Yaani hata CCM wamshangaa Roma wahoji anaficha nini?

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,873
TUUFUNGE HUU MJADALA WA ROMA.

Na Thadei Ole Mushi.

Kutokana na Maelezo ya Roma na kutekwa kwake ni kwamba hajui waliomteka na wala hajui watekaji walikuwa wanahitaji nini.

Maswali ninayojiuliza....

[HASHTAG]#Roma[/HASHTAG] anadai hajui kwa nini alitekwa ila anasema watekaji walipomchukua walienda kumhoji. Kama walimhoji moja kwa moja anawajua waliomteka.

Aidha walimhoji kumuuliza labda kama anatembea na mke wa mtu, au walimhoji kuhusu kujihusisha na siasa, au walimhoji kuhusu nini??

Kutokana na mahojiano hayo moja kwa moja Roma anajua waliomteka ni kina nani kama hawajui atuambie walimuuliza maswali gani tutamsaidia kumwambia ni kina nani hao au na sisi tutaridhika kuwa kwa kweli maswali hayo yalikuwa hayaeleweki.

Sitaki kuongea sana hili naweza kuvuka mipaka na kuzidi kuuweka ukweli upenuni.

[HASHTAG]#Raia[/HASHTAG] wa Tanzania wana ulinzi kiasi Gani??? Kutokana na Issue hii??? Yaani mtu anatekwa na simu yake ipo hewani na sms anasoma ila bado polisi wetu hawajui alipo mtu huyo. Kama haya yanaweza kufanyika jeshi letu halioni linajiondolea weledi mbele ya raia?

Mtu anatekwa Studio taarifa zinafikishwa polisi gari waliyoondoka nayo inajulikana ni Noah na hata number za Gari zitakuwa zinajulikana ila bado polisi wanashindwa kusema ni kina nani hao....

Ubaya mmoja haya mambo hayafuatiliwi na watanzania tu bali hata majirani zetu hamuoni mnawakaribisha wakidhani mu dhaifu kwenye maswala ya kiulinzi?

[HASHTAG]#TongweRecords[/HASHTAG] hawana Mlinzi? Kama wanaye walimteka na yeye?? Maana kipengele hiki wamekisahau kwenye hili Tukio. Kama Mlinzi alikuwepo alikubalije watu kuingia ndani ya Studio na kuondoka na vitu? Je walipoingia Getini hawakujiandkisha?????

[HASHTAG]#Waliotekwa[/HASHTAG] ni wanne kwa nn Roma aende peke yake kujieleza? Katika wote waliotekwa yeye ndiye aliyepigwa zaidi kwa maelezo yake kwa nn hao wengine hawakumsaidia kwenda kuongea na vyombo vya habari wakati yeye akiendelea kujiuguza?

Hawaoni kuwa kwa tafsiri ya kawaida kabisa watakayoipata wananchi ni kuwa kama wangeenda wote wangejichanganya kimaelezo? Tayari kina Roma wanajua kuwa mtaani kuna sintofahamu kuhusu wao hawaoni kuwa kwa kutokufika wote kutaruhusu wazo hili na kuongeza hii sintofahamu??

[HASHTAG]#Roma[/HASHTAG] anadai kuwa walitupwa karibu na dimbwi wakajikokota wakapakia pikipiki wakaenda nyumbani kubadili nguo. Ila walipofika nyumbani hawakumkuta mtu hivyo walilazimika kuvunja mlango....

Ni boda boda gani iliwachukua toka hapo walipotupwa??

Roma bado alikuwa na simu yake kwa nini avunje mlango badala ya kumtafuta mkewe kwenye simu ili aje kumfungulia mlango?

Kama walimnyanganya simu ni kweli kuwa alikuwa hajui simu ya mkewe?? Si angelitafuta simu mahali ampigie?

Je majirani wa kina Roma ni nani walisikia vishindo vya kuvunja mlango??

Na kama walisikia walichukua hatua Gani?.........

[HASHTAG]#Hata[/HASHTAG] eye contact ya Roma ina Mashaka asilimia 90 kashindwa kuamgalia waandishi anajishika usoni tena machoni. Wala hakuwa na hisia za mtu ambaye kweli alitekwa.

