Yaani haya yote,adhabu yake ni kuwazuia wanasiasa wasiseme chochote mpaka wakati wa uchaguzi na wakikaidi Msajili anawafuta katika wigo wa Siasa?

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
Nimesikiliza angalau kipande cha mchango wa Ndugu George Simbachawene kuhusu muswada wa sheria ya vyama vya siasa,nilichokigundua sasa ipo hoja inapazwa kwa kasi kuwa.....

1.Kufa kwa viwanda nchini Tanzania ni sababu ya uamuzi wa mwaka 1992 wa kuruhusu mfumo wa Vyama vingi nchini.

2.Kufa kwa Mashamba makubwa yaliyotoa ajora za kutosha ni kwa sababu ya uamuzi wa mwaka 1992 wa kuruhusu mfumo wa Vyama Vingi nchini.

3.Uwekezaji ambao haukuwa na tija kwa taifa letu kulisababishwa na uamuzi wa mwaka 1992 wa kuruhusu Vyama vingi.

4.Tatizo la ajira nchini ambalo linakuwa siku baada ya siku limesababishwa na mfumo wa Vyama vingi nchini.

5.Kashfa kubwa za Rushwa kama EPA,Escrow,Richmond,Meremeta,Dowans n.k zilisababishwa na nchi kuingia kwenye mfumo wa vyama vingi.

6.Kufa kwa Shirika la Reli,Shirika la Ndege/Anga kulisababishwa na uamuzi wa mwaka 1992 wa kuanzisha mfumo wa Vyama vingi.

Ndiyo maana George Simbachawene anasema nchi kama China ina chama kimoja tu na uchumi wake sasa ni imara.

Simbachawene anatamani Tanzania tubaki na chama kimoja ili tujenge taifa lenye nguvu duniani.Sijui kwa nini George hajatumia mifano ya mataifa ambayo yameendelea na yana mfumo wa vyama Vingi?

George Simbachawene ambaye kama sikosei aliondoshwa kwenye Wizara ya Madini na Mh Rais kutokana na kutuhumiwa na Kamati ya Mh Rais ile ya Makanikia,anasema huko nyuma nchi ilikuwa kwenye presha muda wote na akataja harakati kama..

1. Movement for Change
2. Oparesheni Sangara n.k

Kwa mtazamo wa Ndugu Simbachawene,harakati hizi zilichangia kuchelewesha maendeleo nchini.

Nakumbuka harakati hizi zlikuwa zinapiga kelele dhidi ya hiki anacholia nacho Mh Rais Magufuli kila kukicha,wizi,Rushwa,kujilimbikizia mali, Uwekezaji wa hasara.

Je Simbachawene anataka kusema Vyama vya upinzani vingekaa kimya wakati Buzwagi wanawasainisha mawaziri wetu mikataba mibovu hotelini?

Je Simbachawene anasema Vyama vya Upinzani vingekaa kimya wakati baadhi ya Mawaziri,wafanyabiasha na watumishi wa Umma wanagawana pesa za Escrow kwenye sandarusi?

Je Simbachawene alitaka Vyama vya Siasa vikae kimya wakati wakazi wa Nyamongo wanateseka na maji yenye sumu kutoka mgodi wa North Mara,wanapigwa Risasi na wawekezaji?

Je Simbachawene alitaka Vyama vya upinzani vikae kimya wakati wawekezaji kwenye migodi walipojigeuza miungu watu (wasiguswe), walipokuwa wanawahakisha wenyeji kinyama tena usiku wa manane bila fidia?

Je Simbachawene alitaka Vyama vya upinzani vikae kimya wakati wawekezaji hawa walipokuwa wanachimba madini bila kulipa kodi?huku suala la mapato wakilifanya kuwa ni Siri kati yao na Serikali

Je Simbachawene alitaka vyama ya upinzani vikae kimya wakati Twiga wanahamishwa kwenda nje kwa ndege?wanyama wanauwa na wawindaji haramu?

Je Simbachawene alitaka watu wakae kimya huku kuna watumishi wa Umma walikuwa wanakula mishahara hewa?

Je Simbachawene alitaka wapinzani wakae kimya wakati baadhi ya Viongozi wetu wakuu walipoamua kujiuzia mpaka migodi ya madini?

Yaani haya yote,adhabu yake ni kuwazuia wanasiasa wasiseme chochote mpaka wakati wa uchaguzi na wakikaidi Msajili anawafuta katika wigo wa Siasa?

Mambo haya yanatafakarisha sana sana.
 
Kipindi ni waziri wa tamisemi kushindwa kumanage wizara upinzani wanahusikaje??
Fedha alizokwapua Wizarani upinzani unahusikaje ??
Wanadhani kwamba chama kimoja kutaleta maendeleo, kumbe tatizo ni lack of commitment.
Mataifa yaliyoendelea kwa mfumo wa demokrasia hayajui??
Huyu simbachawene ni zaidi ya ulimbukeni katika forum ya siasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wabunge wa ccm wenye upeo hutawasikia kabisa wakichangia hii miswada ya kijima. Watu wenye mawazo yaliyoko kwenye miswada hii ni hatari sana kwa ustawi wa nchi hii. Some people have simply failed to provide leadership; instead they have resorted to silence any critical voice. Very pathetic. But look at what is happening in Ethiopia!
 
Kwenye masuala kama haya huwa wanachaguliwa watu ambao huwa ni mapopoma wanaokaririshwa na mfano wao mkubwa huwa ni China. Ukiona mtu katolea mfano wa China usiendelee kujiumiza kumjua ni nani jua yuko pale kwa kazi maalumu kuhakikisha upinzani unakufa Tz.

Ila kwa hali ya kidunia ya sasa ni ngumu kuzima upinzani iwe kisheria au kikatiba. Ukizuia formal itaibuka informal opposition.

Sent from my Hisense F31 using JamiiForums mobile app
 
Mh.Simbachawene, ukimsikiliza na sura tofauti, tatizo uoga,vitisho na maelekezo maalumu. Amefanikiwa kuthibiti chama chake pia, anaemtaka atarejea. Mzee baba hana dogo,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
inasikitisha na kuuma saana unapokuwa na mbunge/kiongozi aliyefikia level ya cabinet minister halafu anakuwa purely politician asiyejua hata chembe ya maendeleo yanatokana na nini!!!!!.kama ndivyo hivyo kwa nini mfumo wa chama kimoja uliodumu kwa karibu miaka 25 nchi hii haukutufikisha kwenye uchumi wa angalau wa kati?!? tumeendelea kuwa nchi maskini tangu tunapata uhuru!!!. wajemeni hawa wanasiasa hawaa!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom