Ya Muslim University of Morogoro na Wachina

Ya Muslim University of Morogoro na Wachina

GRAND MUFTI

Senior Member
Joined
Jun 3, 2015
Posts
136
Reaction score
111
Naona hiki chuo kimeleta changamoto kubwa sana lakini pia nadhani kuna la kujifunza hapa

Uchambuzi wa kina pia unahitajika

DSCF3751%2B-%2BCopy%2B-%2BCopy.JPG


MAONESHO ya Elimu ya Juu yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja yamefunguliwa rasmi leo na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Kassim Majaliwa Kassim huku yameonesha mwitikio mzuri kwa vyuo mbalimbali vilivyojitokeza kudahili wanafunzi wanaotaka kujiunga na kozi tofauti kwenye vyuo vyao.

Ili kutoa fursa ya elimu kwa wanafunzi wanaojiunga na vyuo hivyo, Chuo cha Muslim Morogoro kimewataka wanafunzi wachangamkie fursa ya elimu ya lugha ya Kichina inayopatikana katika chuo chao kwani kimeweza kuwasaidia wanafunzi wengine kufahamu lugha hiyo pamoja na kupata nafasi za kusoma nchini China bure.

Akizungumza na Globu ya Jamii, Afisa Habari wa Chuo cha Muslim Morogoro Ngaja Mussa amesema kuwa wanatoa kozi ya elimu hiyo ya lugha ya kichina kwa wanafunzi wote wanaotaka kuifahamu na pia utakaposoma kwa mwaka mmoja na kuifahamu vizuri lugha hiyo unapata nafasi ya kusoma nchini China.

Ngaja amesema kwa sasa kuna walimu takribani saba wanatoa mafunzo ya elimu hiyo katika chuo chao, mbali na kozi hiyo ya lugha ya Kichina wanatoa pia kozi mbalimbali katika ngazi ya astashahada, stashahada na shahada.

Kwa ngazi ya shahada kwa mwaka 2017/18 wana kozi za Bachelor of Arts with Education pamoja na Bachelor of law with Shariah huku ngazi ya Astashahada na Stashahada wana kozi za Procurement and Logistics Management, Journalism, Medical Labaratory Technology, Science and Laboratory Technology, Laws with Shariah pamoja na Islamic Bankinga and Finance

Chanzo: Michuzi
 
In 20yrs miafrika itakua inaitwa Ping, Xi, Cheng, Yang etc.
 
Elezea usmary wao hata kwa mstari mmoja. Sasa hayo masharia wanayotoa wataenda kuapply wapi.
 
Back
Top Bottom