Ya Udinde, hizi ndio shule miaka 46 ya uhuru?

Big Dady

Member
Nov 10, 2009
59
2
shulembuyuuuuu.jpg

Nimeshangazwa sana na picha na nimeachwa hoi bin taabani baada ya kusoam maelezo yanayohusu shule moja huko Mbeya, Wilaya ya Chunya, Kijijicha cha Udinde. Shule inaitwa Iboma. Hii ni kwa mujibu wa gazeti la mwananchi la jana. Shule yenyewe ni mti wa mbuyu. Wanafunzi wameweka viti vya mabanzi ya mbao, eti wanasomea hapo.

Kwanza ni aibu kubwa sana kwa taifa letu lenye miaka 46 ya uhuru. Ni aibu kwa chama tawala CCM kinalojinadi kwa kuwaletea maisha bora watu wake. Aibu kwa taifa linaloenda kwa kauli mbiu ya kasi mpya, ari mpya na nguvu mpya.

Hicho kijiji kina serikali inayowajibika kwa wananchi wake? Uongozi wa wilaya umepokeaje habari hiyo. Mbunge wa eneo hilo anasemaje. Ni aibu tupu.Kwa hali hiyo mbunge mhusika atawwambia ni wanacnhi wake mwakani.

Kwa bahati mbaya sana, watanganyika hawa wamekuwa wadanganyika kweli kweli, tena wepesi wa kusahau. Fulana, kofia na vitenge tu vitawafanya wasahau kila kitu na kuchagua CCM hiyo hiyo na mbunge wake mwaka ujao. Wanatanguliza shukurani kwa miaka mingine mitano. Kwani si hao hao wamekichagua kwa kuwapa kura wenyeviti wa vijiji na vitongiji.

Wananchi wanatakiwa kuamka sasa na kuwatupilia mbali viongozi wasiowajibika. Waachane na chama danganyifu, waangalie mbadala.

Poleni sana walimu mnaoitikia wito wa kufundisha chini ya mibuyu na miti. Nawaone huruma sana. Mungu atawapeni thawabu yebu mbeleni.
 
Nyoka akidondoka wanaenda mapumziko , mvua zikinyesha wanaenda likizo, Hii ndiyo Tanzania
 
Kwa vigezo vya wizara ya elimu, shule inatakiwa iweje?????

Sidhani kama hii shule imesajiliwa na kutambuliwa na wizara ya elimu kama shule per se, unaweza kukuta ni darasa la tuition la huyo mwalimu. Je twaweza pata taarifa kamili toka Chunya, Mbeya au Wizarani kuhusu uwepo wa shule hii??????
 
Subirini wawekezaji~!

Mwekezaji hawezi kuwekeza kwenye elimu hata siku moja, kwani ukierevuka utamzidi akili na ukimzidi akili utamuondoa kwenye, uwekezaji, uwekezaji ni kwenye madini, utalii, kilimo, mafuta, nyumba za NHC, ex govt quaters etc, sio elimu.
 
I m not sure that is primary school, for secondary school i agree with d photo by jibaba, there are too poor conditioned sec schools in TZ. let's have more facts on the primary school photo.
 
Sfsdhali hao wanakalia mawe na kusomea kwenye mwembe wanamwalimu hivyo wanaelewa kiasi. Je ambao wako kwenye shule za voda faster ambako hakuna walimu lakini kuna majengo wanapata nini zaidi ya ujinga? hukumbuki kipindi kile wazee wetu walipokuwa wanasoma elimu ya wetu wazima? walikuwa wanasomea kwenye mti na walijua kusoma na kuandika.
 
Back
Top Bottom