Yako wapi matendo mema ya serikali ya ccm? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Yako wapi matendo mema ya serikali ya ccm?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mendelian Inheritanc, Jan 9, 2012.

 1. M

  Mendelian Inheritanc Member

  #1
  Jan 9, 2012
  Joined: Dec 25, 2011
  Messages: 86
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  YAKO WAPI MATENDO MEMA YA SERIKALI YA CCM?
  Nianze kwa kuwakumbusha watanzania wenzangu kwamba uhalali wa Serikali yoyote ya kidemokrasia kuendelea kukaa madarakani haitokani tu na katiba na sheria iliyoiweka madarakani, bali zaidi hutokana na ridhaa ya wananchi kuendelea kutawaliwa au kuongozwa nayo. Aidha, ridhaa hiyo hutokana na matendo mema ya Serikali hiyo kwa raia wake.
  Hii ni muhimu sana kwa kila mtanzania aliye makini, watanzania tujiulize;

  · Yako wapi matendo mema ya Serikali ya CCM kwa wanafunzi wa vyuo vikuu, madaktari na wananchi maskini pale Muhimbili?

  · Yako wapi matendo mema ya Serikali ya CCM kwa wafanyakazi 350,000 wanaodai mishahara na maslahi yao mengine, wakati Serikali ya CCM inawatisha na kuwafukuza wanapodai haki zao za msingi?

  · Yako wapi matendo mema ya Serikali ya CCM kwa vijana vyuoni tunaodai mahitaji ya msingi ya kielimu, wakati tunashuhudia vijana wakinyanyasika kwa mikopo yenye kubagua mpaka tugome ndio mikopo itoke?

  · Yako wapi matendo mema ya serikali ya CCM kwa wastaafu waliolitumikia taifa hili kwa uadilifu, wakati tunashuhudia mateso makubwa kwa wastaafu wazee wetu wakidhalilika mitaani kwa maji ya kuwasha wanapodai madai yao ya msingi?

  · Yako wapi matendo mema ya Serikali ya CCM kwa walimu, wakati tunashuhudia walimu mpaka wagome ndipo wasikilizwe, naambiwa hata walimu waliomaliza vyuo vikuu mwaka jana mpaka leo post zao hazijatoka,kisa serikali haina hela ila ila inaposho za wabunge tu.

  · Yako wapi matendo mema kwa wafugaji, wakati tunashuhudia wafugaji wakinyanyasika kama wao si raia wa nchi hii.

  · Yako wapi matendo mema kwa wauguzi, polisi na wananchi wanaoishi karibu na migodi yenye utajiri mwingi, wakati tunashuhudia wakiishi maisha duni?

  · Yako wapi matendo mema kwa watoto wakike wanaoteseka kwa kupata mimba wakati tunashuhudia viongozi wa CCM wakiwakebehi kwamba wanaponzwa na viherehere vyao, badala ya kuwapa mazingira bora ya elimu?

  · Yako wapi matendo mema ya Serikali ya CCM kwa watanzania waishio kigamboni wakati tunashuhudia viongozi wa CCM wakiwakebehi kwamba kama hawana 200 za kivuko wapige mbizi, wazunguke kongowe au warudi mikoani wakalime?

  Ø Katika miaka Zaidi Ya 35 Ya Serikali ya CCM, ni bayana kwamba kwa kiasi kikubwa kumekuwepo upungufu mkubwa wa matendo mema kwa raia wake, Hivyo CCM haina ridhaa ya kuendelea kuongoza nchi hii, Nawaomba watanzania wa rika zote kama kuna matendo mema CCM iliyowatendea mniwekee hapa, na kama hakuna nawaomba 2015 mchague mabadiliko. Huu ni mtazamo wangu wakuu msijenge chuki ila naomba kama yapo matendo mema Ya Serikali ya CCM mnipe, Yako wapiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii nipeni?
   
 2. M

  Mendelian Inheritanc Member

  #2
  Jan 9, 2012
  Joined: Dec 25, 2011
  Messages: 86
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama yapo matendo mema nitamsikiliza jk akiongea
   
 3. montroll

  montroll JF-Expert Member

  #3
  Jan 9, 2012
  Joined: Jul 31, 2011
  Messages: 288
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  kuhakikisha vigogo woe na watoto na wajukuu wao wanaishi tanzania kama peponi ! kwao hao tatizo ni kuchagua tu, asome chuo au shule ipi,katika nchi ipi, afanye kazi wapi,,,,,,

  nasinzia, kama vipi potezea ila nilikuwa naota kuwa tafsiri ya neno wananchi kwa ccm ya baada ya nyerere na azimio la znz, ni familia viongozi na familia na marafiki zao!
  Maisha bora kwa kila mwanachi wao,,,,,

  ngoja nisinzie niote tena, ntarudi.
  Some dreams!
   
 4. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #4
  Jan 9, 2012
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,782
  Likes Received: 2,392
  Trophy Points: 280
  Kumkataza mkulima asiuze mahindi nje kwa bei nzuri,na kumruhusu wahindi kununua korosho,mbaazi,dengu,mahindi,mchele kupeleka india
   
 5. M

  Mendelian Inheritanc Member

  #5
  Jan 9, 2012
  Joined: Dec 25, 2011
  Messages: 86
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ninapoelekea kukata tamaa na matendo mabaya ya CCM kwa watanzania,huwa nakumbuka kwamba siku zote ukweli na upendo hushinda. Tanzania imekuwa na watu Mafisadi katili, lakini mwisho wa yote nao pia wameanguka vibaya sana.
   
Loading...