NJELA HELA
Member
- Oct 19, 2012
- 10
- 2
Wana Jf.
Karibuni tujadili hili swala pamoja.
Namshukuru M/mungu kwa kunipa pumzi hadi leo hii nikiandika hili andishi. Pia nitakuwa sitatenda haki kama nisipomshukuru kwa kunipa utashi, akili, haiba hata uwezo wa kutambua jema na baya. Ni ukweli uliothibiti kuwa wako wengi sana wamezikosa neema hizi ambazo mimi niko nazo. Asante M/mungu, na kila sifa njema za kustahiki wewe, Mola wa viumbe wote.
Mimi ni mgeni sana katika tasnia hii ya uandishi wa makala za uchambuzi, pia mimi si muandishi wa habari kitaaluma, yaani kijumla mimi si mwandishi. Pamoja na hayo ile haki yangu ya kutoa maoni na kusikilizwa haiwezi ikapotea kisa tu, si mwanataaluma wa uandishi. Leo naomba niitumia haki yangu hiyo ili nami nitoe yaliyojificha katika moyo wangu. Kikubwa kwa msomi wa andishi hili naomba ashughulishwe zaidi na maudhui hususani katika kipengele cha dhamira na falsafa, masuala ya fani naomba aachane nayo kwani nimeshakiri udhaifu wangu katika hilo.
Tuna uhaba mkubwa wa ajira rasmi katika nchi yetu. Maelfu ya vijana wanamaliza vyuo kila mwaka nchini, lakini wakati wakimaliza chuo, wanajikuta wanaanza chuo kingine, chuo cha kutafuta ajira. Wakati tatizo la ajira likizidi kujiongezea kasi, hali imekuwa ya kukatisha tamaa katika makampuni ya kigeni, kwani katika makampuni hayo idadi ya wafanyakazi wazawa inatuletea viulizo vingi kuliko hata majibu.
Makampuni yanayokuja kuwekeza na/au kufanya utafiti fulani hapa nchini petu yanahitaji wafanyakazi wa fani mbalimbali. Mfano katika makampuni ya utafiti wa gesi na mafuta yanauhitaji wa wafanyakazi wa fani zifutazo, Electrical, Chemical,Mechanical, Drilling, Geology,Geophysics, Catering, nk. Jambo la kushangaza katika makampuni haya idadi ya watanzania ni ndogo sana au hakuna kabisa, wakati idadi ya watanzania ikiwa ndogo au wasiwepo kwenye makampuni hayo, mtaani kuna watanzania wenye fani hizo wakitembea na vyeti vyao wakitafuta kazi.
Nilifanya utafiti wa kuangalia namna ya utoaji ajira katika kampuni fulani ya kigeni inayojishughilisha na utafiti wa mafuta na gesi. Katika kampuni hiyo hadi watu wa kufanya usafi na kupika ni wageni, yaani watanzani ni wachache mno. Na nilipojaribu kufuatilia sababu zinazowafanya waajiri wageni zaidi kuliko wazawa tena hata kwa fani ambazo wazawa wanazimudu nilipata majibu yafuatayo.
KWANZA: Kampuni hii inasema kuwa Tanzania haina wataalamu wa mafuta na gesi, na hata wale waliopo si wazoefu wa kiwango cha kukabidhiwa kazi. Hali hii ndio inayoipelekea kampuni hii iajiri wafanyakazi wengi kutoka nje ya nchi na wachache wajiriwe kutoka nchini kwa lengo la kupatiwa huo uzoefu.
Mimi naamini kuwa mtu akiwa chuoni anajua kazi pindi akienda kwanye mafunzo ya vitendo[field] na anapata uzoefu pindi akianza kazi akiwa kama afisa msaidizi na kama akikabidhiwa ukuu wa kitengo ni lazima apewe semina elekezi. Ndio kusema kuwa mfanyakazi hawezi kuwa mzoefu kwa kuwa nje ya mfumo na kuzurula mtaani kwa kutafuta kazi, bali anakuwa mzoefu kwa kupewa fursa na ajira kulingana na taaluma yake.
Pindi mtu ukitafakari kwa kina utagundua kuwa kinachotazamwa hapa si uzoefu tu, kama ni uzoefu tu, ina maana hakuna watanzania wenye taaluma na uzoefu wa kupika, kufagia, kufua kwakutumia mashine, kuosha vyombo, Roust Bout na Raghnecks na hata kusambaza vyakula kwa wafanyakazi? Hivi tunahitaji kundi kubwa la watu wa kigeni kuja kutuzoesha kazi katika taaluma tulizozisomea? Niseme kitu kimoja kwamba hawa wenzetu hawana mpango wa kutufundisha, na ndio maana hata katika nafasi ambazo wazawa wanaambiwa hawaziwezi hakuna utaratibu wa kumuweka mzawa katika nafasi hiyo ili naye apate huo uzoefu kutoka kwa mtaalamu wa kigeni.
PILI: Japokuwa hili hawaliweki wazi, lakini kampuni hzi na zingine nyingi hazihitaji mtu asiyejua kuzungumza na kuandika kiingereza kwa ufasaha, kama sivyo, ni kwanini katika usahili wa wafanyakazi watumie lugha ya kiingereza? Niko na imani kuwa hata wale wafagiaji waliopo, wako pale kwasababu wanajua kiingereza, kwakuwa watanzania hawajui ndio maana wanaonekana hawajui hata kufagia.
Suala la kiingereza limekuwa ni mwiba wa koo kwa watanzania, kwani ni jambo la kusikitisha kuwa hata kampuni za kizawa zimekuwa zikimdharau mtu asiyejua kiingereza hata kama mtu huyo anaimudu vema taaluma aliyoisomea.
Juzi wakati nikiwa kwenye daladala nilimsikia dereva wa daladala akisema kuwa amekosa ajira katika kampuni fulani kisa tu hajui kiingereza, kwani katika majaribio ya udereva alifuzu na vyeti vyake vinavyothibitisha kuwa yeye ana taaluma ya udereva alivipeleka katika kampuni hiyo. Mara baada ya kufanyiwa majaribio, akapelekwa katika chumba cha mahojiano, alifanikiwa kujibu swali moja tu, swali lilomtaka ataje jina lake, mengine yote aliishia kunyamaza tu kama bubu, na ajira akawa ameikosa.
Hiki kigezo cha kujua kiingereza kitakuwa si mwiba wa koo tu, bali kitakuwa kama roba ya mbao shingoni mwa Watanzania pindi fursa iliyotolewa na mkataba wa Jumuia ya Afrika Mashariki katika soko za ajira ikianza kutumiwa ipasavyo na Wakenya na Waganda. Uwezo wa wananchi wa nchi hizo katika kuzungumza kiingereza ni mkubwa ukilinganisha na Watanzania, Uganda hata mchuuzi wa magazeti anazungumza kiingereza, wakati huku kwa wenye digrii zao bado wengine kiingereza kwao ni mtihani. Nafikiri iko haja ya kumpima mtu kwa taaluma na uzoefu wake na si kwa lugha, la sivyo Watanzania wengi watakosa ajira kama ilivyokuwa kwa yule dereva wa daladala.
Wakati akichangia hotuba ya bajeti ya serikali ya mwaka 2012/2013 mbunge wa jimbo la Ubungo Mh. Mnyika alinukuliwa akisema kuwa Tumefika hapa kutokana na udhaifu wa rais Kikwete, kutokana na uzembe wa Bunge na upuuzi wa CCM. Japokuwa CCM na serikali wameipinga kauli hii kwa nguvu zote, lakini ukweli unabaki palepale kuwa udhaifu wa tasisi ya urais, uzembe wa Bunge na upuuzi wa CCM ndio unaosababisha kilio kwa watanzania.
Serikali inashindwa kuandaa sera nzuri ambazo zitaweza kutoa fursa pana, wazi na sawa za ajira kwa watanzania wote katika makampuni na mashirika ya kigeni yanayofanya shughuli zake humu nchini. Hata zile sera dhaifu za kulinda ajira kwa watanzania ambazo tayari zipo, serikali inashindwa kuzitekeleza na kuzisimamia ipasavyo, yaani, inakuwa kama imetungiwa, kumbe imezitunga yenyewe.
Idara ya uhamiaji ndio inayohusika na kutoa vibali vya kufanyia kazi kwa wageni wanaotaka kufanya kazi au biashara nchini. Pamoja na vigezo vingine vinavyotazamwa kabla ya kibali kutolewa kwa mgeni, inasemekana kigezo kikuu kinachoangaliwa ni kama hiyo kazi anayotaka kuifanya huyo mgeni, hakuna mtanzania mwenye uwezo wa kuifanya. Kama ni biashara, basi kuwe hakuna watanzania wanaofanya biashara anayoiomba kuifanya. Kama wapo, kutaangaliwa kuruhusiwa kwake kufanya biashara hiyo kutahathiri vipi biashara wazifanyazo watanzania.
