Yahaya Jameh kugeukwa na wanajeshi?

Rais2020

JF-Expert Member
Jul 14, 2016
3,248
5,537
Kufikia jana 17/1/2017 jumla ya mawaziri 5 walikuwa tayari wamejiuzulu nyadhifa zao zote nchini Gambia kufutia kukataa kujiuzulu kwa Rais wa nchi hiyo aliyeshindwa kwenye uchaguzi na mfanyabiashara bwana Adama Barrow.

Je, jeshi la nchi hiyo litaweza kumgeuka Dictator Jameh pindi muhula wake utakapokamilika rasmi hapo kesho 19/1/2017? Kama halitamgeuka je, majeshi ya ECOWAS watatimiza azimio lao la kumng'oa kwa nguvu Dictator Jammeh kama atashindwa kujiuzulu?

Karibuni kwa uchambuzi.
 
Tayari Vikosi vya ECOWAS vipo tayari kuingia kati kijeshi, Jana Meli ya kivita ya Nigeria Iliingia pwani ya Ghana ili kutoa shinikizo kwa Jammeh kujiuzuru, leo junatano Wanajeshi kutoka ECOWAS wataelekea Senegal, kuipiga Gambia kutokea Senegal ndio rahisi zaidi.

Kumbukeni, Jammeh anadhani kuwa anapigana na ECOWAS pekee, si hivyo, Tayari UN, African Union nk. Wanatoa support yao, na juzi Ufaransa ilisema kuwa "Kila kitu kifanyike kuhakikisha Rais Mteule anaapishwa"...

Option ya Mwisho ni Vita, na wao ECOWAS wapo tayari.
 
Ukweli hapa inavoonekana ni kwamba jeshi litaacha kumtii rasmi 19/1/2019 kama rais wa nchi hiyo na kama wanajeshi wataendelea kumtii basi watakuwa wamejiandaa kupigana na majeshi ys ECOWAS
 
yahaya anataka kufanya utani na demokrasia.
lakini ngoja tuone ataishia wapi.
 
TUJIFUNZE
27549.jpg
 
Adamma Barrow anarejea Gambia leo usiku chini ya ulinzi mkali wa Jeshi ka ECOWAS ,kuapishwa Urais Kesho.
 
Jameh kaongeza pengo (gap) kwenye kumfanya ntu mweusi hasa Africa kuendelea kudharauliwa!
 
Nilichokuwa nakifikiria ndicho kilichotokea nchini Gambia. Ilikuwa lazma jeshi limgeuke huyu dictator
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom