Pre GE2025 Jimbo la Ukonga ni la mwisho kwa maendeleo Dar es Salaam

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mwangi T.

Senior Member
May 30, 2014
100
57
Pamoja na kuwa jimbo hili limeongozwa na chama twala kwa miaka yote isipokuwa mitano tu tangia nchi ipate uhuru wake lakini bado limekuwa la mwisho kimandeleao jijini Daresalaam!

Kwa Upande wa miundombini hsa barabara imekuwa ndio kilio cha miaka mingi kwa wakazi wa jimbo hili.

Ukiacha barabara kuu ya Nyerere inayotokea mjini kuelekea Pugu na barabara inayoanzia Pugu kuelekea Chanika jimbo halina barabara kabisa!

Hali ni mbaya maeneo ya Kivule-Msongola, hali ni mbaya zaidi maeneo ya Mbondole, Bomba mbili, Zingiziwa, M'bande-Msongola na meneo mengi ya jimbo hili.

Mbunge wetu wa sasa ameendele kujichotea umaarusfukwenye serikali hii ya mama tangu alipokuwa waziri wa ardhi mpaka sasa alipohamishiwa wizara ya habari!

Ingekuwa nafuu sana kwa watu wa Ukonga endapo umashuhuri wa bwana Jerry Silaa mbunge wa Ukonga ungeendana na hali ya maendeleo ya jimbo hili tofauti na hivi ilivyo sasa.

Mwisho niwaombe tu wenye mamlaka juu ya miundombinu mkumbuke pia kuwa hata Ukonga tunaishi binaadamu hata kama Mbunge wetu hatusemei.
 
"JAMII INAYOUMWA HUCHAGUA VIONGOZI WANAOUMWA."
Mkuu kwa namna uchaguzi wa 2020 ulivyofanyika huwezi kusema wana Ukonga tulimchagua huyu Mbunge wetu!
Wananchi waliporwa waziwazi na hadharani haki ya kuchagua kiongozi wao nchi nzima!! Vivyo hivyo na sisi wakazi wa Ukonga hatukumchagua huyu jamaa!

Lakini hata kama hatukumchagua ndo keshakuwa kiongozi wa huku, ingekuwa busara kama angekuwa anatusemea huko serikalini mara kwa mara kuliko ilivyo sasa ambapo anaonekana akijijenga yeye kisiasa zaidi kuliko kulipigania jimbo!!
 
Pamoja na kuwa jimbo hili limeongozwa na chama twala kwa miaka yote isipokuwa mitano tu tangia nchi ipate uhuru wake lakini bado limekuwa la mwisho kimandeleao jijini Daresalaam!

Kwa Upande wa miundombini hsa barabara imekuwa ndio kilio cha miaka mingi kwa wakazi wa jimbo hili.

Ukiacha barabara kuu ya Nyerere inayotokea mjini kuelekea Pugu na barabara inayoanzia Pugu kuelekea Chanika jimbo halina barabara kabisa!

Hali ni mbaya maeneo ya Kivule-Msongola, hali ni mbaya zaidi maeneo ya Mbondole, Bomba mbili, Zingiziwa, M'bande-Msongola na meneo mengi ya jimbo hili.

Mbunge wetu wa sasa ameendele kujichotea umaarusfukwenye serikali hii ya mama tangu alipokuwa waziri wa ardhi mpaka sasa alipohamishiwa wizara ya habari!

Ingekuwa nafuu sana kwa watu wa Ukonga endapo umashuhuri wa bwana Jerry Silaa mbunge wa Ukonga ungeendana na hali ya maendeleo ya jimbo hili tofauti na hivi ilivyo sasa.

Mwisho niwaombe tu wenye mamlaka juu ya miundombinu mkumbuke pia kuwa hata Ukonga tunaishi binaadamu hata kama Mbunge wetu hatusemei.
mbunge wa hovyo kuwahi katika historia, mbinafsi dogo huyu sijui ilikuwaje akapata ubunge, ccm wawe wanachagua watu sahihi kwa wana nchi
 
Kuanzia Moshi bar hadi bomba mbili barabara ni mbovu sana tena sana na haina dalili ya kurekebishwa

Hizi maeneo serikali ni kama wamezikaushia
 
Back
Top Bottom