Kutokana na udhaifu wa tasisi ya urais ndio maana idara hii inashindwa kusimamia ipasavyo taratibu za kutoa vibali vya kufanyia kazi wageni.Mlundikano wa wafagiaji, wapishi na madobi wa kigeni wanaofanya kazi katika makampuni ya utafiti wa mafuta na gesi humu nchini ni viashiria vya uzembe kwa idara ya uhamiaji. Si hivyo tu, hata wajasiriamali wa kichina wanaouza maua na bidhaa za majumbani katika mtaa wa kongo Kariakoo na mitaa ya jirani ni kiashiria pia cha uzembe na udhaifu wa serikali yetu. Nilijaribu kufuatilia kujua hawa watu wanaingia vipi nchini na kuruhusiwa kufanya kazi amabazo zinaweza kufanywa na Mtanzania, jibu nililopata ni kuwa wahausika wakuu ni watu wa uhamiaji wanakula rushwa kumrusu huyu mtu aingie, inakuaje mtu anapewa viza ya kuingia nchi kama amekuja kutembelea ndugu na jamaa cha ajabu utakumata sehemu ya kufanyia kazi tena baharini, hivi inaingia akilini kweli? Kama akipata ajali huko watu wa uhamiaji mtajibu nini? alikopatia ajali ndio kwa ndugu zake?
January Makamba natimu yake walitembelea moja ya makampuni ya utafiti wa gesi na mafuta mwishoni mwa mwaka juzi, kipindi hicho alikuwa ni mwenyekiti wa kamati ya bunge ya nishati na madini. Uchache wa watanzania katika kampuni ile aliuona, na suala la wageni kufanya kazi zinazowezwa kufanya na wazawa aliliona. Na hakuishia kuona kwa macho yake, bali pia aliambiwa kila kitu na na baadhi ya watanzania wanaofanya kazi katika kampuni ile.
Kama mjuavyo, bunge letu ni zembe, je litawezaje kuwa na kamati imara yenye uwezo wa kuisimamia serikali ipasavyo? Kichogo mchawi, alichokifanya Makamba mara baada ya kuondoka wafanyakazi wazawa hawakukijua, walichojua wao ni ahadi ya kushughulikiwa hilo tatizo, lakini hadi leo hakuna kilichofanyika ingawa huyu kijana mwenzetu kazibwa mdomo kwa kusogezwa jikoni.
Niko na shaka na uimara wa rais wetu, kwani alipokuwa akiomba ridhaa kwetu ya kuongoza nchi hii alituahidi mamilioni ya ajira. Sasa kwa hili jambo la Watanzania kukosa ajira na wageni kupata ajira si kiashiria cha udhaifu wa rais? Hivi inamaana ameshasaahu kilichotokea Afrika Kusini kwa wageni kuuawa na wazawa kwasabu ya ajira kuchukuliwa na wageni? Je, amejipanga kutudhibiti vipi sisi wanachi wake endapo tukianza kupita kila ofisi na kuanza kuwatimua wageni? Naomba tusifike huko, bali ni vema serikali ikatatua tatizo hili. Angola, Gabon na nchi zingine ambazo zinamakampuni mengi ya utafiti wa mafuta na gesi wameweka mbele kipaumbele kwa wananchi wake kupewa ajira na si mtu waakutoka nje, hata kama hajui lazima mzawa apewe ajila huku akipata mafunzo kipindi yupo kazini, iweje sisi serikali yetu ishindwe kulisimamia hilo?
Tatizo linaloikaibili nchi yetu ni mfumo mbovu wa mihimili yetu inayounda dola, ubovu wa mifumo hii inasababishwa na ubovu wa katiba. Katiba yetu imetoa madraka makubwa kwa serikali kuliko kwa mihimili mingine ya dola, yaani, bunge na mahakama. Na ndio maana rais anaweza kuingilia kazi za bunge na mahaakama na hakuna yeyote wa kumuhoji. Tunahitaji katiba mpya itakayokuja na majibu ya kero za kimfumo. Kwa kufanya hivyo ndio tutaweza kubadili uongozi legelege na kuleta uongozi imara, kinyume chake itakuwa ndoto kuitoa CCM madarakani, chama ambacho kimeshindwa kuwapatia ajira vijana wa kitanzania.
Mwisho na kwa umuhimu wa pekee napenda kuwashuru wote waliosoma andishi hili, nakaribisha ushauri, mawazo na maoni yenye lengo la kutujenga kama vijana wa kitanzania, vijana ambao kila mwaka mamia kwa makumi elfu wanamaliza elimu zao katika vyuo mbalimbali, wanamwagwa katika soko lajira lenye ufinyu wa bidhaa hiyo iitwayo ajira.
Naomba kuwasilisha.