Ya loliondo na uchumii wetu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ya loliondo na uchumii wetu

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Kingo, Mar 19, 2011.

 1. Kingo

  Kingo JF-Expert Member

  #1
  Mar 19, 2011
  Joined: May 12, 2009
  Messages: 791
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 60
  Nimekuwa nikifuatilia hoja na michango mbalimbali ya wadau katika vyombo vya habari, mitaani na hapa jamvini. Wengi wamemsifu Babu wa Loliondo kwa tiba "ya imani", lakini wengine wamedai haiwezekani kwa dunia ya sasa kuendelea na tiba za "kijima" za namna ile (tiba za ndoto). Kwa waliopona, kila la kheri.
  Sasa utata unakuja, kama tiba ya babu ni ya kijima na haina nafasi katika ulimwengu wa sasa wa sayansi na teknolojia, je uchumi wetu uko wapi? Ni jana tu Mh Mkullo katuambia kuwa uchumi utaporommoka mwezi ujao... na kukua mwishoni mwa mwaka huu! Hiyo afadhali, sasa kwenye mgao wa umeme ndo balaa. Maana tunaambiwa mpaka mvua zinyeshe, mambo yataendelea kuwa magumu na nchi inaweza kuingia gizani! Je huo si uchumi wa kubashiri kwa ndoto na wa kijima?
  Jua la kitropiki tunalo, upepo upo wa kutosha, gesi asilia tunayo, uranium tunayo, (watadakia teknolojia hatuna au duni) makaa ya mawe tunayo, (japo danadana) na vyanzo vya maji vingi tu. Sasa inakuwaje Babu wa Loliondo alaumiwe kwa tiba asili ati ya kijima wakati uchumi wetu unategemea mvua ya utabiri? Kwanini uchumi wetu usiendane na wakati uliopo wa sayansi na teknolojia? Mbona nchi zilizo katika kingo za Jangwa la Sahara (Sahel) hazina mvua za kutosha kwa mwaka lakini migawo ya umeme sijawahi sikia?
  Mi nadhani tatizo ni sera na vipaumbele vianvyotolewa na wanasiasa wetu. Huwezi kutenga almost 75% ya mapato ya nchi kwa matumizi ya kiutawala ya serikali na inayobaki almost 25% ndo bajeti ya maendeleo! Ukakimbia kuita wawekezaji(?) wakati nyenzo muhimu katika uwekezaji kama umeme ni tabu! Ukakimbilia kujenga skyscrapers and flyovers wakati miji haina maji safi na salama kwa nchi inayoongoza barani Afrika kwa vyanzo asili vya maji!
  Ukakimbilia kununua maVX na maVogue ya mabilioni wakati miundombinu ya kuyapitisha na kuegesha ni duni. Ukahesabu pato la wateule wachache ukasema uchumi unakua kwa kasi wakati mamilioni hawana hata senti, wanashindia t-shirt walizogawia wakati wa kampeini.
  Kila mwaka Wizara zinaomba bajeti ya miradi (mingine mipya) lakini mwaka ukiisha hamna anayehakiki utimillifu wa miradi hiyo, pesa inatolewa nyingine, mnabaki na miradi hewa na hela imetafunwa. Kila waziri anaingia na sera yake kana kwamba hatuna dira ya taifa ya maendeleo (RAMANI). Watu wanadunda, siasa inalipa, halafu tunasema kikombe cha Babu wa Loliondo ni ujima!
  Ni mawazo tu.
   
 2. m

  mambomengi JF-Expert Member

  #2
  Mar 19, 2011
  Joined: May 16, 2009
  Messages: 829
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Nilipendekeza kwa serikali kukusanya kodi ya huduma inayotolewa na babu, usafiri, chakula na malazi. Serikali imepoteza pesa nyingi sana ambazo zingetumika kuendeleza kijiji cha Babu na miundombinu yake. Lakini watendaji serikalini wamelala!
  Chukulia mfano babu akifanikiwa kutibu watu milioni moja, atapaswa kulipa kodi Sh. mil. 100. Watoahuduma pia wamepandisha bei ya huduma zao....serikali inaweza kukusanya zaidi ya Sh.Mil 250, nakufanya hesabu za haraka haraka kufikia milioni zaidi ya 350.
   
 3. Smarter

  Smarter JF-Expert Member

  #3
  Mar 23, 2011
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 455
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mawazo mazuri ingawa Practically ni ngumu.....Bado hatujawa efficiency kutekeleza hili....kuna vyanzo vingi tungeweza ku focus for now...................Kwa haraka unadhani serikali inaloose Sh ngapi kwa Babu...............Zungumzia Msamaha wa Tax kwa wawekezaji uchwara na Grace period ya TAX kwa wawekezaji, Madini, Ernegy nakadhalika kwanza then BABu mwisho
   
Loading...