Yajuwe mahitaji 18 muhimu ya mwanamke ktk mahusiano

Aug 8, 2018
13
9
SEHEMU YA 2.

Na Joachim Mkwawa
Rejesha Mahusiano Yaliyovunjika.

Habari mpendwa;
Natumai umzima wa afya.
Karibu na uungane nami tena leo katika mada yetu na leo tupo sehemu ya 2.

Nikumbushie nilipoishia sehemu ya 1.
Utakumbuka nilisema kuwa Mwanamke anahitaji:-
(1)Amani ya Nafsi.
(2)Upendo wa dhati.
(3)Tumaini/Hakikisho.
(4)Mawasiliano.

Sasa leo tiririka nami:-

(5)Ushirikishwaji.
~Waswahili husema kwamba popote palipo na mafanikio ya mwanaume basi utambuwe kuwa nyuma yake yupo mwanamke anayejitambuwa yaani jasiri.
Ukimshirikisha mwanamke katika maono naipango yake kutamfanya ashiriki moja kwa moja kuhakikisha unafanikisha kwa sababu huamini kuwa kufanikiwa kwako ndiko kufanikiwa kwake.Ukimshirikisha mwanamke mipango yako kimaendeleo kunamfanya awe jasiri kujitoa na hata kuisimamia na mkafanikiwa.Kumshirikisha mwanamke huwa kunampa hali ya kujiamini,ari ya kusimamia,nguvu na uwezo wa kukutetea na kuitetea ama kuilinda mali yenu kama familia.

Ushirikishwaji ktk mahusiano humfanya mwanamke ajiamini na kuhisi anakubalika kwako.Hivyo humfanya awe msikivu,mtii,mnyenyekevu na mweny utayari kukuvumilia hata ktk magumu mnayopitia.Lkn pia humpa msukumo wa kutimiza wajibu wake kwako,kukutumikia na kutenda sawia na mahitaji ama malengo ya familia.

Unapomuachia kodi ya meza mfano zaidi ya ile aliyoizoea kila siku na huku huna uhakika wa kupata pesa siku hiyo au siku za usoni ni vema ukamwambia.Akilijuwa hilo huwa inamlazimu yeye kuwa makini ktk matumizi yake na hata ikawavusha salama ktk hali hasi mtakayoipitia.Lkn kama husemi usishangae mwenzio akalipa mchezo sijui,mara kapita muuza vijiko kanunua,mara Mangi dukani akalipwa deni au hata kukopesha majirani halafu baadaye unashangaa anakuagiza jioni uje na mboga ilihali asubuhi ulimuachia pesa ya kutumia.

Kumshirikisha mwanamke kunafanya aijuwe vema hali yako na kujipanga akabiliane nayo vipi.Ukiwa huna kitu wewe huwezi kwenda kwa Mangi dukani akupe unga na sukari kwa mkopo lkn yeye anaweza kupewa bila shida.Mfano mnaweza kuwa na unga na mkaa ndani lkn mboga hamna na baba(mwanaume)huna kitu;ukweli huwezitoka chumbani kwako ukaenda kwa mke wa mwenzio kuomba mboga.Lkn mkeo anaweza enda kuomba akapewa.

Hivi hujawahi ona mke anampa mumewe nauli ya kutoka nyumbani kwenda kazini??.Au hujawahi kuona uliacha pesa ya tembele asubuhi lkn unarudi jioni unalishwa mnofu wa nyama??.Ulijiuliza katoa wapi??, na je, ulikula ama hukula??.

Hiyo ndiyo nguvu ya ushirikishwaji.
Usipomshirikisha mwanamke hakika hutoyajuwa mawazo yake ktk ufanikishaji wa mipango na malengo yako.Utamfanya ahisi humjali na wala hujali uwepo wake.Hivyo unafanya Aishi mguu ndani mguu nje.Na huo ndiyo unakuwa mwanzo wa mke kuiba ndani na kujenga ama kuhonga nje.Yote ni kutafuta naye awe na chakwake.

(6)Penzi
~Ndiyo!!;
Huyo siyo dada yako!.
Mwanamke anahitaji mwanaume lijali mwenye kukidhi haja zake za kimwili.Ni wajibu wako mwanaume kumshughulikia mkeo tena ipasavyo,kwa utulivu na ustadi wa hali ya juu.
Kasumba iliyopo ni kwamba wanaume wengi tunadhani kwamba kufika kwetu kileleni mara nyingi ndiyo ulijali na ushababi wa kimapenzi.Hebu jiulize ikiwa wewe mwanaume umekojoa mara 4 hadi 7 halafu mkeo hajafika kileleni hata mara 1 kuna haja gani kujidai??.

Sasa kwa taarifa yako nadhani hata wanawake waliyopo humu watanisaidia ni kwamba ktk jamii yetu ni wanawake wengi sana hasa waliyopo ktk mahusiano au ndoa hawajawahi kufika kileleni.Wengi haijui tamu hasa ya penzi.Na wengi hata kuzaa wamezaa lkn hawaijui raha ya lile tendo.Hivyo wao hufanya tu kana kwamba ni wajibu kwao hawana namna.

Sababu ni kwamba wanaume wao hawana nguvu,hawana ubunifu ktk tendo na mambo kadha wa kadha yafananayo na hayo.Ndiyo maana mwanamke mwenye changamoto hii ktk ndoa yake siku akikutana na kijana chakalamu na fundi waichezo hii adhimu no rahisi sana kuisaliti ndoa na ndiyo unakuwa mwanzo wa jeuri,kejeli,majibu na kauli zisizo na staha kwa mumewe nk.

