Ya lema & mnyika na siasa zetu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ya lema & mnyika na siasa zetu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Bilionea Asigwa, May 26, 2012.

 1. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #1
  May 26, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,627
  Likes Received: 9,838
  Trophy Points: 280
  Mbinu ambazo CCM imekua ikitumia katika siasa zake zimekua zikibadilika sana, Mbinu kama UENEZAJI WA PROPAGANDA dhidi ya upinzani(kama ya CUF na UDINI au CHADEMA na UKANDA au NCCR ya MREMA na UMAMLUKI), zimefanikiwa kwa muda lakini sasa zinaonekana kuanza ku fail hasa kutokana na mwamko wa wananchi katika kufuatilia siasa au labda uwezekano wa wananchi kutaka tu mabadiliko..

  Mbinu nyingine ilikua ni kuwavua ubunge wabunge wa upinzani walioonekana wana mvuto sana katika maeneo yao kwa kutumia mahakama.. mfano ya LEMA, walicho kuwa wamepanga kwa LISU na hata kwa MNYIKA.. Mbinu hii ilionekana ni nzuri sana kwao lakini HASARA NI KUBWA KULIKO FAIDA...Uwepo wa mtu kama LEMA nje ya bunge umeonekana kukipa nguvu sana CHADEMA mikoa ya ARUSHA, MANYARA, KILIMANJARO na mikoa ya KANDA YA ZIWA karibu yoote na kuifanya kugeuka ngome ya upinzani

  Kama wangefanikiwa kuwanyofoa LISU na MNYIKA bungeni basi mikoa ya KANDA YA KATI, MIKOA YA PWANI ingekumbwa na kimbunga kama cha kule kwa LEMA na ingegeuka kuwa ngome ya upinzani vile vile...kama mnavyojua mikoa kama SINGIDA, DODOMA, PWANI , DAR ES SALAAM na mingine bado ina WANAZI wengi walioikumbatia ccm wengi wao wakiwa ni kwa sababu ya upofu wao tu, siku wakifumbuliwa macho wanaweza kukitosa CCM forever kama kilivyotoswa KWA LEMA...

  MY OPINION
  Njia aliyoionesha LEMA, SUGU na MCH MSIGWA kwa kujikita katika maeneo walikotoka inafaa sana kutumiwa na MNYIKA , LISU na KABWE katika kuibomoa CCM katika mikoa ya kati,pwani na baadhi ya MIKOA YA MAGHARIBI ambako bado CCM inapumulia PUA MOJA...Staili hii ni nzuri hasa ukizingatia kuwa MAJEMBE haya yana mvuto sana katika maeneo hayo, na karibu woote bado ni vijana sana wanaweza kushuka mpaka vijijini kule ndani kabisa bila bugdha za umri...

  NI MAWAZO YANGU TUU
   
 2. Bado Kidogo 2015

  Bado Kidogo 2015 JF-Expert Member

  #2
  May 26, 2012
  Joined: May 24, 2012
  Messages: 207
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu hao mabwana hazina yao imekauka ndiyo maana wamekubali yaishe lakini kama ingekuwa imetuna kama kipindi kile Ben kaiacha nchi wangepigwa chini ili kuwachanganya wananchi na wenyewe wabunge.

  Ukifikiri CCM wanahaya utakuwa umekosea sana, akili zao zinawatosha kuvuka reli tu ukimleta avuke barabara jua umemchanga na kumpa mtihani mkubwa sana!!!!
   
 3. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #3
  May 26, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,627
  Likes Received: 9,838
  Trophy Points: 280
  Ila kama wanauezekano wa kulipa gharama za kesi na bado gharama za uendeshaji wa kesi kma ya mnyika kwa serikali ni kama biliioni moja..huoni kuwa pesa kwao si tatizo,..ila tu mambo yako tyte upande wao wa kisiasa
   
 4. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #4
  May 26, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,197
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Mkuu asigwa Baada ya mkutano wa leo kanda ya pwani ndio inaanza kuyoyoma kwenda upinzani CCM wataanza kupumulia machine muda si mrefu
   
 5. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #5
  May 26, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,705
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  CCM inapumulia machine kwenye chumba cha maututi,

  CHEZEA LEMA WEYEEEEEEE!
   
 6. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #6
  May 26, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,627
  Likes Received: 9,838
  Trophy Points: 280
  YAP Ni kweli kama unachokisema maana najua nguvu kubwa zaidi inahitajika huku PWANI kuliko mikoa mingine maana unazi bado mwingi sana ukilinganisha na miko mingine
   
 7. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #7
  May 26, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Na Nassari anaeneza propaganda za CCM?
   
 8. chuki

  chuki JF-Expert Member

  #8
  May 26, 2012
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,691
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Unajenga gorofa hewani eeehh!!
  fuatilia Mwanza Mjini ujue kinachoendelea leo.

  "Chadema kinakufa kabla ya 2015"-Wasira
   
Loading...