Ya makinikia yameisha, vipi kuhusu Geita GM na North Mara GM ambao hawana Makinikia?

The Evil Genius

JF-Expert Member
Mar 21, 2014
5,902
19,093
Naoipongeza serikali kwa kumaliza hili jambo la makinikia baada ya wanaohusika kukubali kulipa kitakachokubaliwa na pande zote mbili.

Jitihada nyingi zimeelekezwa kwenye makinikia na imeonyesha kua pesa ambayo tumepoteza kila mtu angekua na Noah yake mpya zero kilomita.

Naomba kujua je hatuna cha kupata au kupokea kutoka kwenye migodi ambayo haina makinikia kama mgodi uliopo Nyamongo wilaya ya Tarime wa North Mara Gold Mine, Geita Gold Mine na mingine ambayo 100% ya dhahabu yake inachenjuliwa hapo hapo mgodini?.

Mods hii mada inajitegemea.
 
Mkuu hiyo migodi uliyotaja hapo haizalishi concengtrate (Makinikia)
Kwa hiyo dhahabu iko nyingi kwenye makinikia kuliko huko ambako hakuna makinikia?

Na kwenye migodi inayozalisha makinikia, kama makinikia yana thamani kubwa hivyo, je ile ambayo imechenjuliwa mgodini itakua na thamani kubwa kiasi gani?
 
Mleta mada una hoja ya msingi, mikataba YOTE ya madini inapaswa kupitiwa upya tena na team maalum huku nje ya bunge.
Ikikamilika ipelekewe hao vilazaz waipitishe (wasiguse kitu wataharibu!) then ipelekwe kwa rais iwe sheria.
 
Kwa hiyo dhahabu iko nyingi kwenye makinikia kuliko huko ambako hakuna makinikia?

Na kwenye migodi inayozalisha makinikia, kama makinikia yana thamani kubwa hivyo, je ile ambayo imechenjuliwa mgodini itakua na thamani kubwa kiasi gani?
Sio hivyo mkuu grade ya madini (dhahabu, silve, copper) yaliyopo kwenye makinikia hua ni kubwa kuliko yale mawe unayotoa mgodini (Mineral Ore) kwa sababu makinikia unakua ushaondoa uchafu ambao unakua umjichanganya kutoka mgodini.
Ndo maana kuna sehem za wachimbaji wadogo (small scale) wanachenjua wakishaweka mabaki pembeni (concentrate) watu wenye hela nyingi wanaenda kununua na kuchenjua mara ya pili kwa kutumia technology nzuri/kubwa zaidi na wanapata dhahabu nyingi.

Ndo maana unaona kuna dhahabu, silver na copper nyingi kwenye makinikia
 
Back
Top Bottom