Kijana/ mwenzangu jitahidi kumridhisha mkeo.Unaporudi punguza sana kuchati,punguza kuangalia tamthilia na seasons hadi usiku wa manane.Ufikapo nyumbani hata kama wewe ni jemedali wa jeshi hakika magwanda yako na manyota yako ni bure mbele ya mkeo.
Jitahidi kuwa na mchanganyiko mzuri wa mapishi kwa mkeo pindi muwapo faragha.Kuwa tofauti kila siku.Yaan dah!!
hahahahaa ni vema ikiwa wewe ni wa dakika 5 chali basi jitahidi kujizuia na kuwa mtundu unayetumia muda mwingi ktk kumuandaa na ikiwezekana ktk maandalizi ni vema ukahakikisha anafika kileleni kabla hamjaanza mchezo.Utaonekana bora zaidi kuliko kumtekenya na kumchezea mtoto wa watu halafu dakika 5 mbele wewe chali kama kuku wa mdondo ilihali mtoto wa mwenzio ndiyo kwanza mashetani yanaanza kumpanda huku wewe huna hali.
Watakuibia sana ukizembea.

Hilo uliweke kabisa ktk ratiba zako.Furaha yako na kufanikiwa kwako kazini huwa kunaanzia nyumbani.Ukiheshimika nyumbani hata nje utaheshimika.Mfanye mwanamke wako ahisi yupo pahala salama na pa kipekee kwako.Mfanye awe na majibu ya kwakata ngebe akina Mangi madukani,watu wa magengeni,sokoni,mabuchani nk.Ni aibu sana kuona mwanamke ana mme mzuri,maisha mazuri,wana mafanikio lkn cha ajabu anatoka na mlisha nguruwe wao au muuza tembele na mchicha kwenye baiskeli.

(7)Kuelekezwa:-
~Mwanamke ni mtu wa taarifa.
Ndiyo maana kila mara unaona mara kakubibu,mnamaliza kuongea dakika chache mara kakuuliza vipi kazi,mara vi sms nimekumiss dear nk.Yote ni kutaka kujuwa nini kinaendelea juu yako.Mwanamke ni kama mtoto ndugu yangu kwani hucopy unachoeleza ama kukifanya.Ikiwa umemzoesha saa 2 tu upo nyumbani kuangalia taarifa ya habari basi siku unapochelewa unapaswa kumueleza.Anapokosea usimclash bali ongea naye taratibu kwa kumuelekeza.Na hata anapokukwaza ukajikuta umempiga basi mwisho wa siku mueleze zababu ya kumpiga iwe ktk marumbano alikujibu vibaya,alikutukana nk.
Muelekeze mkeo unapopanga mipango yako una maratajio gani na kwa nini?.Umemuweka kwenye biashara muelekeze yupo pale kwa sababu gani,kinachopatikana kinatakiwa kifanyiwe nini na kwa nini??.Bure fremu mtairudisha kwa mwenyewe maana Atauza pipi ya 200 atanunua kashata za karanga kwa muuza kahawa anakula.Ndiyo si hujamwambia.
Unachomueleza mkeo ndicho hutembea nacho na kukiishi.Kuna vitu anavifanya anakukwaza usikae kimya mueleze na kumuelekeza abadilike kwa sababu vijitabia kama hivyo uvionavyo unaona kwamba vinalenga kuwabomoa na si kuwajenga.

Mwanamke huwa hapendi mtu mbumbumbu.Mtu mkimya kimya muda wote.Mtu anayewaza kupiga tu ngumi hata ktk makosa madogo.Mtu wa makelele na kila aina ya gubu kila mara ama mtu wa kulalamika muda wote.Mwanaume wa kweli kauli yake 1 tu huleta utulivu na amani ndani ya nyumba.Unaposema sitaki basi iwe sitaki kweli lkn elekeza hiyo sitaki yako ni kwa sababu gani??.Na sababu kubwa ni yale matokeo hasi ya kilichotokea.

Naishia hapa.
Mchana tena nitaendelea.
Wako ktk Mapendo
Mr.Rejesha
Joachim L Mkwawa
REJESHA MAHUSIANO YALIYOVUNJIKA.
joachimmkwawa8@gmail.com
+255 625887699
IMG_20190613_212150_159.jpeg
 
Mbona nikimuuliza hayo yote ulioandika huwa haniambii nimfanyie ..eti yeye unataka pesa tu ..hahahh
Umeoa mfanya biashara?.
Kama ndivyo basi ni dhahiri kwamba Hapo hakuna tumaini la kuendelea kwenu.Hampo kwa ajili ya maisha.Na maana yake ni kwamba umejifunga wewe mwenyewe kulingana na vile ulimuingia mara ya kwanza.Km uliingia kwa kutumia pesa basi usishangae kwamba bila pesa hurambi unga(hupati penzi).
Ushauri badili life style yenu ama ikibidi badili mahusiano na umuepuke kwa mustakabali wa maendeleo yako.
Hatuoi tu ili kukidhi haja zetu kimwili bali tunaoa ili Kupata washauri wema na wasimamizi wazuri wa malengo yetu maishani.
 
Haya ulioeleza yanasaidia kwa nyakati flani lakini sio mara zote....
 
Back
Top Bottom