Ya Okwi na ujinga wa Mrisho Ngassa

Nyenyere

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2010
Posts
14,843
Reaction score
10,765
Kitendo cha Emmanueli Okwi kugoma kurejea Tunisia kukalia benchi kunamfanya Mrisho Ngassa aonekane mwenye busara zaidi na aliyeona mbali. Sasa Okwi inasemekana yuko radhi mkataba wake uvunjwe arejee Bongo. Pesa inafumba hadi ufahamu aisee!
 
The glory of Christianity is to conquer by forgiveness - William Blake
 
Kitendo cha Emmanueli Okwi kugoma kurejea Tunisia kukalia benchi kunamfanya Mrisho Ngassa aonekane mwenye busara zaidi na aliyeona mbali. Sasa Okwi inasemekana yuko radhi mkataba wake uvunjwe arejee Bongo. Pesa inafumba hadi ufahamu aisee!

Pesa usipojua kuiweka under control lazima ikupoteze. Do you know secret to remove any emotional attachment to material welfare?
 
Pesa usipojua kuiweka under control lazima ikupoteze. Do you know secret to remove any emotional attachment to material welfare?

The "old" form of religion could have done it. Guess what, money is the root of all evil.
 
Kitendo cha Emmanueli Okwi kugoma kurejea Tunisia kukalia benchi kunamfanya Mrisho Ngassa aonekane mwenye busara zaidi na aliyeona mbali. Sasa Okwi inasemekana yuko radhi mkataba wake uvunjwe arejee Bongo. Pesa inafumba hadi ufahamu aisee!

ili kuutendea haki mshororo (thread) huu, maneno 'ujinga wa' kwenye kichwa cha habari yarekebishwe kwa 'hekima za'. Kwa sababu Ngassa ameonesha busara kubwa sana kukataa kwenda Sudan. Angalia sababu hizi, miongoni mwa nyinginezo: (1) alijua kwamba mpango wowote wenye Rage ndani yake si mpango ni gundu. Nitajie mpango mmoja tu wa Rage, hasa kwenye michezo, hasa ndani ya Simba, uliokaa sawa nami nitakuambia siku za kupatikana fedha ya Okwi! (2) alimwangalia Sunzu walipokuwa wote Simba ambaye alitokea hukohuko Sudan kwenye timu yenye hali inayofanana na ya El Mireikh. Alipombaini ni hoahehahe kuliko yeye, akajua Sudan hakuna jipya. (3) Alijua kwamba riziki popote, lakini kwanza nyumbani. Si lazima Sudan kama Tanzania inapatikana. (4) ingawa aliahidiwa mshiko si haba El Mireikh, lakini akajua mipango si matumizi. Moja shika wende si kumi nenda uje. Asiyelijua hilo amwulize Okwi. (5) alijua inayovutaniwa na washindani wawili ni kamba ya mchezoni, si mchezaji mpira. Alijua kuvutwa katikati ya Azam na Simba kungemnyofoa yeye. (6) alijua kwamba ligi ya Sudan inahusisha pia Darfur ambako mchezaji anatakiwa kuwa makini zaidi kwenye roho yake moja kuliko pointi tatu za timu. (7) alijua kwamba wanaomn'gan'ganiza kwenda Sudan - waandishi, mawakala na viongozi wa timu walio pia wafanyabiashara - walitaka kujinufaisha kwa mgongo wake. Maana kama maslahi yako Sudan basi vyombo vya habari pia viko huko, wachezaji wa kutafutiwa timu pia wako, kadhalika na timu zinazohitaji viongozi sambamba na fursa za biashara. Kwa nini wasitangulie wao, au angalau kuahidi kuambatana naye?
kwa hivyo wanaomwona Ngassa Mjinga kwa kukataa kuuzwa utumwani, huenda wanahitaji miwani ya vioo badala ya mbao wanayoitumia kumwangalia!
 
Rage kafanikisha kuchukua 100m/- za Azam Tv, hongera zake.
 
Rage pesa ya okwi karudisha clubuni? Ya Mafisango je?
 
Rage kafanikisha kuchukua 100m/- za Azam Tv, hongera zake.

Kupitia MoU ambayo TFF wanasuasua kusaini mkataba halisi! Kama hayo ni mafanikio, basi na pesa za Okwi zitapatikana siku mojawapo ndani ya wiki mojawapo ya mwezi mmojawapo wa mwaka mmojawapo wa karne ijayo!
 
Hahaaa wabongo bana leo ndo mnamwona ngasa wa maana bada kukutupushwa warabuni
 
nakubaliana na uchambuzi wako wa busara.lakini ubongo wa ngasa haupo hivyo.kilicho dhahiri ni kwamba upenzi wa yanga pekee ndio ulimbakisha tz.mengineyo ni hekima zako tu.
 
Kitendo cha Emmanueli Okwi kugoma kurejea Tunisia kukalia benchi kunamfanya Mrisho Ngassa aonekane mwenye busara zaidi na aliyeona mbali. Sasa Okwi inasemekana yuko radhi mkataba wake uvunjwe arejee Bongo. Pesa inafumba hadi ufahamu aisee!

Hii habari na kichwa chake havina uhusiano. Kama Okwi angefanikiwa huko, labda suala la Ngasa ndio ungeita ujinga. Na sijui kama unajua hata maana ya ujinga. Mjinga ni mtu asiyejua kitu fumani - anakuwa mjinga wa kitu hicho! pengine Ngasa aliyajua hayo, ndio maana hayakumpata ya Okwi!
 
nakubaliana na uchambuzi wako wa busara.lakini ubongo wa ngasa haupo hivyo.kilicho dhahiri ni kwamba upenzi wa yanga pekee ndio ulimbakisha tz.mengineyo ni hekima zako tu.

Huwezi kujua. There is so much good in the worst of us, and there is so much bad in the best of us, it is difficult to know who of us should judge the rest of us.
 
Kitendo cha Emmanueli Okwi kugoma kurejea Tunisia kukalia benchi kunamfanya Mrisho Ngassa aonekane mwenye busara zaidi na aliyeona mbali. Sasa Okwi inasemekana yuko radhi mkataba wake uvunjwe arejee Bongo. Pesa inafumba hadi ufahamu aisee!

Kweli ng'ombe wa masikini hazai. Sasa Mkataba ukivunjwa si ina maana jamaa Zangu wa SIMBA watakosa
$ 300,000.00 walizozisubiri kwa muda mrefu!!!!. Masikini SIMBA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…