Yafanyike marekebisho CAG awe mbunge kama ilivyo kwa AG ( Mwanasheria mkuu)

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,968
141,975
Ili kupata mawasiliano yenye uhakika ni vema pakafanyika mabadiliko madogo ya katiba ili kumuwezesha CAG kuwa mbunge.

Tumeona faida ya mwanasheria mkuu kuwa mbunge kwamba anajibu hoja zetu zote zenye utata wa kisheria pale bungeni, vivyo hivyo CAG akiwa mbunge ataweza kuzitolea ufafanuzi hoja zote za kikaguzi na zikapata ulinzi wa bunge.

Mfano swala la fedha za escrow kuwa ni za Umma au za akina Rugemalira lingemalizwa vizuri na CAG ndani ya bunge.

Nini mawazo yako hapa?

Maendeleo hayana vyama!
 
Kwa hali hii nadhani atakayekuwa anajibu atakuwa mmoja tu nae ni mkuu wa muhimili yote
 
Hiyo itawezekana tu kwa kuwa sasa CAG, amegeuzwa kuwa kama DC, kitu ambacho sio sahihi ndio maana watu wenye akili zao waliona mbali na kuamua kuwa hicho cheo kiwe kinalindwa kikatiba, ili awe huru na sio kumyenyekea mtu ali kuwepo pale!! Kwani yeye ndio mlinzi wa matumizi ya pesa za umma!! Lakini kwa kuwa tumeamua kujifanya hatunazo ili kumrizisha mtu mmoja, bora pasiwe tu CAG, wa kuchonga, awe yeye ndiye WAZIRI WA FEDHA, CAG, JAJI MKUU, kuliko sasa anajificha kwenye msitu wa mchicha!!!! kiongozi mkuu wa kanisa/dini anazibitiwa na sheria, kanuni, sembuse mwana siasa!!! Tena wa kiafrika kabisaa?!!!
 
Ili kupata mawasiliano yenye uhakika ni vema pakafanyika mabadiliko madogo ya katiba ili kumuwezesha CAG kuwa mbunge.

Tumeona faida ya mwanasheria mkuu kuwa mbunge kwamba anajibu hoja zetu zote zenye utata wa kisheria pale bungeni, vivyo hivyo CAG akiwa mbunge ataweza kuzitolea ufafanuzi hoja zote za kikaguzi na zikapata ulinzi wa bunge.

Mfano swala la fedha za escrow kuwa ni za Umma au za akina Rugemalira lingemalizwa vizuri na CAG ndani ya bunge.

Nini mawazo yako hapa?

Maendeleo hayana vyama!
Sikubaliani na hoja hii.
CAG anapaswa kuwa INDEPENDENT from any pillar of state, ingawa ana report to parliament na kuchaguliwa na the executive
 
Mnataka kuharibu Nchi sasa. Kila kitu mnakitazama kwa jicho lenye makengeza ya kisiasa
Ili kupata mawasiliano yenye uhakika ni vema pakafanyika mabadiliko madogo ya katiba ili kumuwezesha CAG kuwa mbunge.

Tumeona faida ya mwanasheria mkuu kuwa mbunge kwamba anajibu hoja zetu zote zenye utata wa kisheria pale bungeni, vivyo hivyo CAG akiwa mbunge ataweza kuzitolea ufafanuzi hoja zote za kikaguzi na zikapata ulinzi wa bunge.

Mfano swala la fedha za escrow kuwa ni za Umma au za akina Rugemalira lingemalizwa vizuri na CAG ndani ya bunge.

Nini mawazo yako hapa?

Maendeleo hayana vyama!
 
Hivi Mimi sijui au kwamba mwanasheria mkuu ni mbunge??, Sasa akiwa mbunge na akachaguliwa na wabunge was ccm anaweza kutoa majbu tofauti na ya mwenyeket/Rais kuhusiana na ufisadi wenu?? Au lengo liwe kutoa report za uongo za vifijo na mapambio Kama alivyoambiwa Kichere😂
 
Kuna mapungufu makubwa kukosa check and balance ya mihimili yetu.Tukitaka kuimarisha mihimili yetu tusipuuze kubadili katiba yetu .Kwa mfano spika wa bunge letu tukufu hapashwi kuwa kada wa chama fulani atoke nje ya bunge,pasiwepo na wabunge wakuchaguliwa au viti maalumu wabunge wote wachaguliwe na wananchi.Wanawake wachaguliwe kwa kushindanishwa kutoka kwenye vyama vyao .Mahakama iwe na judicial commission itakayowajibika kuteuwa majaji kwakukidhi vigezo na sifa za kimahakama.Uchaguzi wa Executive uwe wa majority votes hapo usiseme eti atakaye mushinda mwenzie kwa kura moja eti ameshinda kama nusu ya wapiga kura wamesema hapana uchaguzi urudiwe
 
Back
Top Bottom