Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,612
Sio mara moja wala mara mbili, misafara ya wataalamu wa baadhi ya sekta za kiserikali, huwa inajumuisha mpaka watu wasiokuwa na uhusiano na safari ya nje. Tunapokwenda nje kutafuta misaada, wale tunaowapelekea bakuli la kuomba tupewe chochote kitu, wanafahamu kwa undani kila mhusika wa safari na uhusiano alionao na safari yenyewe.
Kwetu sisi safari hizi ni chanzo kingine cha picha nyiiiingi za kupost kule facebook, whatsapp na instagram, safari za gharama zinakuwa chanzo cha marafiki kutambiana kwenye magroup ya mitandaoni, tunaokwenda kuwaomba fedha wanayajua madudu yetu haya.
Inawezekana wazungu wanazo tabia za kupenda kulambwa miguu kupita kiasi, wanakuwa na ule wivu wa chini chini kila wanapomuona asiye mzungu ambaye amejaaliwa rasilimali fulani za gharama kubwa. Lakini inawezekana pia kwamba hata jinsi ambavyo wanasiasa wetu wanavyojichukulia wanapokuwa karibu na wazungu kikazi, na yenyewe ni sababu ya sisi kudharaulika.
Matanuzi tunayapenda sana, lakini siku zote huwa yana gharama kubwa, ambazo ni lazima mtu fulani aje kuzilipa "hakuna chakula cha mchana cha bure". Zile siasa za ubanaji matumizi zimekuja katika kipindi muafaka, ni lazima tujenge utamaduni wa kupenda kuwa na kiasi.
Hao hao wazungu ambao wanatupatia fedha za misaada zenye kuambatana na kero, huwa wanapokuja kuwatazama wanyama wetu, ile fedha wanayoitumia kwenye utalii, wanakuwa wameanza kuidunduliza kwa miezi kadhaa kabla hawajapanda ndege na kuja kuwapiga picha simba na tembo wetu.
Inasikitisha, yaani pamoja na safari zote zile, vikao vyote vilivyojumuisha wataalam wetu wengi, waliolala kwenye mahoteli makubwa, bado kundi linalotuhusu ni lile la kukosa!!.