Yafahamu magereza hatari zaidi duniani

Yafahamu magereza hatari zaidi duniani

Boss Manyota

Member
Joined
Nov 3, 2018
Posts
10
Reaction score
4
Habari wana JF

Nimekuwa nikifuatilia juu ya matukio ya mauaji na mateso yanayotekelezwa katika magereza dunian.

Hii imenifanya kufahamu zaidi kuwa MAGEREZA mbalimbali duniani yamegawanywa kutokana na aina ya wafungwa waliopo.
Hii ikiwa na maana kuwa wafungwa wakorofi zaidi duniani kuwekwa katika gereza moja na hali hii imepelekea magereza hayo kudubikwa na hali ya vurugu na machafuko.

Magereza haya yenye machafuko zaidi duniani ni maeneo ambayo wafungwa hupigana karibu kila siku ili kuwa salama au ili waendelee kuishi ya yamekuwa maeneo ambayo vifo na mauaji yamekuwa ni matukioo ya kila mara.

Fahamu hapa Juu ya magerezaa 10 hatari zaidi duniani.

NAMBA 10 .San Quentin, hili nigereza likoloko katika jimbo la California nchini Marekani ambalo limeanzishwa mwaka 1852 na linatajwa kama gereza kongwe zaidi California.
Lakini licha ya kuwa gereza hili linaeneo la kuuwa wafungwa kwa kutumia gesi ya sumu, mauaji pekee yanayofanyika hapa ni kupitia kemikali zenye sumu ambapo mhusika huchomwa sindano yenye kemikali hiyo.
Vurugu ni matukio yasiyoisha katika gereza la San Quentin likihusisha pia hata idadi kubwa ya walinzi.
Miongoni mwa matukio yaliyowahi kuripotiwa katika gereza hili ni pamoja na lile la mwaka 2006 ambapo kulitokea machafuko yaliyopelekewa na ubaguzi wa rangi ambayo yalisababisha majeruhi ya wafungwa 100 na vifo vya wafungwa wawili.
Inaelezwa kuwa gereza hili ni maarufu kwa kuwa na hali mbaya ya maisha ambapo ripoti iliyotolewa mwaka 2005 ilitoa maoni kuwa gereza hili ni sehemu hatari zaidi kwa watu kuishi.
NAMBA 9
Gereza la Bang Kwang , gereza hili linapatikana katika jiji la Bangkok nchini Thailand na linafahamika zaidi kwa jina la utani kama “the Bangkok Hilton.”
Hatahivyo gereza hili ni eneo ambalo hakuna yeyote anayeweza kutamani kuishi.
Gereza hili pia ni maarufu kwa kuwatesa wafungwa wake kila wakati ambapo wafungwa hulundikwa katika vyumba vidogo vidogo na hukumu za vifo hutangaza ndani ya masaa mawili baada ya kupelekwa eneo la mauaji.
NAMBA 8
Rikers Island, hili ni gereza linalopatikana katika jiji la New York na linahistoria kubwa sana ya wafungwa wakorofi.
Mwanaume mmoja aliyefahamika kwa jina la John Reyes ambaye alikuwa mlinzi katika gereza hilo mwaka 1991 awahi kusema kuwa kila wakati amekuwa na wasiwasi kutokana na vipigo na mauaji aliyokuwa akishuhudia gerezani hapo.
Inaelezwa kuwa kutokana na historia ya vurugu na ukorofi wa wafungwa katika gereza hili, gereza hili limekuwa moja ya magereza yenye sheri kali mno duniani ambapo mabadiliko mbalimbali yalifanywa na kusaidia kupunguza idadi ya wafungwa wakorofi ndani kwa kipindi cha mwaka mmoja kutoka 1000 hadi 70.
NAMBA 7 Gereza la Alcatraz Island
Gereza hili linapatikana katika Kisiwa cha Alctraz mwishoni mwa pwani ya kisiwa cha San Francisco jimboni California.
Inaelezwa kuwa gereza hili limewahi kufungwa miaka kadhaa, limekuwa gereza linaowahifadhi miongoni mwa wafungwa hatari zaidi katika historia ya wafungwa duniani.
Mmmoja wa wafungwa wa maarufu katika gereza hili alikuwa Al “Scarface” Capone.
Inaelezwa pia kuwa gereza hili lilikuwa likifahamika kwa matukio ya vurugu ya kujaribu kutoroka kwa wafungwa na tukio la aina yake lilifahamika kama “Battle of Alcatraz” mwaka 1946.
Hatahivyo gereza hili lililazimishwa kufungwa mwaka 1963 tarehe 21 mwezi machi kutokana na kuwa na hadhi mbaya pamoja na kuwepo kwa gharama kubwa kila mara za kushughulikia gereza hilo.
NAMBA 6 ADX- Florence
Hili ni gereza linalopatikana Colorado nchini Marekani na limeundwa maalumu kwa ajili ya kuwashikilia wafungwa wakorofi zaidi duniani hasa walio na madhara makubwa katika jamii.
Ifahamike kuwa makubaliano ya kisheria yalisitishwa mwezi wa 6 mwaka 2012 nawafungwa mbalimbali katika gereza hilo, usitishwaji ambao ulishutumu kuwepo kwa hali mbaya ya gereza hilo ikiwemo kudhalilishwa kwa wafungwa na kuteswa.

NAMBA 5. La Sante
Namba tano inashikiliwa na gereza kutoka nchini Ufaransa lifahamikalo kaa La Sante, gereza hili linafahamika kama eneo la mateso ambalo wafungwa wengi wamejiua wakiwa wanatumikia vifungo vyao ambapo mwaka 1999 wafungwa 124 walijiua.
Vurugu katika gereza hili hazishikiki kutokana na wafungwa kuwa nje ya sero masaa manne pekee kwa siku nzima.
Hatahivyo mfumo wa gereza hilo umefanya kuwepo kwa uongozi wa kufuatana ambapo umepelekea baadhi ya wafungwa kuwa na nguvu zaidi kuliko wengine hivyo kufanya wasiokuwa na nguvu kuwa na hali mbaya zaidi.

NAMBA 4. Gereza la Diyarbakir
Gereza hili linapatikana nchini Uturuki, na inaelezwa kuwa mazingira ya gereza hili yamekuwa ya kinyama zaidi.
Miongoni mwa matukio ya kinyama yaliyowahi kushuhudiwa katika gereza hili ni pamoja na kuwafungwa watoto kutumikia vifungo vya maisha.
Hali ya vurugu katika gereza hili imekuwa ikishuhudiwa sana upande wa walinzi wa gereza kuliko wafungwa wenyewe.
Mnamo mwaka 1996 lilitokea tukio ambapo walinzi wa gereza hilo na polisi walimpiga mfungwa kipigo cha mbwa koko tukio ambalo lilipekekea vifo vya wafungwa 10 na majeruhi 23.
NAMBA 3 Gereza la Lasabbaneta.
Gereza hili linapatikana nchini Venezuela, Marekani ya kusini. Miundombinu ya gereza hili imejengwa kuwahifadhi wafungwa 15,000 pekee lakini linawahifadhi wafungwa 25,000.
Gereza hili pia linawafanyakazi hafifu ambapo kwa makadirio kila mlinzi mmoja wa gereza anawalinda wafungwa 150.
Kubwa zaidi gereza hili linafahamika kwa matukio ya vurugu, mwaka 1994 vurugu zilizohusisha mapigano ya risasi yalipelekea vifo vya wafungwa 108
Na mwaka 1995 wafungwa 196 waliuawa huku 624 wakijeruhiwa katika vurugu zilizozuka katika gereza hilo.
NAMBA 2 Gereza la Tadmor.
Hili ni gereza la Kijeshi katika mji wa Palmyra nchini Syria. Gereza hili linafahamika kama moja ya magereza yenye kunyanyasa zaidi wafungwa duniani kutunza muda
Shirika la Kimataifa la Amnest International lilieleza kuwa kila sehemu ambayo waliitazama inaonyesha kufanywa kwa vitendo vya kinyama kwa wafungwa wake.

NAMBA 1
Gereza la carandiru penitentiary linalopatikana nchini Brazil. Hili linatajwa kama gereza lenye vurugu zaidi duniani na ambalo linamatatizo mengi ya kiafya ambap ripoti zinasema kuwa kati ya watu watano ndani ya gereza hili mmoja kati yao anavirusi vya ukimwi.

Kwa maelezo ya kina zaidi tazama video hii

Mwenye madini zaidi juu ya magereza haya anaweza kushare hapa.
 
Umenikumbusha mbali kipindi niko mbeya gerezani niliambiwa napelekwa huko sema uzuri nilikata rufaa kesi yangu so nikatoka ila nilipanga nitoroke tu endapo ningeenda huko ngwara
Lipo moja Tz linaitwa Ngwara lipo Chunya Mbeya.Limejengwa katikati ya mbuga ya wanyama Pori.
 
Hapo sijaona guantanamo bay au siku hizi halipo ktk list ya magereza hatari mkuu....
 
Mkuu hayo ni magereza hatari yanayoongoza kwa vurugu zaidi,,,yapo ambayo yanaongoza kwa ulinzi mkali ikiwemo Guantanamo Bay
 
Ohooo hapo nimeelewa mkuu basi nilikua nachanganya kwa hatari na ulinzi...thnks
Mkuu hayo ni magereza hatari yanayoongoza kwa vurugu zaidi,,,yapo ambayo yanaongoza kwa ulinzi mkali ikiwemo Guantanamo Bay
 
ahh yote cha mtoto segadansi balaa maji enzi hizo hakuna sasa nasikia kuna maji yanaitwa maji ya sheik ponda. unaweza kutana na mtu anauza suruali kama machinga. sigara kali inakatwa mara nne una badilisha sukari robo
 
Mzee baba SONA ni hatari sana ..kwanza walinzi walishawaacha mnafanya mnachotaka wao wako nje na M16 zao..kule kila kesi kati ya mfungwa na mfungwa inamalizwa by combat
 
Magereza Qatari yapo Africa. Gambia, Nigeria, Malawi mayo humour siara leoni.

Report ya Human right watch ya mwaka 2000 inaonyesha binadamu atakayeweza kuishi kwenye magereza ya Africa basi anao uwezo wa kuishi motoni yaaani jehanam.
 
Lipo moja Tz linaitwa Ngwara lipo Chunya Mbeya.Limejengwa katikati ya mbuga ya wanyama Pori.
Halijajengwa katikati ya Mbuga, lipo pembeni mwa kijiji cha Ngwala ila linapakana na Mbuga, hilo gereza lina historia ndefu sana.
 
Habari wana JF

Nimekuwa nikifuatilia juu ya matukio ya mauaji na mateso yanayotekelezwa katika magereza dunian.

Hii imenifanya kufahamu zaidi kuwa MAGEREZA mbalimbali duniani yamegawanywa kutokana na aina ya wafungwa waliopo.
Hii ikiwa na maana kuwa wafungwa wakorofi zaidi duniani kuwekwa katika gereza moja na hali hii imepelekea magereza hayo kudubikwa na hali ya vurugu na machafuko.

Magereza haya yenye machafuko zaidi duniani ni maeneo ambayo wafungwa hupigana karibu kila siku ili kuwa salama au ili waendelee kuishi ya yamekuwa maeneo ambayo vifo na mauaji yamekuwa ni matukioo ya kila mara.

Fahamu hapa Juu ya magerezaa 10 hatari zaidi duniani.

