sambeke
JF-Expert Member
- Nov 26, 2014
- 713
- 652
Anaandika Mzee wangu Yahya Msangi
BUNGE LETU LIMEKUWA KICHAKA CHA WAHALIFU
Mheshimiwa raisi nikupongeze kwa hatua uliyochukua ya kumwajibisha Waziri ambaye alikiuka maadili ya uongozi. Siku moja kabla niliandika makala kuonyesha kuwa sakata hili la Makonda linaongozwa na wazungu wa unga. Nilikutaarifu pia kwamba ulikosea sana kuhamisha vita toka kwa aliyeianzisha! Bahati mbaya umeshateua mtu si vyema kumpokonya! Lakini tafadhali hakikisha aliyeaianzisha anashiriki! La sivyo mkuu hutapata kitu!
Lakini mheshimiwa una kazi! Bunge limeshikwa na wazungu wa unga! Mimi naamini kijana wako Nape katumika tu bila kujitambua. Lakini yeye kama waziri kukosa kujitambua ni kosa kwa hiyo alistahili ulichompatia. Nadhani akikaa na kutafakari ataona jinsi alivyotumika na wazungu wa unga au jinsi ambavyo hakuwaza vyema.
Waziri huyu aliratibu ziara ya wabunge kutembelea Clouds! Utaona kabisa basi lililoleta wabunge lililakiwa na yeye! Hivi toka lini bunge letu linashiriki kila tukio la kihalifu au linaloshukiwa kuwa la kihalifu? Hivi ikitokea ajali wakafa watu (na imetokea mara nyingi tu) bunge linatuma wabunge kwenda kwenye tukio? Hivi mara ngapi kumetokea ujambazi katika benki zetu? Bunge lilienda lini kwenye tukio? katika kauli ya kihayawani kabisa Serukamba anadai Waziri kaunda Tume na ikitoa taarifa itawasilishwa bungeni ili waijadili! Huu utaratibu wameiga wapi? Bogota au Mexico City? Hivi mbona ripoti ya makontena yanavyoibwa bandarini hawakuiomba waijadili? Bado tu hamuoni hii ni shughuli ya wazungu wa unga?
Nani huyu kule bungeni aliidhinisha safai hii? Ni Spika? Ni Naibu Spika? Ni Katibu wa Bunge? Je wamelipwa posho? Kama wamelipwa huu ni wizi wa hela za umma! Warejesha haraka! Kama hawakuchukua posho za bunge nani huyo aliyegharamia safari yao?
Hivi kama Waziri alikuwa na nia ya kuunda tume iweje aratibu ziara ya wabunge clouds? Hivi ilikuwaje Waziri akafika muda huo huo na muda aliofika Reginald Mengi pâle Clouds? Waliwasiliana? Reginald asingeweza kupokelewa Clouds bika kuwepo Waziri? Hii coordination nia yake nini haswa? Hivi kila mmiliki wa chombo cha habari anageamua kuwa na akili ya Waziri na Reginald kwenda Clouds Waziri angekaa ofisini kweli au angeshinda mwezi Clouds? Nani huyo alimpa wazo hili au alilengeshwa?
Kule Ifakara kuna mtu anaitwa Lijualikali alishiriki kukichoma moto kituo cha radio mbona Waziri na Kamati ya Bunge hawakufanya ziara? Hivi mbona mtu alipoita press conference na kudai rais wa nchi atakufa hatukumuona Waziri wala Kamati ya bunge wakija kukufariji? Au faraja ni kwa Clouds tu?
Toka lini bunge letu limeanzisha utaratibu wa kuzuru na kuwafariji na kujionea wenyewe matukio? Hivi katika tetemeko la ardhi kule Bukoba Bunge liltuma kamati? Au tukio la Clouds ni zito kwao kuliko la tetemeko?
Spika na Naibu wake wanatakiwa kukueleza ni nani aliidhinisha safari hii? Walipewa shinikizo? Nani hao waliwashinikiza?
Mbona msafara huu ulisheheni wabunge wenye sifa zenye utata? Kina Sugu, Bashe, Zungu, Serukamba na wa aina hii?
Je bado tuna bunge? Ninaamini kuna wabunge safi ila bunge likishatekwa na wauza unga hata hao wasafi wanachafuka au tuseme wanachafuliwa.
Mheshimiwa kumbadili waziri peke yake hakutoshi! Tatizo ni kubwa zaidi ya hapo! Lakini unapo pa kuanzia! Una wa kuanzia! Ni watu wa chama chako! Wahoji walioidhinisha na kuratibu safari hii maana hakika ni wa chama chako! Wahoji wabunge wote wa chama chako waliokuwa kwenye huu msafara! Hawa hawana tofauti kikosa ukiwalinganisha na Nape! Wamo kwenye chama kinachounda serikali unayoiongoza lakini wanaihujumu kama alivyohujumu Nape! Panga lako lisiishie kwa Nape! Ukiwaacha watajenga mazoea! Ni dhahiri hawa miili wako kwenye chama chako kiroho aidha wako kwa wapinzani wako au kwenye payroll ya wazungu wa unga!
Ni bora kutokuwa nao kundini waamue kusuka au kunyoa!
Ukichelea utakuja kulia msibani! Hawa wanasubiri wakonyezwe wasepe! Bora wasepe sasa kwa kufukuzwa! Niliwahi kutoa makala katika gazeti la RAIA MWEMA mwaka 2015 kuwa CCM haijamaliza kukata! Iendelee kukata! Juzi juzi mmekata kwenye kikao chenu Dodoma lakini mtakuja lia ikiwa mtaendela kukata nusunusu! Mbona wanafahamika? Hofu ya nini?
Ni mie raia wako!