[HASHTAG]#Unatekwa[/HASHTAG] unateswa unaumizwa halafu unaenda nyumbani kubadili nguo..... Si unapoteza ushahidi?? Kwa nn aende Polisi akiwa ameshabadili nguo?

Sitaki uamini kama ninavyoamini tuendelee na story zetu za kawaida........nilishasema hutakiwi kufikiri sana ukiwa Tanzania.
 
Roma ukimuangalia usoni anapoongelea kutekwa kwake hakuhitaji use na PhD ili ugundue kama anafanya komedi,,najilaumu sana kwa nini nilimuonea huruma niliposikia ametekwa,,kwa ule ukweli Roma mungu anamuona, hakika Roma kuna kitu kakificha,,:eti hajjui walimpeleka wapi,!!?,inamaana eneo alilojikuta baada ya kumwachia halijui !!?,,mbona hasemei kuhus PC zilizochukuluwa !?mmmmmmmmmmm Roma maelezo yake kwangu yana ukakasi
 
Unawafahamu waliokamteka Dr Ulimboka, unawafahamu waliokamteka yeriko nyerere. Subir na wewe utekwe ndio utawajua watekaji
 
Kitu ambacho hamtaki kujua nikua Roma bado ametekwa hivyo anazungumza kile anacho ambiwa.
Lazima mjiongeze Mwakembe alifwata nini ktk mkutano wa Roma? Kabla ya kuongea na wandishi wa habari Roma na Mwakembe waliongea nn?
Je mmefikia hatua ya kusahau kauri "Roma atapatikana kabla ya jumapili"
Roma ni TV tu remote iko mahali hivyo kumlaumu ni kumuonea bure
 
Kitu ambacho hamtaki kujua nikua Roma bado ametekwa hivyo anazungumza kile anacho ambiwa.
Lazima mjiongeze Mwakembe alifwata nini ktk mkutano wa Roma? Kabla ya kuongea na wandishi wa habari Roma na Mwakembe waliongea nn?
Je mmefikia hatua ya kusahau kauri "Roma atapatikana kabla ya jumapili"
Roma ni TV tu remote iko mahali hivyo kumlaumu ni kumuonea bure
Nashukuru kwa kunikumbusha,,,yaani Roma tulikuwa tumemuonea huruma,,ni sawa na wale wanaowaonea huruma wanoigiza kufa kwenye movie,, Roma alifanikiwa pakubwa kuichezea akili ya yangu pakubwa,,,mungu aendelee kumuona hakika
 
Roma ukimuangalia usoni anapoongelea kutekwa kwake hakuhitaji use na PhD ili ugundue kama anafanya komedi,,najilaumu sana kwa nini nilimuonea huruma niliposikia ametekwa,,kwa ule ukweli Roma mungu anamuona, hakika Roma kuna kitu kakificha,,:eti hajjui walimpeleka wapi,!!?,inamaana eneo alilojikuta baada ya kumwachia halijui !!?,,mbona hasemei kuhus PC zilizochukuluwa !?mmmmmmmmmmm Roma maelezo yake kwangu yana ukakasi
Kwa sababu hua mnakurupuka kuweka huruma mbele baadae mnakuja kujiona wajinga,, sorry lakin kwa lugha yangu ngum
 
Binafsi najilaumu kwa nini niliuruhusu moyo wangu kuumia kwa lile igizo la utekwa kwa Roma

Igizo la kitoto, la kijinga , la kipumbavu na halistahili nafasi yoyote katika jamii ya watu wenye uelewa, ni kupotezeana muda wa kuwaza namna ya kupambana na changamoto za ugumu wa maisha
 
Nilivyomuelewa Roma ni eti, maelezo ya kina kuhusu waliomteka na maelezo waliyoulizwa wakati wakipewa vipigo wameyaripoti kituo cha Polisi Oysterbay, ambako akina ruge waliripoti tukio hilo la jinai.

Kwa madai ya Roma kwamba kwakuwa ametoa maelezo hayo Polisi Oysterbay basi amewaachia wao wanayafanyia kazi na kwamba angeyaeleza pale kwenye Press angeweza kuharibu upelelezi wa tukio.

Tujiulize ni muda gani Polisi Oysterbay watafanyia kazi tukio hilo na hatua stahili zichukuliwe kwa waliotenda tukio hilo ?
Wacha tusubiri.
 
Back
Top Bottom