NAMBA 10 .San Quentin, hili nigereza likoloko katika jimbo la California nchini Marekani ambalo limeanzishwa mwaka 1852 na linatajwa kama gereza kongwe zaidi California.
Lakini licha ya kuwa gereza hili linaeneo la kuuwa wafungwa kwa kutumia gesi ya sumu, mauaji pekee yanayofanyika hapa ni kupitia kemikali zenye sumu ambapo mhusika huchomwa sindano yenye kemikali hiyo.
Vurugu ni matukio yasiyoisha katika gereza la San Quentin likihusisha pia hata idadi kubwa ya walinzi.
Miongoni mwa matukio yaliyowahi kuripotiwa katika gereza hili ni pamoja na lile la mwaka 2006 ambapo kulitokea machafuko yaliyopelekewa na ubaguzi wa rangi ambayo yalisababisha majeruhi ya wafungwa 100 na vifo vya wafungwa wawili.
Inaelezwa kuwa gereza hili ni maarufu kwa kuwa na hali mbaya ya maisha ambapo ripoti iliyotolewa mwaka 2005 ilitoa maoni kuwa gereza hili ni sehemu hatari zaidi kwa watu kuishi.
NAMBA 9
Gereza la Bang Kwang , gereza hili linapatikana katika jiji la Bangkok nchini Thailand na linafahamika zaidi kwa jina la utani kama “the Bangkok Hilton.”
Hatahivyo gereza hili ni eneo ambalo hakuna yeyote anayeweza kutamani kuishi.
Gereza hili pia ni maarufu kwa kuwatesa wafungwa wake kila wakati ambapo wafungwa hulundikwa katika vyumba vidogo vidogo na hukumu za vifo hutangaza ndani ya masaa mawili baada ya kupelekwa eneo la mauaji.
NAMBA 8
Rikers Island, hili ni gereza linalopatikana katika jiji la New York na linahistoria kubwa sana ya wafungwa wakorofi.
Mwanaume mmoja aliyefahamika kwa jina la John Reyes ambaye alikuwa mlinzi katika gereza hilo mwaka 1991 awahi kusema kuwa kila wakati amekuwa na wasiwasi kutokana na vipigo na mauaji aliyokuwa akishuhudia gerezani hapo.
Inaelezwa kuwa kutokana na historia ya vurugu na ukorofi wa wafungwa katika gereza hili, gereza hili limekuwa moja ya magereza yenye sheri kali mno duniani ambapo mabadiliko mbalimbali yalifanywa na kusaidia kupunguza idadi ya wafungwa wakorofi ndani kwa kipindi cha mwaka mmoja kutoka 1000 hadi 70.
NAMBA 7 Gereza la Alcatraz Island
Gereza hili linapatikana katika Kisiwa cha Alctraz mwishoni mwa pwani ya kisiwa cha San Francisco jimboni California.
Inaelezwa kuwa gereza hili limewahi kufungwa miaka kadhaa, limekuwa gereza linaowahifadhi miongoni mwa wafungwa hatari zaidi katika historia ya wafungwa duniani.
Mmmoja wa wafungwa wa maarufu katika gereza hili alikuwa Al “Scarface” Capone.
Inaelezwa pia kuwa gereza hili lilikuwa likifahamika kwa matukio ya vurugu ya kujaribu kutoroka kwa wafungwa na tukio la aina yake lilifahamika kama “Battle of Alcatraz” mwaka 1946.
Hatahivyo gereza hili lililazimishwa kufungwa mwaka 1963 tarehe 21 mwezi machi kutokana na kuwa na hadhi mbaya pamoja na kuwepo kwa gharama kubwa kila mara za kushughulikia gereza hilo.
NAMBA 6 ADX- Florence
Hili ni gereza linalopatikana Colorado nchini Marekani na limeundwa maalumu kwa ajili ya kuwashikilia wafungwa wakorofi zaidi duniani hasa walio na madhara makubwa katika jamii.
Ifahamike kuwa makubaliano ya kisheria yalisitishwa mwezi wa 6 mwaka 2012 nawafungwa mbalimbali katika gereza hilo, usitishwaji ambao ulishutumu kuwepo kwa hali mbaya ya gereza hilo ikiwemo kudhalilishwa kwa wafungwa na kuteswa.

NAMBA 5. La Sante
Namba tano inashikiliwa na gereza kutoka nchini Ufaransa lifahamikalo kaa La Sante, gereza hili linafahamika kama eneo la mateso ambalo wafungwa wengi wamejiua wakiwa wanatumikia vifungo vyao ambapo mwaka 1999 wafungwa 124 walijiua.
Vurugu katika gereza hili hazishikiki kutokana na wafungwa kuwa nje ya sero masaa manne pekee kwa siku nzima.
Hatahivyo mfumo wa gereza hilo umefanya kuwepo kwa uongozi wa kufuatana ambapo umepelekea baadhi ya wafungwa kuwa na nguvu zaidi kuliko wengine hivyo kufanya wasiokuwa na nguvu kuwa na hali mbaya zaidi.

NAMBA 4. Gereza la Diyarbakir
Gereza hili linapatikana nchini Uturuki, na inaelezwa kuwa mazingira ya gereza hili yamekuwa ya kinyama zaidi.
Miongoni mwa matukio ya kinyama yaliyowahi kushuhudiwa katika gereza hili ni pamoja na kuwafungwa watoto kutumikia vifungo vya maisha.
Hali ya vurugu katika gereza hili imekuwa ikishuhudiwa sana upande wa walinzi wa gereza kuliko wafungwa wenyewe.
Mnamo mwaka 1996 lilitokea tukio ambapo walinzi wa gereza hilo na polisi walimpiga mfungwa kipigo cha mbwa koko tukio ambalo lilipekekea vifo vya wafungwa 10 na majeruhi 23.
NAMBA 3 Gereza la Lasabbaneta.
Gereza hili linapatikana nchini Venezuela, Marekani ya kusini. Miundombinu ya gereza hili imejengwa kuwahifadhi wafungwa 15,000 pekee lakini linawahifadhi wafungwa 25,000.
Gereza hili pia linawafanyakazi hafifu ambapo kwa makadirio kila mlinzi mmoja wa gereza anawalinda wafungwa 150.
Kubwa zaidi gereza hili linafahamika kwa matukio ya vurugu, mwaka 1994 vurugu zilizohusisha mapigano ya risasi yalipelekea vifo vya wafungwa 108
Na mwaka 1995 wafungwa 196 waliuawa huku 624 wakijeruhiwa katika vurugu zilizozuka katika gereza hilo.
NAMBA 2 Gereza la Tadmor.
Hili ni gereza la Kijeshi katika mji wa Palmyra nchini Syria. Gereza hili linafahamika kama moja ya magereza yenye kunyanyasa zaidi wafungwa duniani kutunza muda
Shirika la Kimataifa la Amnest International lilieleza kuwa kila sehemu ambayo waliitazama inaonyesha kufanywa kwa vitendo vya kinyama kwa wafungwa wake.

NAMBA 1
Gereza la carandiru penitentiary linalopatikana nchini Brazil. Hili linatajwa kama gereza lenye vurugu zaidi duniani na ambalo linamatatizo mengi ya kiafya ambap ripoti zinasema kuwa kati ya watu watano ndani ya gereza hili mmoja kati yao anavirusi vya ukimwi.

Kwa maelezo ya kina zaidi tazama video hii

Mwenye madini zaidi juu ya magereza haya anaweza kushare hapa.
Sikhizi wazungu wakiandika nyie mnatafsiri na kutuandikia humu, Afrika nazani ndo kuna magereza hatari kuliko kokote duniani, ukilemaa unakufa haraka sana.
 
Kuna gereza nchini Rwanda nimelisahau kwa jina, hilo nadhani ndyo gereza hatar kuliko yote Duniani,huwa inafikia mahali wafungwa wanawala wafungwa wenzao kama nyama au chakula kutokana na uhaba wa chakula!
 
Back
Top Bottom