale. 'Mesage sent and delivered'.

 
Mkono kitala kitabakia kiiunoni ... lakini kumbuka Zelothe na wakina meja Gen. Kijuhu wameshastaafu kwa hiyo. Pale watakua.kiraia tu... lakini kama wangekua inservice ndo angepiga salute ya mkono wakat kitala kipo kiunoni
 
Mkono kitala kitabakia kiiunoni ... lakini kumbuka Zelothe na wakina meja Gen. Kijuhu wameshastaafu kwahyo.pale watakua.kiraia tu... lakin kama wangekua inservice ndo angepiga salute ya mkono wakat kitala kipo kiunon
Wamevaa uniform mkuu wote,sasa nimeshangaa sana kuona Zelothe ana kitala lakin bado kapiga salute kwa mkono
 
Hii thread mtakomenti maafwande tu wengine tutakua tunachukua maujuzi tukasimuliane vijiweni kwetu...
 
Wamevaa uniform mkuu wote,sasa nimeshangaa sana kuona Zelothe ana kitala lakin bado kapiga salute kwa mkono
Kuanzia hadhi ya Deputy commissioner na jeshi ngazi ya canal salamu ya heshima kwa mkuu ni ya mkono halafu.kitara ni sehemu ya heshima kwa gwaride sio kama unakitala ndo utoe salam kwa kitala... ukiona harusi au gwaride la heshima ndio hutumika maana unakua na kombania ya watu wengi
 
Kuanzia hadhi ya Deputy commissioner na jeshi ngazi ya canal salamu ya heshima kwa mkuu ni ya mkono halafu.kitara ni sehemu ya heshima kwa gwaride sio kama unakitala ndo utoe salam kwa kitala... ukiona harusi au gwaride la heshima ndio hutumika maana unakua na kombania ya watu wengi
Nimekusoma mkuu nashukuru kwa ufafanuzi
 
Rais Magufuli ana kauli za kibabe aisee, ila kaongea suala la msingi sana kuhusu ujambazi mikoa ya Kagera na Geita. Sisi wasafiri wa njia hiyo tunapata tabu sana na majambazi, ukipita lile pori roho inakuwa juu juu maana hujui kama utavuka salama.

Asante sana kwa kutupelekea mkuu wa mkoa Mjeda.
 
Mkono kitala kitabakia kiiunoni ... lakini kumbuka Zelothe na wakina meja Gen. Kijuhu wameshastaafu kwahyo.pale watakua.kiraia tu... lakin kama wangekua inservice ndo angepiga salute ya mkono wakat kitala kipo kiunon

Katika mambo ya kijeshi mavazi sio cheo Bali mtu au muhusika na heshima aliyokuwa mayo ndio silaha yake ndio maana mh pombe alivyovaa kijeshi bado alipewa heshima kama amiri jeshi mkuu hivyo ni halali kwa wanajeshi wastaafu kupiga saluti halafu ni jambo la kiheshima sana
 
Nimeshuhudia uapishaji wa wakuu wa mikoa wapya, nimeona sura za ukakamavu upole roho ngumu lakini pia za mashaka
Wakuu hawa wameteuliwa kutokana na Changamoto za mikoa wanayoenda kutumikia
Tanga kama kawaida ina bahati mbaya mara zote na Changamoto kubwa ikiwa ni elimu.. Shigela kapewa Tanga ila tuko dhoofu sijui ninini kinamsumbua tunamuombea
Shigela ndugu yangu unaenda Tanga jiandae kule nyumba mchawi/mganga, nyumba bwanyenye/mwinyi nyumba basha! Karibu Tanga
 
Nimecheka sana watu hawajui ata kitala ila nikweli kama hujawahi pita huko sasa basi kama mme wahi ona gwaride mtu anae ongoza gwaride huwa anakuwa na kitu amekishika kama jambia hiv kile ndio kitala kama mtu hajaelewa ntakuja baadae kwa ufafanuzi.
 
Nimecheka sana watu hawajui ata kitala ila nikweli kama hujawahi pita huko sasa basi kama mme wahi ona gwaride mtu anae ongoza gwaride huwa anakuwa na kitu amekishika kama jambia hiv kile ndio kitala kama mtu hajaelewa ntakuja baadae kwa ufafanuzi.

Mimi nilipita lakini ni kwa mujibu wa sheria JKT ,lakini sikufundishwa kitala,na wala sikucheza yale magwaride ya kuadhimisha sherehe za uhuru.
 
Rais ameyasema hayo wakati wa kuwapishwa kwa Wakuu wapya wa mkoa.
Rais amewaagiza Wakuu hao wapya kwenda kuhakikisha tatizo la watumishi hewa katika Halmashauri zote nchini linatatuliwa. Aidha amewataka kwenda kuhakikisha migogoro ya wakulima na wafugaji inamalizika, kuhakikisha usalama wa wananchi katika mikoa yao bila kusahau kuwachukulia hatua viongozi ambao wataonekana kuwanyanyasa wananchi wasio na makosa. Zaidi amewataka Wakuu hao wa Mikoa kuhakikisha wanasimamia watu wafanye kasi badala ya kujihusisha na mambo ambayo siyo ya uzalishaji kama vile vijana kucheza pool n.k. ili kuondokana kabisa na matatizo ya uhaba wa chakula katika mikoa yao
 
Back
Top Bottom