Yajue haya kabla ya kuingia kwenye ndoa

umenikuna..japo ndoa yangu ishavunjika lkn nimepitia 80% ya uliyoyaainisha ktk mada yako hivo sishangai nimefika hapa .
 
YAJUEHAYA KABLA YA KUINGIA KWENYE NDOA:

1. Sherehe ya Harusi ni ya siku moja tu, na Ndoa ni ya maisha yote. Usichanganye hivi vitu viwili!

2. Mwanamume/Mwanamke aliyezoea kuchepuka kabla ya Ndoa, ataendelea kuchepuka hata baada ya Ndoa. Usifuge mamba nchi kavu siku atarudi mtoni!

3.Upole na ukimya si kiashiria cha tabia njema. Wengi walikuwa wapole kama Maria aliyemzaa Yesu..

4. Ukikitaka ambacho hakijawahi milikiwa na mtu yeyote, ni lazima ufanye jambo ambalo halijawahi fanywa na mtu yeyote. Km onja onja utakutana na vilivyo onjwa tu, km hujaonja utakutana na visivyoonjwa!

5. Mungu akitaka kukubariki hukuletea mtu, na Shetani akitaka kukuangamiza hukuletea mtu. Chunga na weka maombi mbele, wote ni watu!

6. Bora uishi mwenyewe kuliko kuoa ama kuolewa na mtu asiye sahihi. Maisha yatakuwa majuto makubwa na mateso ya moyo!

7. Aina tatu za wanaume wakuepukwa:
(a) Walevi
(b) Wazinzi
(c) Wagomvi.

Aina tano za wanawake wa kuepukwa;
(a) Walevi
(b) Wazinzi
(c) Wachawi
(d) Wagomvi
(e) wasio tii

8 .Kuolewa na Mchekeshaji hakutakufanya uwe na Ndoa yenye furaha. Kwani ile ni kazi sio furaha yake, kuolewa na mwimbaji pia si kuburudika..

9. Maneno matatu yanayojenga amani katika Ndoa:
(a) Nakupenda, usilisahau!
(b) Samahani. Ukoseapo
(c) Asante. Kwa kila jambo shukuru!

10. Kupiga punyeto kwa mwanaume na kujichua kwa mwanamke ni kuharibu mwili wako mwenyewe. Unajiua mwenyewe kidogo kidogo

11. Kuoana kabla ya kuwa marafiki ni kama gari bila mafuta. Hamuwezi kufika popote. Uchumba na urafiki kabla ya ndoa ni muhimu mno!

12. Mafanikio ya Ndoa siku zote ni pembetatu:
>Mungu mmoja
> Mume mmoja
> Mke mmoja.
Changanya mengine uone!!

13. Furaha ya kudumu maishani hutegemea na chaguo lako la mwenzi ktk Ndoa. Usichaguliwe, ila zingatia ushauri!

14. Usioe/kuolewa na pesa au mali. Oa/Olewa na mtu. Pesa/Mali hufilisika lakini utu hudumu milele.
Kuna tofauti kati ya mapenzi na mali!

15. Uchumba uliovunjika ni bora zaidi kuliko Ndoa isiyo na amani wala furaha. Kuvunja uchumba kusikuumize kama unataka furaha ya kweli katika maisha!

16. Usiweke kipaumbele chako kwa muonekano mzuri wa mwanamke. Hakuna mwanamke mbaya, bali anahitaji kupendezeshwa. Tunza uone kama hajapendeza!

17. Mapenzi si upofu. Upofu ni kuoa ama kuolewa na mwanamume/mwanamke kwa sababu tu anakidhi haja zako kingono. Hapa pameharibu wengi, ngono utamfunza ila tabia ni vigumu kubadili!

18. Ukiwa rafiki mwema, utawavutia marafiki wema. Vivyo hivyo kwa marafiki wabaya (Bad company corrupt good character) Shikamana na marafiki wema upate mema!

19. Asili ya mikono inayojali ni moyo unaojali. Kuwa mtu wa kujali kadri ya uwezo.

20. Iepuke Ndoa mbaya kabla haijaanza... Bora kuvua kiatu mapema kuliko kuvaa kikakubana safari yote!

""Mungu awabariki Sana"".
Kuoa au kuolewa si mchezo
Ndoa ni ya miaka
Harusi ni ya siku moja.

Tafuta mke bora usitafute uzuri
Tafuta mume bora usitafute pesa!
Bora masikini mwenye Furaha na amani kuliko tajiri anayeishi maisha ya Mateso na kukosa amani ya moyo!

#wants_to_see_you_change_everyday.
Mr Franco Samuel

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom