Yaani hata CCM wamshangaa Roma wahoji anaficha nini?

Ongeza na hili Mwakyembe alifata nini pale? Je mkulima akidhurumiwa na akitaka kufanya press na waandishi je waziri wa kilimo ataongozana nae?
 
Nilivyomuelewa Roma ni eti, maelezo ya kina kuhusu waliomteka na maelezo waliyoulizwa wakati wakipewa vipigo wameyaripoti kituo cha Polisi Oysterbay, ambako akina ruge waliripoti tukio hilo la jinai.

Kwa madai ya Roma kwamba kwakuwa ametoa maelezo hayo Polisi Oysterbay basi amewaachia wao wanayafanyia kazi na kwamba angeyaeleza pale kwenye Press angeweza kuharibu upelelezi wa tukio.

Tujiulize ni muda gani Polisi Oysterbay watafanyia kazi tukio hilo na hatua stahili zichukuliwe kwa waliotenda tukio hilo ?
Wacha tusubiri.
Roma katudanganya sana,,tena mungu atatakiwa amchape
 
A
TUUFUNGE HUU MJADALA WA ROMA.

Na Thadei Ole Mushi.

Kutokana na Maelezo ya Roma na kutekwa kwake ni kwamba hajui waliomteka na wala hajui watekaji walikuwa wanahitaji nini.

Maswali ninayojiuliza....

[HASHTAG]#Roma[/HASHTAG] anadai hajui kwa nini alitekwa ila anasema watekaji walipomchukua walienda kumhoji. Kama walimhoji moja kwa moja anawajua waliomteka.

Aidha walimhoji kumuuliza labda kama anatembea na mke wa mtu, au walimhoji kuhusu kujihusisha na siasa, au walimhoji kuhusu nini??

Kutokana na mahojiano hayo moja kwa moja Roma anajua waliomteka ni kina nani kama hawajui atuambie walimuuliza maswali gani tutamsaidia kumwambia ni kina nani hao au na sisi tutaridhika kuwa kwa kweli maswali hayo yalikuwa hayaeleweki.

Sitaki kuongea sana hili naweza kuvuka mipaka na kuzidi kuuweka ukweli upenuni.

[HASHTAG]#Raia[/HASHTAG] wa Tanzania wana ulinzi kiasi Gani??? Kutokana na Issue hii??? Yaani mtu anatekwa na simu yake ipo hewani na sms anasoma ila bado polisi wetu hawajui alipo mtu huyo. Kama haya yanaweza kufanyika jeshi letu halioni linajiondolea weledi mbele ya raia?

Mtu anatekwa Studio taarifa zinafikishwa polisi gari waliyoondoka nayo inajulikana ni Noah na hata number za Gari zitakuwa zinajulikana ila bado polisi wanashindwa kusema ni kina nani hao....

Ubaya mmoja haya mambo hayafuatiliwi na watanzania tu bali hata majirani zetu hamuoni mnawakaribisha wakidhani mu dhaifu kwenye maswala ya kiulinzi?

[HASHTAG]#TongweRecords[/HASHTAG] hawana Mlinzi? Kama wanaye walimteka na yeye?? Maana kipengele hiki wamekisahau kwenye hili Tukio. Kama Mlinzi alikuwepo alikubalije watu kuingia ndani ya Studio na kuondoka na vitu? Je walipoingia Getini hawakujiandkisha?????

[HASHTAG]#Waliotekwa[/HASHTAG] ni wanne kwa nn Roma aende peke yake kujieleza? Katika wote waliotekwa yeye ndiye aliyepigwa zaidi kwa maelezo yake kwa nn hao wengine hawakumsaidia kwenda kuongea na vyombo vya habari wakati yeye akiendelea kujiuguza?

Hawaoni kuwa kwa tafsiri ya kawaida kabisa watakayoipata wananchi ni kuwa kama wangeenda wote wangejichanganya kimaelezo? Tayari kina Roma wanajua kuwa mtaani kuna sintofahamu kuhusu wao hawaoni kuwa kwa kutokufika wote kutaruhusu wazo hili na kuongeza hii sintofahamu??

[HASHTAG]#Roma[/HASHTAG] anadai kuwa walitupwa karibu na dimbwi wakajikokota wakapakia pikipiki wakaenda nyumbani kubadili nguo. Ila walipofika nyumbani hawakumkuta mtu hivyo walilazimika kuvunja mlango....

Ni boda boda gani iliwachukua toka hapo walipotupwa??

Roma bado alikuwa na simu yake kwa nini avunje mlango badala ya kumtafuta mkewe kwenye simu ili aje kumfungulia mlango?

Kama walimnyanganya simu ni kweli kuwa alikuwa hajui simu ya mkewe?? Si angelitafuta simu mahali ampigie?

Je majirani wa kina Roma ni nani walisikia vishindo vya kuvunja mlango??

Na kama walisikia walichukua hatua Gani?.........

[HASHTAG]#Hata[/HASHTAG] eye contact ya Roma ina Mashaka asilimia 90 kashindwa kuamgalia waandishi anajishika usoni tena machoni. Wala hakuwa na hisia za mtu ambaye kweli alitekwa.

[HASHTAG]#Unatekwa[/HASHTAG] unateswa unaumizwa halafu unaenda nyumbani kubadili nguo..... Si unapoteza ushahidi?? Kwa nn aende Polisi akiwa ameshabadili nguo?

Sitaki uamini kama ninavyoamini tuendelee na story zetu za kawaida........nilishasema hutakiwi kufikiri sana ukiwa Tanzania.


ALICHO HOJIWA NI KUHUSU NANI ANATOA REMIX NA NYIMBO ZA KUKOSOA SERIAKLI NA NANI ANAMUIMBA BASHITE KWENYE AUDIO..NA KAMA STUDIO YAO INAHUSIKA....
HAKUJIBU KAPATA KIPIGO..MIGUU IMEPASULIWA NA MWILI UMEUNGUZWAz KWA PASI YA MOTO..IANGALIE VIZURI UTAONA MIKONO IMEBABUKA
 
Mshaambiwa hata pale kwenye conference Roma hakuna huru , conference ya Roma waziri anakuja then MTU anaeongoza conference afisa wa serikali unatarajia Roma aseme nini.
 
Roma anasema maisha yake yako hatarini, hayuko Salama! Asingeweza kumwaga yote hadharani! Muacheni anagugumia maumivu tupo tuliomuelewa. Walijikuta maeneo ya Ununio si mbali na Msitu wa Mabwepande!
 
Checking...100%
Searching...100%
Downloading...100%

Network connected !
Near by Ifisi Mbeya.
 
Mm bhado nasisitizaa Roma hata asiposema ukweli bhado ukweli utajulikana tu tutajua soon maana hajatemwa peke yake wametekwa 4 hao wengine wanaweza vumilia vivuli vya watekaji kwa mda gani ? Na mm ninaimani Roma bhado katekwa hadi now
 
We are living in the mysterious world let us wait for the day of judgement.
 
Msimlaumu sana pengine watekaji waliwapa vitisho vikali pengine na kuwapiga picha mbaya ambazo zinaweza muharibia CV ya udume wake
Tumwache huwezi fahamu yaliyomkuta
 
Msimlaumu sana pengine watekaji waliwapa vitisho vikali pengine na kuwapiga picha mbaya ambazo zinaweza muharibia CV ya udume wake
Tumwache huwezi fahamu yaliyomkuta
 
Hapo alipo Roma bado katekwa........
Huu ndo ukweli ambao hatuujui mengine tutamuonea tu Roma.We ushasikia alitekwa akafungwa pingu unataka kujua kina nan wanakaa na pingu.Watekaj gan wanajeuri ya kukaa na simu yako bila kuizima.Roma ni mtu mdogo sana achen akae kimya.
 
Amekwepa camera karibu muda wote wa mahojiano!
Ni ishara mbaya sana unapojitolea maelezo, kumbuka ukiwa unataka kitu, unafundisha, unahubiri etc, huwa unatazama watu kutaka kuwasoma kuwa je wanakuelewa, vitu kama nodding, mshangao, vilio na vicheko fanani yeyote huwa anavifuatilia kwa makini!
Alichokuwa anakifanya at least kwa pale ni kuwasilisha yale maelezo na hakutaka kupata mrejesho kwa audience, hiyo ni ishara kubwa ya kuwa anachokitoa hajali kitapokelewaje ila yeye ametimiza kazi yake ya kusema tu yale aliyoyapanga kuyasema!
team ya watumishi wa serikali ilikuwa pale kumsaidia asiende nje ya focus!
alikuwa anaweza kusubiri j3 kwa formal press release lakini often kwa mtu aliyeumizwa ungepata hata baadhi ya informal news toka kwa watu wake wa karibu! kwa hili hakuna, tulipoambiwa j3 ilikuwa ni kusubiri kweli hadi j3!

Anyway, huwezi jua kuna nini nyumba ya camera!
 
Kuna kitu hapa pia ambacho Roma angepaswa kuulizwa, hivi ile boda boda waliyokodi walilipa au hawakulipa? Na kama walilipa je walikuwa na fedha mifukoni mwao au ilikuwaje!
Pia tv na computer zilizochukuliwa ziko wapi?
ugali mtamu asikwambie mtu, mke kaoa juzi tu hapa awaachieni?
 
Back
Top Bottom