Yajayo yanafurahisha. Je, uko tayari?

roservelt

JF-Expert Member
Aug 31, 2016
1,418
1,510
Heri ya mwaka mpya wana JF…
Niende moja kwa moja kwenye mada,
Ni wazi dunia ya sasa (karne ya 21) ni tofauti kabisa na dunia ya karne zilizopita katika Nyanja za Kiuchumi, Kisiasa, Kijamii na Kiteknolojia. Mafanikio ya sasa ni matokeo ya juhudi, uwajibikaji uliofanywa na watu mbalimbali kipindi cha nyuma. Wanasayansi kwa kutumia maarifa yao na kufanya tafiti mbalimbali wameweza na wanaendelea kugundua vitu mbalimbali kufanikisha Dunia na viumbe vyote waishio ndani yake vinakuwa salama na kufaidi matokeo ya ubunifu wao ikiwemo kurahisisha kazi mbalimbali.

Nyanja ya kiuchumi:
Miaka ya nyuma vyanzo vikuu vya utajiri vilikua ni malighafi mbalimbali (material things) mfano madini (dhahabu, chuma, makaa ya mawe) pamoja na visima vya mafuta. Dunia ya leo chanzo kikubwa cha utajiri ni maarifa.

Miaka ya nyuma ili nchi ziweze kuwa na uchumi imara zilikua zinatumia njia mbalimbali kama uvamizi (conquest) kuvamia nchi nyingine na kupora mali zao kama vile madini. Mfano mzuri ni nchi ya Ujerumani iliivamia Ufaransa na kupora majimbo yake mawili ya Alsace na Lorrane yaliyokuwa na utajiri wa chuma na makaa ya mawe. Uvamizi huu ulipeekea kuibuka kwa vita baina ya hayo mataifa mawili iliyojulikana kama Franco- Prussian war (1870-1871).

Dunia ya sasa nchi nyingi zinatumia maarifa zaidi ili kuweza kuwa na nguvu kiuchumi, kisiasa, kijeshi, kijamii na kiteknolojia. Mfano mzuri ni China, kwa kiasi kikubwa China amefanikiwa kuliteka soko la Africa na dunia kwa ujumla kwa kuanzisha mahusiano ya kibiashara na nchi mbalimbali na kufanikiwa kupata soko la bidhaa zake hasa za kielektroniki kwa kuziuza kwa bei ambayo inatofautiana kati ya bara moja na lingine kuendana na ubora wa bidhaa husika.

Pia dunia ya sasa inafurahia mchango mkubwa wa maendeleo ya sayansi na teknolojia katika Nyanja ya usafirishaji( fast moving cars, aeroplane, Jet), kuwasiliana(internet, social network, smartphones and computer), biashara( online tradings/ E- Commerce) kilimo(modern farming equipment and irrigation), na kuongezeka kwa ubora na wingi wa bidhaa za viwandani.

Nyanja ya teknolojia.
Kihistoria kila baada ya takribani miaka 500 dunia hupokea mabadiliko makubwa, kwa sasa tupo kwenye information age, kabla ya hapo dunia ilikua kwenye industrial age ilyoishia miaka ya 1989 baada ya kuvunjika kwa ukuta wa Berlin.”The information age means we all need to become more self-sufficient, grow up and take personal responsibility for our future”

Kwenye information age tutaangalia mchango wa mwanasayansi Elon Musk katika project zake mbalimbali. Huyu ni mwanzilishi wa kampuni kama Space X inayojihusisha na maswala ya anga na TESLA inayojihusisha na utengenezaji wa magari yanayotumia umeme. Dunia ya sasa inategemea mambo makubwa mengi kutoka kwa Elon kwani ana mipango mingi ya kuibadilisha dunia kupitia project zake nyingi.

Elon ana mpango wa kupeleka dunia kuishi kwenye sayari ya Mars. Pia kupitia ugunduzi wake ana mpango wa kuanzisha magari yatakayotumia nishati ya umeme. Kubwa kutoka kwa mwanasayansi huyu ana project inayojulikana kama Hyperloop. Hii ni teknolojia ya treni yenye kasi zaidi ambayo itakuwa inatumia mwendokasi wa kilomita 1200 kwa saa. Treni hii itakuwa inapita ndani ya tunnel ambalo halina hewa ndani yake(vaccum).

Nyanja ya Kijamii.
Kwa kiasi kikubwa maendeleo ya sayansi na teknolojia yameleta mchango mkubwa sana katika Nyanja hii. Ugunduzi wa kinga na madawa dhidi ya magonjwa mbalimbali kama TB, Ebola, Flu na saratani umechangia kupunguza vifo vya watu na pia makadirio yay a kuishi kwa watu (life expectancy) yameongezeka kutoka miaka 40( karne ya 18) hadi kufikia miaka 70( karne ya 21) kwa nchi zilizoendelea.

