Ya Zanzibar tatizo ni waliotunga Katiba

shikulaushinye

JF-Expert Member
Aug 29, 2014
828
456
Wakuu nimeona siyo mbaya kushare vipengele viwili vinavyokanganya (very controversial) ndiyo maana mambo yamekwama. Tatizo ni hawa wataalamu wa sheria waliotunga, sijui kusudi lao lilikuwa lipi kuweka mkanganyiko huu.


28.(1) Kufuatana na Katiba hii mtu ataendelea kuwa Rais mpaka:

(a) Rais anayefuata ale kiapo cha kuwa Rais; au

(b) afariki wakati akiwa Rais; au

(c) hapo atapojiuzulu; au

(d) iwapo amechaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya

Muungano wa Tanzania; au

(e) kwa sababu yoyote nyengine ameacha kuwa

Kiongozi kwa mujibu wa vifungu vyengine vya Katiba

hii.


(2) Kufuatana na maelezo ya kijifungu (1) cha kifungu hiki,

Rais ataacha madaraka yake baada ya kumalizika miaka mitano

kuanzia tarehe, ambapo:

(a) kama yeye ni mtu ambaye ndiye mara ya kwanza

amechaguliwa kuwa Rais chini ya Katiba hii alipokula

kiapo cha uaminifu na kiapo cha kuwa Rais; na

(b) kwa sababu nyenginezo mtu wa mwisho kushika

madaraka hayo kwa mujibu wa Katiba hii alipokula

kiapo cha uaminifu na kiapo cha kuwa Rais, au

pasingelikuwa na sababu ya kifo chake, basi angalikula

kiapo hicho.
 
Back
Top Bottom