Utafiti wa kisayansi ulofanywa na wanasayansi Aubrey de Grey na Ray Kurzwel (winner of the 1999 US National Medical of Technology and Innovation), unaeleza kwamba kufikia miaka ya 2100 kuna uwezekano mkubwa vifo vikapungua kwa wingi sana na life expectancy kufikia miaka 150. Hili litachagizwa zaidi na ugunduzi wa madawa yatakayosaidia kutibu magonjwa pamoja na kuziongezea nguvu tissues na organ mbalimbali kama ngozi, ubongo na macho.

Madawa hayo yatazifanya organ na tissue hizo kufanya kazi kwa muda mrefu bila kuchoka. Pia itamlazimu mwanadamu kupata kinga fulani labda kila baada ya miaka10 kwa lengo la kuboresha organ na tissue mbalimbali za mwili.

Utafiti wa kisayansi unaonesha kwamba kifo ni matokeo ya makosa ya kiufundi (technical problem) na kila kosa la kiufundi lina suluhisho. (You can accept death, deny it or fight it). Mfano ukiumwa utaenda hospitalini na muuguzi atakufanyia uchunguzi kasha atakupa majibu ya kinachokusumbua, labda unasumbuliwa na malaria, flu, typhoid au TB. Majibu ya muuguzi kamwe hayawezi kuwa wewe unasubiri kifo, kwa sababu anajua hayo magonjwa yanatibika. “Every technical problem has got it solution”

Wanasayansi wanaenda mbali kwa kusema kwamba majanga ya asili kama tetemeko la ardhi, milipuko ya volcano, mafuriko na ukame yanasababishwa na makosa ya kiufundi. Hivyo kama serikali itatengeneza sera nzuri na kuchukua tahadhari mapema, kutakua na asilimia kubwa ya kupunguza vifo vitokanavyo na majanga ya asili na kupelekea makadirio ya kuishi kwa mwanadamu kufikia miaka 150.

Ongezeko la makadirio ya kuishi kwa mwanadamu litaleta mabadiliko makubwa sana kwenye mahusiano, ndoa, masuala ya kiuchumi na kisiasa pia. Kama mwanadamu atakuwa na uwezo wa kuishi miaka 150 hivyo pia nafasi ya watu kuoa au kuolewa itabadilika. Tutegemee kuona watu wakioa au kuolewa katika umri wa miaka 70..80….90 na kuendelea. Pia kwenye siasa tutegemee kuona katiba za nchi kuhusu muda wa kiongozi kukaa madarakani kubadilika pia.

It is therefore likely that major epidemic diseases will continue to endanger humankind in the future, only if humankind itself creates them.
The future is exciting!!!!!!!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
uzuri wa sayansi mambo yake mengi unaweza prove na matokeo yake yanaonekana tofauti na dini inahitaji zaidi imani.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sayansi na dini vinapishana sana maana unakuta kitabu kinasema kuna watu waliishi miaka 200 nk lkn ikaja ikashuka wastani hadi wa 40 sasa tena sasa tena technology inasaidia wanafika wastani wa 70 huenda huko mwaka 3000 tukafika wastani wa 200 kwa developed countries.
 
Unajua kuna ugonjwa ambao binadamu wengi unatusumbua huu ugonjwa unauhusiano mkubwa sana na akili na moyo,huu ugonjwa ni kutokutambua mipaka ya akili zetu na ufahamu wetu.

Suala la kusikitisha ni kuwa mpaka leo wanasayansi wana jua ya kwamba kifo ni makosa ya kiufundi ?

Wanashindwa kujua au wao wanaona kifo tu ni kwa magonjwa,sisi tuna sema magonjwa ni miongoni mwa sababu tu katika zile sababu za kifo.

Lakini pia nimefurahi kwa wao kukubali kivitendo ya kuwa kifo hakizuiliki,na hapajawahi kutokea mtu akafa kabla ya siku yake,na sisi huwa tuna sema hivi ikifika siku yako haicheleweshwi hata sekunde moja.

Wastani wa kuishi kwa mwanadamu wa zama zetu ni miaka sabini,ikitokea umevuka hapo basi ni kwa mapenzi ya Mola mlezi na hili halitakuja kuwezekana.

Nipo ....
 
Unajua kuto tambua uwezo wetu binadamu hupelekea hao wajiitao wanasayansi kuudanganya sana ulimwengu.
 
Mada hatari sana hii na inaonyesha sisi wala hatuna habari na kinachoendelea
World Economic forum leo wameongelea kuhusu wachina na kasi yao
Na kubwa zaidi ni jinsi gani wanapambana kuwalisha watu wao 1.4b
Na walishaji sisi tumo pia can you imagine
Lakini sijawahi kusikia hii
Na kweli mpaka tumbo lishibe ndio uongeze maarifa
dade54b8f2aced59ee5c025d9ca6e971.jpg
093f16589d1428860cd2d21dce89aee3.jpg
3e3d6e5c3786e10cdcaebefdc6e4f931.jpg

Sent from my SM using Tapatalk
 
Unajua kuna ugonjwa ambao binadamu wengi unatusumbua huu ugonjwa unauhusiano mkubwa sana na akili na moyo,huu ugonjwa ni kutokutambua mipaka ya akili zetu na ufahamu wetu.

Suala la kusikitisha ni kuwa mpaka leo wanasayansi wana jua ya kwamba kifo ni makosa ya kiufundi ?

Wanashindwa kujua au wao wanaona kifo tu ni kwa magonjwa,sisi tuna sema magonjwa ni miongoni mwa sababu tu katika zile sababu za kifo.

Lakini pia nimefurahi kwa wao kukubali kivitendo ya kuwa kifo hakizuiliki,na hapajawahi kutokea mtu akafa kabla ya siku yake,na sisi huwa tuna sema hivi ikifika siku yako haicheleweshwi hata sekunde moja.

Wastani wa kuishi kwa mwanadamu wa zama zetu ni miaka sabini,ikitokea umevuka hapo basi ni kwa mapenzi ya Mola mlezi na hili halitakuja kuwezekana.

Nipo ....
Unajua kuto tambua uwezo wetu binadamu hupelekea hao wajiitao wanasayansi kuudanganya sana ulimwengu.
Watu wanawaza ni jinsi gani wavuke hiyo mipaka ili kuleta usalama na urahisi duniani wewe unawaza kukwama.

Ama kweli hizi dini zimetuharibia watoto

Kwahiyo hata madawa na mashine za kisasa huko mahospitalini ni za uongo?

Unapopewa tahadhari ya vimbunga, matetemeko, mvua kubwakubwa, tahadhari ya magonjwa fulani nk, unakuwa unadanganywa?

Vipi hiyo smartphone inayotumia kupost hapa jf?

Unaelewa ni mahesabu ya namna gani yamepigwa hadi kufanya internet ipatikane mataifa yote duniani?

Unawabeza wanasayansi wakati inasemekana mitume wako walipansa wanyama ilihali wewe unaweza kupita hadi angani
 
Unajua kuna ugonjwa ambao binadamu wengi unatusumbua huu ugonjwa unauhusiano mkubwa sana na akili na moyo,huu ugonjwa ni kutokutambua mipaka ya akili zetu na ufahamu wetu.

Suala la kusikitisha ni kuwa mpaka leo wanasayansi wana jua ya kwamba kifo ni makosa ya kiufundi ?

Wanashindwa kujua au wao wanaona kifo tu ni kwa magonjwa,sisi tuna sema magonjwa ni miongoni mwa sababu tu katika zile sababu za kifo.

Lakini pia nimefurahi kwa wao kukubali kivitendo ya kuwa kifo hakizuiliki,na hapajawahi kutokea mtu akafa kabla ya siku yake,na sisi huwa tuna sema hivi ikifika siku yako haicheleweshwi hata sekunde moja.

Wastani wa kuishi kwa mwanadamu wa zama zetu ni miaka sabini,ikitokea umevuka hapo basi ni kwa mapenzi ya Mola mlezi na hili halitakuja kuwezekana.

Nipo ....
Mkuu kwa dunia ya sasa..na utafiti uliofanywa na unaoendelea kufanywa na wanasayansi kuna uwezekano wa kuja na majibu yakosolve changamoto mbalimbali zinazoikumba dunia. We angalia maendeleo ya dunia ya sasa ktk nyanja tofauti ni tofauti kabisa na maendeleo yaliyopatikana kipindi cha nyuma. Hivyo tutegemee kuona makubwa huko mbeleni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu wanawaza ni jinsi gani wavuke hiyo mipaka ili kuleta usalama na urahisi duniani wewe unawaza kukwama.

Ama kweli hizi dini zimetuharibia watoto

Kwahiyo hata madawa na mashine za kisasa huko mahospitalini ni za uongo?

Unapopewa tahadhari ya vimbunga, matetemeko, mvua kubwakubwa, tahadhari ya magonjwa fulani nk, unakuwa unadanganywa?

Vipi hiyo smartphone inayotumia kupost hapa jf?

Unaelewa ni mahesabu ya namna gani yamepigwa hadi kufanya internet ipatikane mataifa yote duniani?

Unawabeza wanasayansi wakati inasemekana mitume wako walipansa wanyama ilihali wewe unaweza kupita hadi angani
Umeongea ukweli kabisa. Yaani inabidi aelewe kwanza dini na sayansi ni vitu viwili tofauti. Na jinsi binadamu anakumbana na changamoto nyingi ndivyo wanasayansi wanaongeza nguvu kwenye uvumbuzi wa kutatua hizo changamoto.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom